Rais Samia: Kijana aliyeongoza Uokoaji atafutiwe nafasi Jeshi la uokozi

Jeshi la zimamoto na uokoaji linahitaji maboresho.
 
Nampongeza Rais wangu kwa Jambo Hilo maana amefanya kitendo Cha kiungwana Sana kilichogusa hisia za watu wengi Sana ambao walitamani kusikia maneno hayo kutoka kwa Rais wetu mzalendo
Unaonaje Sa100 akiwapeleka Zima moto wakawe wavuvi, Ili kupokezana na wavuvi wanaoajiriwa Zima moto Ili KAZI iendelee???😠😠😠
 
Na pia nashauri apandishwe na cheo kabisa, japo ukoplo ama usajent.....
 
Kusaidia katika majanga mbalimbali hiyo ni jambo la kawaida kabisa kwa watanzania walio wengi, yaan ghafla unamuona mtu anapata shida pale lazima ile instinct ya ubinadamu ichukue nafasi yake haraka sana
 
Kabisa mkuu..nilivyoona 'breaking news' kwamba ndege imeanguka ziwani,nilimshukuru Mungu kwa maana nilijua abiria wataokolewa haraka.
Ila imekuwa tofauti kabisa na matarajio.
 
punguzeni kuturoga!!
jamaa ali opt calculated risk aliangalia hivi itakuwaje wakachelewa kuivuta na abiria wote wakafa au wakazama? inakuwaje iwapo wanakosa hewa? vyovyote vile wacha tujaribu kuokoa wachache itakavyokuwa na iwe!

tukiin'gan'ganiza inaweza ikatokea hadithi ya mtoto wa mdosi aliposhukuru kuwa asante kwa kumwokoa mwanangu katika bwawa la kuogelea kisha dogo akamwambia usijali! mdosi akamwambia unaniambia usijali mambo madogo kiatu chake kimoja kiko wapi!
 
Safi sana .Sasa akapate mafunzo na uzoefu alio nao kwenye maji. Huyu kijana bila yeye watu wote 43 wangeperish .
Dogo alijiongeza sana, angesubiria wale jamaa wa airport wangekataa mlango usivunjwe. Kwa akili zao wanadhani ndege ni waterproof
 
Mimi naomba yule aliemkataza huyo kijana asivunje kioo atajwe. Tumpe pongezi kwa kuua marubani
Hakuna mtu mjinga kama huyo kiongozi, kawaua marubani...

Mkuu wa Mkoa anatakiwa awajibishwe, Mkuu wa Uwanja, Usalama wa Uwanja, Zimamoto Mkoa.

Hawa wote wawajibishwe
 
Kwamba waajiriwa wa serikali Hakuna walichofanya zaidi ya kuiangalia ajali kama zoezi la majaribio.

Huyo dogo kwa jinsi alivyoelezea, alikuwa wa kwanza kurespond kwa sababu aliona mwenendo wa ndege si wa kawaida...
 
Ni agizo kutoka kwa Rais Samia,
Amiri Jeshi Mkuu, ameagiza Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni kuanza mchakato wa ajira ya huyo kijana mara moja...
Maana yake ni kwamba Rais ameona kuwa kijana yule ana akili, uwezo na ujasiri kuwazidi askari wetu.

Ingependeza zaidi wakati huyu anaingizwa huko jeshi la Polisi, wanfetajwa na wale wa kufukuzwa kutoka Jeshi la Polisi kwa kukosa maarifa, ujuzi na ujasiri.
 
Tena ingependeza kama baada ya kuajiriwa awe kamanda mkuu wa kikosi cha Zimamoto. Maana kazi aliyoifanya imeonekana.
 
Ni agizo kutoka kwa Rais Samia,
Amiri Jeshi Mkuu, ameagiza Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni kuanza mchakato wa ajira ya huyo kijana mara moja...
Hebu acheni ujinga.

Kuzamia tunakubaliana ila kwenda kifungua mlango Kwa nje tena majini! Sio ulifungukiwa kutoka ndani!
Sawa basi ajirini vijana wengi na mnunue vifaa vya uokozi kuweka kila Kona ya aina hii ya majini na kuwe na zimamoto kila Wilaya na gari zake.

Acheni kupiga pesa za misaada na kila bata kila siku safari na vikao.

Waziri Mkuu anasema tume ya kuchunguza kitu gani?

Tume ngapi ameunda zimeleta majawabu?
 
Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Majaliwa Jackson almaarufu Majamunyama ambaye ni mmoja wa vijana waliojitokeza kusaidia ...
Kama isingelitokea hii ajali hakungekuwepo na ajira!

Hii inadhihirisha wazi kuwa nchi haina dira ya miaka 10 hadi 30 ijayo kuweka wataalamu katika nyanja mbalimbali. Utopolo wa juu kiwango!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…