Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Unajua kwenye uongozi Kuna muda unatakiwa ufanye maamuzi magumu kwa mustakhabali wa wengi. Sasa unaposhindwa kufanya hivyo ndiyo hayo madudu hutokea na huendelea kutokea kwa kuwa walio chini yako wanakufahamu jinsi ulivyo.

Tutoe mfano mdogo kwenye kumkataa mzabuni wa Bilioni 616, afu mnamkubali wa Trioni 1.16 uko kwa akili ya kawaida tu at ungekua ww ndiye biashara yako unamchagua nani hapo. Itoshe kusema upigaji umezidi na utaendelea kama Rais hatachukua hatua za makusudi kuweza kulizuia au kulipunguza

Hayo tunayoelezwa na CAG huenda ni machache kati ya mengi, lakini pia tujiulize tutaenda ivi hadi lini jamani yaani sisi tunashindwa at kujifanya wazalendo kiunafiki tukaziba mengne

Tanzania tuna safari ndefu sana ya maendeleo kwa staili hii viongozi punguzeni wizi na upigaji aisee.

Tanzania imeshakua nchi ya mchongo, viongozi nao ni wamchongo wanaendelea kupiga michongo. Tunaoumizwa ni watu wa chini afu et unataka tulipe Kodi kwa maendeleo yetu au ni kwa maendeleo yenu jamani

Ukiangalia at adhabu wanaozitunga Zina upendeleo kwao mtu mnajua kabisa kafanya kosa et mnasema muhamisheni kituo kweli badala ya kulifunga jela ***** mnaleta sera za kulindana tu

TANZANIA BADO TUNA FAMASIKHARA TU.
 
Watu wanaoiba kuku kitaa wanafungwa ila wanaoiba mabilioni ya uma wanaachwa hatar sana!
Saivi tunataka watuachie Wananchi tuwalete kwenye Mahakama zetu za kitaa tuwape kichapo kidogo labda akili zitawakaa sawa ***** hao viongozi wapigaji na Wezi waliowashindwa wao
 
KWANZA HIVI NDIO VYEO VYAKE

1) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Mkuu wa nchi na kiongozi namba moja kwa pande zote mbili za Muungano.
3) Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa Rais kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.

Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake Rais eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo ili zikatumike katika mambo mengine ya kimaendeleo.

Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.

Yani mwizi wa ndala akamatwe na kufungwa huku mwanasheria wa serikali akitafuna kodi zetu kwa kuendesha kesi yake, afu yule anayeiibia serikali mabilioni ya shilingi ahamishwe tu kituo ili akaendelee na utafunaji wa fedha zetu huko katika ofisi nyingine. Ni kwanini asifukuzwe kazi ili nafasi yake ichukuliwe na mtu mungine na ukizingatia kuna watu wengi wana elimu zao mitaani lakini kazi hawana?

Lakini pia sio aishie kufukuzwa tu bali afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na mali zake zote zitaifishwe na kurudishwa katika mikono ya wananchi.

China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi hiyo kusimamia vyema kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali. Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.

Rais na amiri jeshi mkuu ukibaki kulalamika, unafikiri mawaziri na viongozi wengine wa kawaida wataweza kuwa na uwezo wa kujiamini kuchukua hatua kweli.

Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.

Hebu tumia nguvu zako ulizopewa na katiba yetu kuwachukulia hatua wabadhilifu wa kodi zetu, kabla na sisi hatujaingia barabarani kama wakenya.

Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
Rais mwenyewe kuna watu wanaompigania aendelee kuwepo pale.., na walewale wanaompambania wana watu wao wanaopiga kadri wawezavyo.., nguvu ya kuwawajibisha anaitoa wapi. Kelele zake ni sawa na mbwa anayebweka saaana lakini hamuumi mwizi, mwizi anaiba then anaondoka na kesho yake mwizi anarudi tena mbwa yule anabweeka tena tena saaan, lakini mwizi anaiba nakuondoka daaaah yataka Moyo sana kuishi kwenye hii Nchi.
 
