Tofauti na hoja ya viti maaluma huna hoja nyingine yoyote ya msingi.
Kuhusu wanawake kupata nafasi za upendeleo katika masomo ni sahihi kwa sababu jamii nyingi hasa za vijijini hazikuthamini masomo kwa mtoto wa kike kwa muda mrefu hivyo serikali inachofanya ni kusahuhisha hiyo injustice ya muda mrefu. Kuna visa vya watoto wa kike wanaambiwa wafeli mitihani ya darasa la saba makusudi ili waolewe.
Hivi ni vitu gani unaandika wewe mbona kama haujatumia hekima hata kidogo ingawa unataka kuonekana mwenye hekima?!
Sasa nikuulize swali la kikuda, unataka kuniambia kwasababu kuna changamoto za kijamii zinazosababisha watoto wa kike kushuka kielimu basi suluhu ni kuwawekea vigezo legezi ili wapitishwe lengo likiwa ni kuonyesha matokeo chanya katika makaratasi ya wizara ila vipi uhalisia wa matokeo ya kiufanisi?
Wewe umeambia taaluma zinataka watu wanaobebwa?! Mfano mtu anatamani kuwa daktari ila hana uwezo wa kushika masomo ya udaktari nini unategemea kitokee hapo?!
Si ndio mwisho wa siku tunapata watu wanaokalia taaluma ambazo hawana weledi nazo?!
Kitu ambacho watanzania tumekuwa na vichwa vizito kujifunza ni kutokujifunza na makosa.
Miaka ya nyuma wizara ya elimu waliamua kwa makusudi kushusha vigezo vya watu kusomea Ualimu. Wakaweka vigezo vya chini kabisa kwamba mtu akiwa hata na division 4 atapata kazi ya Ualimu na mkopo juu.
Fast Forward leo hii. Hivi unaona namna elimu inavyozidi kudidimia sababu ya maamuzi ya kipumbavu kama yale. Na watu walikemea sana lile jambo wakasema kwann tusilimi watu kwenda ualimu mwisho iwe division 2. Watu wakatoa sana kauli za kishujaa bila kuwazia hatima ya taifa miaka 100 ijayo.
Leo miaka hata 20 haijapita tumeanza kuvuna hasara. Idadi ya walimu imekuwa kubwa kupita uwezo wa serikali kuajiri.
Walimu wenyewe wengi wanapata udahili kwa vigezo vya chini na matokeo skills zao ni questionable.
Leo serikali inalazimika kutengeneza shule nyingi ili kuajiri walimu ambao kiuhalisia haiwezi wamudu kuwalipa kwa wingi wao.
Impact ipo wapi tukitazama wanafunzi wetu wa sasa unaweza linganisha na wale wa miaka hiyo ya nyuma. Wanafunzi wa sasa wana low but very poor academic performances.
Haya ni matokeo ya maamuzi ya kipumbavu ambayo hayalengi kufanya maboresho bali ni kutokana na upotofu wa akili.