Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Nchi inaendeshwa kwa kufuata katiba. Rais akiamua kutumia madaraka yake unavyotaka si tutarudi kwenye mambo ya awamu ya 5? Vyombo vya dola ndo vinatakiwa viwakamate wahusika na kuwapeleka mahakamani. Tukisema Mama aanze kutumia ubabe hakutakalika. Tumshukuru sana kwa kuamua kufuata utawala wa kisheria.
Ona huyu chawa!! Takataka kabisa, kuagiza polisi kuwakamata na kuwahoji watuhumiwa ni ubabe?

Hii nchi inahitaji kiongozi dikteta over
 
Tatizo la mama ni kutaka kuonekana mwema machoni pa kila mtu. Pia anaogopa kufuata nyayo za mtangulizi wake maana ashaonekana mara nyingi akimkataa. Sasa amejikuta haelewi nini afanye hivyo anajiendea tu.
 
Sasa Mkuu... Utawasimamisha wangapi uache wangapi? Rais mwenyewe anakwambia yanaanzia ndani hayo!
Zamani kipindi hatuna uhakika wa sabuni chawa walikuwa ni marafiki zetu. Sasa ukiwa hujui mtabaki kama nyani wale wanavofanya leo mnaanza kutafuta chawa mmoja mmoja. Nakwambia walikuwa hawaishi asee.
Wazazi wenye akili walikuwa wanachukua nguo zote na kuziloweka kwenye maji moto. Basi mtakuwa na amani kwa muda kadhaa!
Hiyo ndo overhaul ninayozungumzia... Yaliyopo kote kote TTCL, TRC, ATCL, BANDARI, TRA, Benki, etc ni matokeo ya mfumo.
Ondoa mfumo ulete unafuu
KUONDOA Mfumo wa kishenzi ni kufukuza wachache kama mfano. Mbona nchi ilitulia na hospitali watu walipokelewa kama hotelini.
Ila kitendo cha yule bwana kufa tu sahizi pharmacy zote za hospitalini hazina dawa hadi ukanunue nje.
 
Kuna mfano tu huu nimekumbuka
Kuna tajiri mmoja alikuwa na mfanyakazi wake ila huyu jamaa mwisho alikuja kuwa mwizi anamuibia sana tajiri wake

Na tajiri hamfanyi kitu ila mambo yalizidi kuwa mabaya tajiri akabanwa na ndugu ikabidi amsimamishe kazi
Sasa wanako hawakunyamaza na siri wanaijua

Hayo tuyaache nimefunga
Ila mnaweza kujaza wenyewe maana wabongo tunajuana nionyeshe trailer makuhadithia picha lote kabla sijaliona

Sasa hawa waizi ndio hawa hawa wanaohakikisha wazidi kuwepo madarakani
Na hela hizo ndio zingine mnapewa vitenge na kofia

Wanajuana sana na siri wanazo wao hamtasikia watu wanafungwa
Ilitokea ya kina Yona basi no more
 
Sasa Mkuu... Utawasimamisha wangapi uache wangapi? Rais mwenyewe anakwambia yanaanzia ndani hayo!
Zamani kipindi hatuna uhakika wa sabuni chawa walikuwa ni marafiki zetu. Sasa ukiwa hujui mtabaki kama nyani wale wanavofanya leo mnaanza kutafuta chawa mmoja mmoja. Nakwambia walikuwa hawaishi asee.
Wazazi wenye akili walikuwa wanachukua nguo zote na kuziloweka kwenye maji moto. Basi mtakuwa na amani kwa muda kadhaa!
Hiyo ndo overhaul ninayozungumzia... Yaliyopo kote kote TTCL, TRC, ATCL, BANDARI, TRA, Benki, etc ni matokeo ya mfumo.
Ondoa mfumo ulete unafuu
Mkuu mimi najua kwamba ni vigumu kwa nchi yoyote kutokomeza wizi serikalini. Hata huko Marekani kwenye mifumo bora ya uongozi, leo hii unasikia raisi mstaafu wa taifa hilo Donald Trump anataka kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa sababu zinazofanana na hizi tunazozungumzia hapa.

Ila sasa pamoja na kwamba ni vigumu kudhibiti wizi serikalini kwa 100%, kuna njia ambazo zinaweza kutumika japo kupunguza wizi huo kwa kiasi kikubwa na watu hawatokuwa tena wanailalamikia serikali kama ilivyo sasa. Ukisoma vizuri nilichoandika huko juu utanielewa.