Nimesononeka baada ya kusema hao wapigaji waondolewe sehemu zenye ulaji mwingi wapelekwe sehemu zisizona neema ili wakapate tabu kidogo

Kwanini wasishitakiwe?
Labda katiba haimruhusu kuwaondoa na kuwashitaki ?! Maajabu haya !! Huku zinakopwa maana tunakopesheka na huku zinagegenwa na wajanja wa mjini !! So sad 😞
 
KWANZA HIVI NDIO VYEO VYAKE

1) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Mkuu wa nchi na kiongozi namba moja kwa pande zote mbili za Muungano.
3) Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa Rais kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.

Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake Rais eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo ili zikatumike katika mambo mengine ya kimaendeleo.

Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.

Yani mwizi wa ndala akamatwe na kufungwa huku mwanasheria wa serikali akitafuna kodi zetu kwa kuendesha kesi yake, afu yule anayeiibia serikali mabilioni ya shilingi ahamishwe tu kituo ili akaendelee na utafunaji wa fedha zetu huko katika ofisi nyingine. Ni kwanini asifukuzwe kazi ili nafasi yake ichukuliwe na mtu mungine na ukizingatia kuna watu wengi wana elimu zao mitaani lakini kazi hawana?

Lakini pia sio aishie kufukuzwa tu bali afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na mali zake zote zitaifishwe na kurudishwa katika mikono ya wananchi.

China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi hiyo kusimamia vyema kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali. Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.

Rais na amiri jeshi mkuu ukibaki kulalamika, unafikiri mawaziri na viongozi wengine wa kawaida wataweza kuwa na uwezo wa kujiamini kuchukua hatua kweli.

Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.

Hebu tumia nguvu zako ulizopewa na katiba yetu kuwachukulia hatua wabadhilifu wa kodi zetu, kabla na sisi hatujaingia barabarani kama wakenya.

Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
Rais atangaze msamaha kwa wafungwa wa wizi maana waalimu wao bado wapo maofisini na wanalamba teuzis
 
Saivi tunataka watuachie Wananchi tuwalete kwenye Mahakama zetu za kitaa tuwape kichapo kidogo labda akili zitawakaa sawa ***** hao viongozi wapigaji na Wezi waliowashindwa wao
Mwizi aliyekwapua simu anachomwa moto ! Wezi wa $49m wanaambiwa pumbafu !! Imeisha hiyo !! Mungu anatuona Kwakweli !! Karma !
 
Labda katiba haimruhusu kuwaondoa na kuwashitaki ?! Maajabu haya !! Huku zinakopwa maana tunakopesheka na huku zinagegenwa na wajanja wa mjini !! So sad 😞
Kukopa tukope sisi, kulipa tulipe sisi, lakini kuliwa ziliwe na wengine. Inasikitisha sana.
 
Unategea CCM ipambane na ubadhirifu...tangu lini kwa mfano?
 
Rais atangaze msamaha kwa wafungwa wa wizi maana waalimu wao bado wapo maofisini na wanalamba teuzis
Mwizi wa ndala muendesha kesi wa serikali anaomba afungwe hata miaka miwili ili iwe fundisho kwa wezi wa ndala wengine.

Mwizi wa mabilioni ya kodi zetu anahamishwa ofisi kutoka wizara ya mifugo na kupelekwa wizara ya fedha au ya michezo.
 
Nchi inatetemeka kwa ujambazi wa watawala
 
Tunaolalamika na kuumia ni sisi ambao hatupo kwenye huo mfumo wa wizi, lakini wanaonufaika na huo wizi ndio hao kila siku wanasifu na kuabudu mama anaupiga mwingi, nani kama mama
KWANZA HIVI NDIO VYEO VYAKE

1) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Mkuu wa nchi na kiongozi namba moja kwa pande zote mbili za Muungano.
3) Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa Rais kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.

Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake Rais eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo ili zikatumike katika mambo mengine ya kimaendeleo.

Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.

Yani mwizi wa ndala akamatwe na kufungwa huku mwanasheria wa serikali akitafuna kodi zetu kwa kuendesha kesi yake, afu yule anayeiibia serikali mabilioni ya shilingi ahamishwe tu kituo ili akaendelee na utafunaji wa fedha zetu huko katika ofisi nyingine. Ni kwanini asifukuzwe kazi ili nafasi yake ichukuliwe na mtu mungine na ukizingatia kuna watu wengi wana elimu zao mitaani lakini kazi hawana?

