Rais Samia kuanza kusafiri na Wasanii kwenye ziara zake nje ya nchi
Raisi wa Kenya yupo Washington DC kashapata $500M na wawekezaji wa technology wakubwa. Nchi ina katiba mpya

Mama yetu hatuna katiba, badala ya kutengeneza wafanyabiashara Mama anatengeneza machawa tu. Sasa kila mtu atatoa nyimo zinaitwa Mama 🤣
Kwenye vyombo vya habari tv,,redion nchi imegeuka mapambio na kusifu atar sana
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mara nyingi anapokwenda nje ya Nchi huwa anafuatana na jopo la Wafanyabiashara lakini kwa sasa anataka kugeuka kidogo na atakuwa anasafiri pia na Wasanii ili kuwapa nafasi ya kujifunza zaidi kutoka nje ya Nchi na kutanua wigo wa kazi zao.

Rais Samia amesema hayo usiku huu wa leo May 25,2024 wakati akishiriki uzinduzi wa album mpya ya Msanii Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambapo amesema “Tunapofungua Nchi Wageni wanakuja kwetu na sisi tunakwenda kwao na mara nyingi ninapokwenda kwao huwa nafuatana na jopo la Wafanyabiashara, sasa nataka kugeuka kidogo nataka sasa niwe nachukua Wasanii”

“Nataka nifuatane na Wasanii inategemea ratiba yangu kule nakokwenda lakini kila ninapokwenda kukiwa na matamasha ya utamaduni nitabeba Wasaniii lakini zaidi nitakuwa na safari keshokutwa na moja ya kazi ninayokwenda kuifanya ni kutafuta nafasi za mafunzo kwa Wasanii wetu hasa Waigizaji”

“Tunakwenda Korea na mnawajua ni Wazuri sana kwa kuigiza, michezo yao naona inatambatamba kwenye TV zetu, kwahiyo tunaenda kutafuta nafasi za mafunzo na nadhani tutafanikiwa”
Nonsense
 
Dah balaa lingine hili m
Watu mna chuki na wasanii kama waliwalia vyenu,
Kwanini hamtaki wafaidi keki ya Taifa wajameni?
Chuki za nini sasa hivi mnajisahaulisha ya kwamba mama Kizimkazi ni bonge la actor kwenye Loyo tour?

Kwanini asiwape na fursa wengine kama nafasi ipo,
Ni wivu na Roho mbaya tu!
😁😁
Mkuu vijana au wazee wa kitanzania hatuna chuki na wasanii kabisa hata kama wakipewa pesa na mama pamoja na kwamba wanakuja kututambia sisi wenyewe tunaokamuliwa, tatizo lipo hapa bado nchi ina shida nyingi sana ambazo kama kiongozi mkuu inapaswa kuwekeza nguvu zake ili nchi ikae sawa mzee kuna mengi sana hii nchi haipo sawa ku mention yote ni kujipa stress zingine humu jf. Ki ufupi hatutendewi haki kabisa watu wanateseka aisee hali ya maisha ngumu sana labda kwa nyie wengine yako vizur kiasi kwamba unaona sawa yanayotokea......
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mara nyingi anapokwenda nje ya Nchi huwa anafuatana na jopo la Wafanyabiashara lakini kwa sasa anataka kugeuka kidogo na atakuwa anasafiri pia na Wasanii ili kuwapa nafasi ya kujifunza zaidi kutoka nje ya Nchi na kutanua wigo wa kazi zao.

Rais Samia amesema hayo usiku huu wa leo May 25,2024 wakati akishiriki uzinduzi wa album mpya ya Msanii Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambapo amesema “Tunapofungua Nchi Wageni wanakuja kwetu na sisi tunakwenda kwao na mara nyingi ninapokwenda kwao huwa nafuatana na jopo la Wafanyabiashara, sasa nataka kugeuka kidogo nataka sasa niwe nachukua Wasanii”

“Nataka nifuatane na Wasanii inategemea ratiba yangu kule nakokwenda lakini kila ninapokwenda kukiwa na matamasha ya utamaduni nitabeba Wasaniii lakini zaidi nitakuwa na safari keshokutwa na moja ya kazi ninayokwenda kuifanya ni kutafuta nafasi za mafunzo kwa Wasanii wetu hasa Waigizaji”

“Tunakwenda Korea na mnawajua ni Wazuri sana kwa kuigiza, michezo yao naona inatambatamba kwenye TV zetu, kwahiyo tunaenda kutafuta nafasi za mafunzo na nadhani tutafanikiwa”
Sasa ipi tena! Wale aliokwenda nao India wasanii wa Bongofleva hawakunogesha ziara?
 
Watu mna chuki na wasanii kama waliwalia vyenu,
Kwanini hamtaki wafaidi keki ya Taifa wajameni?
Chuki za nini sasa hivi mnajisahaulisha ya kwamba mama Kizimkazi ni bonge la actor kwenye Loyo tour?

Kwanini asiwape na fursa wengine kama nafasi ipo,
Ni wivu na Roho mbaya tu!
😁😁
Kumbe ni pisi kali kabisa jana alipendeza sana nashauli apendeze hivyo ata akiwa inje ya inchi,mm nilikua na muangalia yeye tu alivyo pendeza mengine sikuyasikia.
 
Kufungua nchi ni pamoja na kurahisha upatikanaji passport yaani unakuta mfano hai wasanii hawawezi safari kwenda kwenye matamasha kujifunza wakiomba passport wanaambiwa Lete barua ya mwaliko ndio tukupe.
Sasa tanasha Mtu hawezi kwenda kivyake akaangakie wanavyofanya ili naye akirudu akitoka kuandaa lake ajue linakuwaje

Raisi aliangalie Hilo pia Mtu sio Lazima awe na barua ya mwaliko kwenda nje.Hayo masharti yaondolewe
 
Back
Top Bottom