Kwamba mtu anapopatikana na hatia ya wizi serikalini kitu cha kwanza kinachotakiwa kufanywa na raisi, waziri au kiongozi wake ni kumsimamisha mtu huyo na kuagiza akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

1) Ikionekana kwamba mhusika hausiki na wizi bali alitengenezewa tu zengwe pengine kutokana na utendaji wake mzuri wa kuzuia upigaji, basi arudishwe kazini na ikiwezekana apandishwe cheo ili kutoa motisha kwa wengine kusimamia vyema maeneo yao ya kazi.

2) Ikionekana kweli aliiba basi afutwe kazi amepelekwe mahakamani ahukumiwe kifungo cha muda mrefu au arudishe fedha zote alizoiba na nyingine ya juu kama fidia ya wizi wake aliofanya.

Ikiwa tutakwenda kwa mwendo huo wengi wataogopa kuiba, na hivyo kupelekea wizi kupungua au kuisha kabisa serikalini.
 
Nchi inaendeshwa kwa kufuata katiba. Rais akiamua kutumia madaraka yake unavyotaka si tutarudi kwenye mambo ya awamu ya 5? Vyombo vya dola ndo vinatakiwa viwakamate wahusika na kuwapeleka mahakamani. Tukisema Mama aanze kutumia ubabe hakutakalika. Tumshukuru sana kwa kuamua kufuata utawala wa kisheria.
Swali langu kwako mwaka uliopita walichukuliwa hatua gani?
 
Ripoti ya CAG sio hukumu ya Mahakama,ikithibitika hatua zitachukukiwa..

Kumbuka Rais Samia sio mtu wa mihemko,kukurupuka na ku loose temper kirahisi ,ukifanya hivyo anaweza umiza wengi.
Basi kama ni hivyo aache kulalamika
 
Binafsi naona vyama vyote Tanzania au Afrika vimeanzishwa kwa lengo kutafuna fedha za wananchi, ndomaana ukivichunguza hata uendeshaji wao ni wa upigaji upigaji.

Cha kufanya ni kuwa na wagombea huru ambao watagombea uongozi bila kupitia chama chochote cha siasa. Maana wanasiasa wote ni wezi, waongo na wanafiki.
unafikiri hao wagombea binafsi sio wanasiasa? au unafikiiri wanatoka nje ya Africa. suluhisho ni kuwa na katika bora inayoweza hata kumwajibisha Rais aliyepo madarakani, inayoipa nguvu mihimili mingine hasa Bunge na mahakama bila hivyo hata Malaika waje waongoze hii nchi watageuka kuwa mashetani
 
Nchi inaendeshwa kwa kufuata katiba. Rais akiamua kutumia madaraka yake unavyotaka si tutarudi kwenye mambo ya awamu ya 5? Vyombo vya dola ndo vinatakiwa viwakamate wahusika na kuwapeleka mahakamani. Tukisema Mama aanze kutumia ubabe hakutakalika. Tumshukuru sana kwa kuamua kufuata utawala wa kisheria.
Vyombo vya usalama vinashindwa au naweza kusema vinaogopa kuwakamata kwa sababu havina watu madhubuti wa kuwalinda.

Kwahiyo acha raisi mwenyewe achukue maamuzi yanayowashinda wa chini yake. Yeye ndio bosi wa serikali na mwenye maamuzi ya mwisho kwa mtu yoyote mwenye tuhuma za wizi au ufisadi.
 
unafikiri hao wagombea binafsi sio wanasiasa? au unafikiiri wanatoka nje ya Africa. suluhisho ni kuwa na katika bora inayoweza hata kumwajibisha Rais aliyepo madarakani, inayoipa nguvu mihimili mingine hasa Bunge na mahakama bila hivyo hata Malaika waje waongoze hii nchi watageuka kuwa mashetani
Nakubaliana na mia kwa mia
 
CCM ni janga kubwa Sana hapa nchini.

Solution ya hiyo "laana" ni kuipiga chini CCM katika uchaguzi ujao

Hayo ni maneno ya kila Mwaka, miaka nenda miaka rudi. Bila katiba mpya na Uchaguzi huru KAMWE CCM haitatoka madarakani

Na sasa F. Mbowe anaunga juhudi uongozi huu usitegemee chochote tena

Labda Rais aamue kuwa mkali na kutumbua wabadhirifu wote

Vinginevyo Hamna kitu hapa.
 
Back
Top Bottom