Lakini pia sio aishie kufukuzwa tu bali afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na mali zake zote zitaifishwe na kurudishwa katika mikono ya wananchi.

China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi hiyo kusimamia vyema kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali. Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.

Rais na amiri jeshi mkuu ukibaki kulalamika, unafikiri mawaziri na viongozi wengine wa kawaida wataweza kuwa na uwezo wa kujiamini kuchukua hatua kweli.

Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.

Hebu tumia nguvu zako ulizopewa na katiba yetu kuwachukulia hatua wabadhilifu wa kodi zetu, kabla na sisi hatujaingia barabarani kama wakenya.

Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
 
Cag na yeye atafute chance apige sio tu akae kazi yake kuorodhesha wapigaji..kazi hi imekuwa haina thamani tena.
 
Hii nchi sasa ishakua mtihani, watu wanaiba mabilioni ya fedha na hawafanywi lolote..
Wamepewa vyeo ili kuiba kuna watu walitumbuliwa kwa wizi na kuhujumu nchi, leo hii wepewa nafasi ya mahamuzi, mfano Mwanasheria mkuu wa serikali alitumbuliwa na Magufuli kipindi tu Magufuli anaingia Ikulu alianza na huyu Feleshi na Hosea, huyu Feleshi alikuwa mkurungezi wa mashtaka alihujumu kesi ya Samaki wa Magufuli leo hii kapewa cheo cha Mwanasheria mkuu wa serikali.
 
unafikiri hao wagombea binafsi sio wanasiasa? au unafikiiri wanatoka nje ya Africa. suluhisho ni kuwa na katika bora inayoweza hata kumwajibisha Rais aliyepo madarakani, inayoipa nguvu mihimili mingine hasa Bunge na mahakama bila hivyo hata Malaika waje waongoze hii nchi watageuka kuwa mashetani
Hivi mtu aliyeiba biloni 300 utampeleka mahakamani ashindwe kwenye nchi ya kijamaa yenye mabepari walioko madarakani na wananchi wanaowaza kuwa mabepari.
Rushwa itahamia kwenye taasisi zitakazomchunguza na mahakamani . Hakimu Gani anayetaka kuwa maskini wakati anaona majaji ni mabilionea?
Polisi Gani au Takukuru Gani anayetaka kuwa maskini wakati serikali haiwezi hata kufidia familia yake anapokufa akiwa anapambana na majambazi au anapokuwa mlemavu Hana fidia maalumu ya kuhakikisha anaishi maisha mazuri pamoja na ulemavu wake ? Polisi mwadilifu akistaafu anachekwa na jamii nzima na KUONEKANA kuwa ana laana ya kudhulumu watu. Yaani waliofanya ufisadi wakapata fedha nyingi wao ndio jamii inawaona kuwa walikua wema na Mali walizo nazo ni baraka ya wema wao. Jamii isiyojua watu wema haiwezi kutoa viongozi Bora . Anahitajika mtu mmoja madhubuti atakayeitengeneza njia. Mtu mmoja ataifanya jamii kuwatambua na kuwatofautisha watu wa baya na watu wema.

Nchi kama hii hahitaji TU Bora peke yake Bali mtu mmoja anayeweza kuwanyoosha wahuni. Na kuhakikisha watu wanaogopa kuchezea Mali za umma.
JPM aliweza Kwa kiasi Fulani kupambana na wahuni japo wahuni walikua na mtandao mpana sana mana wamejikita kila Kona ndani ya Chama na serikali na wamejineemesha Kwa kiwango kikubwa sana . Wanaweza kuhonga yoyote . Hii nchi inahitaji Rais dikteta kamili. Anayeweza kutembeza chuma Kwa watu hata laki Moja. Yaani atakayesafisha mafisadi na wezi na vizazi vyao vyote bila hofu.
Yaani akijua kuwa Jaji amekula rushwa akatoa hukumu ya kumsafisha fisadi naye ananyooka naye. Kule Kenya tunaona majaji wanavyotumika kuidhoofisha serikali na kuwahalalisha mambo ya hovyo na Sasa kuhalalisha ushoga ,maandamano yasiyo na umuhimu wowote na yanayoweza kulifanya taifa kuwa kama Libya na wote wakaumia na nchi ikaporomoka kabisa kiuchumi .

