Rais Samia kapata wapi ujasiri wa kusafiri ilhali kuna majanga nchini?

Rais Samia kapata wapi ujasiri wa kusafiri ilhali kuna majanga nchini?

Ninaandika post hii ni saa 9 kasoro usiku machozi yananitiririka nashindwa kulala nipo nimeshika biblia na Quran hapa nashindwa hata la kufanya

Roho inaniuma maana kuna ndugu zetu wapo chini ya vifusi hadi muda huu na wanapigiwa simu zinaita wanalia tu na kutuma voice za huzuni za kuomba msaada[emoji24][emoji24].

Kuna binti yupo chini ya kifusi huko na ni mjamzito hapa nashindwa hata niandike nini

Rais anapata wapi nguvu ya kusafiri?Hiyo nguvu ya kupanda ndege hadi Brazil kaitoa wapi? Its shame and disgusting!! Yaani nyumbani watoto wako wapo chini ya kifusi halafu wewe kama mzazi unaenda kwenye sherehe ya jirani serious??

Sisemi kwa ubaya lakini Rais wetu kwa hili kakosea sana!!kaonesha ni jinsi gani asivyojali hili taifa!! Kaonesha ni jinsi gani asivyo na huruma na raia wake?

Huo mkutano una umuhimu kuliko roho za mamia ya watu walio chini ya kifusi?Rais amepata wapi huu moyo?nawaza nakosa jibu kabisa[emoji24]

Roho inaniuma mnoo!! Kwa hili rais Samia umekosea pakubwa mnoo!! its shame ni aibu mnoo na dharau kubwa kwa taifa hili.

PIA SOMA
- PICHA: Rais Dkt. Samia aelekea Brazil kushiriki mkutano wa G20
Inahuzunisha sana, tena sana!
 
Gentleman,
kua mkweli,
machozi yanakutitirika kwasababu ya madeni ya kausha damu unayopitia au ugumu wa maisha unaopitia, huenda kwasababu za uvivu wako?

Hata hivyo mbona ni dhahiri shahiri uchungu wako, wala sio hata kwaajili ya wahanga wa jengo lililoporomoka huko kariokoo ?

Mihemko yako ni dhidi ya jitihada za Rais Dr Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kwamba, licha ya changamoto, dosari na kasoro mbalimbali za kiasili na kibinadamu, bado hachoki wala kukata tamaa kuhakikisha anatumia fursa zote zinazoonekana Kitaifa na kimataifa kwa maslahi mapana ya wananchi na waTanzania wote?

Kamati ya maafa Kitaifa, iliyo chini ya waziri mkuu Kasimu Majaliwa, na makamu wa pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah, ipo kazini tangu kutokea kwa tukio hilo, unahitaji nani afanye nini tena gentleman?

Rais afanye nini zaidi ya hapo gentleman? Hakuna haja ya makasiriko na kuibua hisia potofu zenye chuki dhidi ya mkuu wa nchi.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Wewe kuna siku utapigwa na utakosa wa kukutetea 😏
 
Zanzibar ina watu milioni moja sawa na wilaya ya kinondoni hapa Dar, wewe unawashwa nini utoke huku bara uende kugombea udiwani huko visiwani wakati umeacha ardhi ya hekari laki tisa?.

Ubaguzi huwa unaziumiza nafsi zenu, JPM alibaguliwa kwa usukuma wake Chato pakaonekana sio sehemu ya Tanzania leo kaja Samia nae anaitwa sio mtanzania.

Akili za kibaguzi za namna hii huwa tunaziombea kila siku tunapopiga magoti makanisani.
JPM alikuwa mhutu.
 
Mapete,abiduli na mama kizimkazi wanaupiga mwingi ,MITANO TENA kwao na hapa ipo.
Screenshot_20241117-135040~2.png

😂 MukuLungwa man odi match!
 
Kuna haja ya kuwafanyia psychometric tests na analysis hawa wapuuzi kabla ya kuwateua kuwa viongozi , huwezi kuteua jitu lina Iq ya 50 halafu unatarajia jitu kama hilo liwe think-tank ya taifa ,ni upuuzi
Mtu mwenye IQ hio ni average, nadhani atakuwa around 30 sumthin
 
Huo mwaliko ni mkubwa sana hawezi kuacha kwenda lakini nchi ina viongozi wengine amnao wanafanya kazi nzuri mno hadi sasa
Hakuna mwaliko mkubwa ambao mtu hauwezi kukataa na kuacha kwenda.
 
Kifo Ni kifo Tuuuu aliwah sema,,, UNATEGEMEA KWA HILI KUNA MABADILIKO??? wanasema MSIBA usikie kwa jiran
 
Kwahyo Mbowe yupo ndani ya kifusi anaokoa watu syo,
hebu acheni kujitoa ufaham, kwani duniani si kina Vita vinaendelea umeskia Kuna udhuru wwte kisa Vita?
After all; jengo limeporoka Mh. Rais akiwa ameshaondoka lakini je Kuna kitu kimesmama? Mnaendekeza siasa za kipumbavu sana
Mbowe hatunzwi kwa kodi za raia wa Tanzania.
 
Kuna muda unakera ujue 😹
Watakupiga kotekote subiri uone..!!

Mi niko mzima, kuna muda punguza kuandika pumba watu tuna machungu ujue…
siku zote ukweli ni mchungu sana, na unatabia ya kukera sana aise. Pole sana lakini itabidi uzoeee mtumishi..

binafsi huandika ukweli mtupu mtumishi, na sina cha kupunguza au kuongeza kwenye vyote ninavyoandika ambavyo kwa kiwango kikubwa mno vinajitosheleza.

Hata hivyo naomba radhi kwa wote ikiwa ukweli huu unakwaza 🐒
 
Tanganyika kama koloni..ukiuliza utaambiwa 'sababu mama sio wa imani ileee,,anaamini huku'
 
Back
Top Bottom