Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Kuhusu changamoto ya Mitaji kwa Vijana amesema kuna Fedha za Halmashauri na Mifuko kadhaa ambayo inatoa Mikopo kwa Vijana imeanzishwa, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi kubwa ya Vijana
Lazima tukae kwenye mkeka tueleweshwe. Kama kazi zipo ama vijana ni wengi?
 
Tatizo vijana wengi wameelekeza nguvu zao, muda na maarifa mitandaoni. Hawataki kujishughulisha na kazi ya mikono au akili, muda mwingi wanautumia kuwapigania na kuwatetea wanasiasa wachovu ambao wengine wanaishi Ulaya kula bure, kulala bure nk. Wanasiasa hawa hawana msaada wowote wa maana kwao na familia zao. Sana sana wanaishia kutumiwa vijibando tu mtandaoni na buku buku ya kula.

Kwani hawa wanasiasa wa Ccm walioko hapahapa nchini wana faida gani?
 
Huku Mkwe wake akiwa waziri na binti yake akiwa mbunge.

Tunaponya nchi.

kwa hiyo mkuu kwako wewe haiwezekani kumpa mtaji mwanao au mkwe wako wakiwa kwenye nyakati ngumi na wewe uwezo unao...

Lakini pia wapi pameandikwa ukiwa Rais au kiongozi wa umma basi member wa familia yako hawapaswi kuwa na hizo nyadhifa...
 
kwa hiyo mkuu kwako wewe haiwezekani kumpa mtaji mwanao au mkwe wako wakiwa kwenye nyakati ngumi na wewe uwezo unao...

Lakini pia wapi pameandikwa ukiwa Rais au kiongozi wa umma basi member wa familia yako hawapaswi kuwa na hizo nyadhifa...

Kumbe kwa wengine wao kua kwny wkt mgumu ni kipindi wakiwa na cheo cha urais/makamu wa rais.

Hakika definition ya wkt mgumu imebadilika sana miaka hii mkuu.
 
Yupo sahihi vipi mtu unakua huna kazi, mfano rahisi hizi taka ukizifanyia kazi zinaweza kua mbolea.
Unafanyaje kazi bila kula au atatulisha bure ili tufanye kazi zozote zilizo mbele yetu😅 sababu hata kumzomea ndugai ni kazi ila ukiifanya inapaswa uwe na hela ya kula njaa ikikuuma!
 
Mkuu Biblia inasema asiyetaka kufanya kazi na asile. Sio asiyefanya kazi. Kumaanisha kama kuna kazi na ukakataa kufanya hiyo ndo shida.
Kazi zipo ila malipo ndio hamna na hakuna mtu anayetaka fanya kazi ya bure hata huo uraisi ukiondolewa maslahi ya pesa akawa anaamkia ofisini na kwenda site bila kulipwa sidhani kama ataendelea kuhudumu!

Kazi bila malipo ni kujitolea, so azungumzie kujitolea maana hamna anaekubali kufanya kazi za kanisa.
 
Back
Top Bottom