Vinginevyo tukubali kuwa hakuna wa kumnyooshea mtu kidole zaidi ya Kuruhusu Demokrasia ifanye kazi Kwa uwazi na watu wabadili Chama ili wabadili sura za walaji na huenda watu wema nao wakaonekana.
Watu wengi wanachaguliwa au kuteuliwa kupitia connection ya kujuana na urafiki na undugu. Lakini connection nyingi zinapatikana kwenye starehe kama pombe ,uzinzi n.k. Hakuna connection nje ya hapo labda undugu na urafiki. Sasa kama mtu alimuunganisha mtu akateuliwa Kwa sababu ya ni kampani yake ya pombe au ni demu wake au mpenzi wake unategemea Kuwa Kuna uwajibikaji hapo ?

Faida ya kubadili Chama ni kubadili walaji na marafiki zao na jamaa zao Huko nako wanapeana Walevi na mahawara .
Kama sio Udikteta basi pawe na Demokrasia nje ya vyama vya siasa , angalau hapo kidogo inawezekana wakaanza kujitokeza watu wenye Nia njema na waadilifu wakajipenyeza.

Tumeona Kenya Raila na Uhuru wameungana kulinda Mali zao na familia zao dhidi ya Ruto anayeonekana kukerwa na watu waliopora Rasilimali za umma Kwa muda mrefu.

Chama kama Chadema na CCM ukiviangalia namna vinavyoendeshwa ni ubadhirifu mtupu. Yaani wamelenga Kupiga pesa tuu . Usione sijui mikutano sijui maandamano ni wizi mtupu. Kuna watu wanawaza kuuza tishrt, bendera, posho za safari, scafu, vitenge, majora ,kupamba majukwaa lakini sio kujenga ofisi rasmi na kuweka mitandao ya kuweza kujitangaza Chama kimtandao kama CCM ilivyokuwa Miaka ya 80 na ujenzi wa maofisi na maukumbi nchi nzima mpaka Leo ni Mali za Chama.
Sasa watu wanaowaza kuchwa kutwa maandamano na safari za kufanya mikutano hata wakiingia Ikulu watawaza hayo hayo mana hayana faida Kwa jamii zaidi ya kujinufaisha Kwa posho za safari na kumaliza fedha za taasisi au Chama.

Leo mtu akiiba ndani ya Chadema akafukuzwa atakimbilia CCM na ataonekana wa maana anaweza akatumiwa kwenye kampeni na kuwaponda wapinzani . Akiiba ndani ya CCM atahamishwa idara alimradi akae kimya ale urefu wa kamba yake.

Tuna watu wabunge 19 walisio na vyama kinyume na katiba ya nchi na kanuni za Bunge wanalipwa mabilion ya fedha ambazo zingetumika Kununua nafaka na kuweka kwenye ghala la serikali ili mahindi yasipande Bei lakini Bunge na mahakama ndio vimetumika kuhalalisha wizi na ufisadi huo. Sasa hapo katiba ndio mbovu au watu waliopewa dhamana ndio wabovu.
 
Mifumo ipi mkuu? Kwamba raisi kumsimamisha kazi au kumfukuza kazi mtu alietafuna fedha za umma na kuagiza vyombo vya ulinzi vimkamate na kumhoji na ikiwezekana afikishwe mahakamani nayo inahitaji kubadilisha mfumo?
Mkuu anazungumzia mfumo maanisha mfano Waziri kaiba pesa PCCB wanaweza kumkamata na kumshtaki bila kuwasiliana na Rais? Au Katibu mkuu kiongozi kafanya ufisadi je mkurungezi anaweza akamfungulia mashtaka bila kumuomba kibali Raisi?
 
Nchi hii kila Mtu anajichukulia anavyotaka

Ni kama vile Wenye mamlaka hawana nguvu yoyote
DDP, PCCB , AG, wote wamewekwa kwa kusudi la kulinda wezi tu, siku DDP au Mkuu wa PCCB wakijaribu kuwashtaki mafisadi ujue kwasho yake wanatumbuliwa.
 
Back
Top Bottom