Rais Samia kuanza kusafiri na Wasanii kwenye ziara zake nje ya nchi
Isiwe ni wasanii wa muvi na muziki tu, wachukuliwe hadi wachoraji, wachongaji na wasanii wengine. Kina mpoto, shilole, steve, mond wanajulikana sana, wachukuliwe wasanii wasiojulikana kabisa na wao wajulikane
 
Huo muda wa kusafiri na wasanii, hayana manufaa kwake Rais wangu, ni kheri akaenda kuhiji.

1. FARIDHA YA HIJA.
HIJA:

Faridha ya Hijja ni moja katika nguzo tano za Kiislamu, faridha hii ameilazimisha Allah mtukufu katika Kitabu chake Qur-ani tukufu pale aliposema: ((Na Allah amelazimisha kwa watu Kuihiji nyumba (Al-Qaabah) mwenye kuiweza njia yake)) [Aala Imaraan 97] na kutoka kwa Ibn Abbaas (r.a) amesema: Alituhutubia Mtume wa Allah (s.a.w) basi akasema: ((Enyi watu imelazimishwa kwenu kuhiji)) akasimama Al-Aqraa bin Haabis na akasema: Jee! Ni kila mwaka ewe Mtume wa Allah? Basi Mtume (s.a.w) hapo akasema: ((Lau nitalisema basi lingelazimika, na lau lingelazimika musingeliifanya na musingeliweza, Hija ni mara moja, na mwenye kuongeza basi amejitolea))
 
Sanaa zote ni potential kwa nchi hii na ni ajira tosha kwa wananchi. Kuna sanaa hazipewi coverage kubwa kama music na movi na ndio haohao wasanii wake ndio watapata shavu kuambatana na rais huko ziarani. Ziko sanaa zingine wanafanya wananchi, wasanii wake nao wanapaswa kujumuishwa kwenye ziara ya rais wakajifunze zaidi huko kwa wenzao nje
 
Daa
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mara nyingi anapokwenda nje ya Nchi huwa anafuatana na jopo la Wafanyabiashara lakini kwa sasa anataka kugeuka kidogo na atakuwa anasafiri pia na Wasanii ili kuwapa nafasi ya kujifunza zaidi kutoka nje ya Nchi na kutanua wigo wa kazi zao.

Rais Samia amesema hayo usiku huu wa leo May 25,2024 wakati akishiriki uzinduzi wa album mpya ya Msanii Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambapo amesema “Tunapofungua Nchi Wageni wanakuja kwetu na sisi tunakwenda kwao na mara nyingi ninapokwenda kwao huwa nafuatana na jopo la Wafanyabiashara, sasa nataka kugeuka kidogo nataka sasa niwe nachukua Wasanii”

“Nataka nifuatane na Wasanii inategemea ratiba yangu kule nakokwenda lakini kila ninapokwenda kukiwa na matamasha ya utamaduni nitabeba Wasaniii lakini zaidi nitakuwa na safari keshokutwa na moja ya kazi ninayokwenda kuifanya ni kutafuta nafasi za mafunzo kwa Wasanii wetu hasa Waigizaji”

“Tunakwenda Korea na mnawajua ni Wazuri sana kwa kuigiza, michezo yao naona inatambatamba kwenye TV zetu, kwahiyo tunaenda kutafuta nafasi za mafunzo na nadhani tutafanikiwa”
Daah!! ukisikia kupatwa kwa nchi ndio huku sasa
 
Tukiendelea hivi kimasihara tutakuja kuwa kama Congo. Watu wanaopotea mara nyingi wanaaamini hawawezi kufeli kwa sababu haijawahi kuwatokea. Ikitokea wanashtuka imekuwaje ?
 
Tukiendelea hivi kimasihara tutakuja kuwa kama Congo. Watu wanaopotea mara nyingi wanaaamini hawawezi kufeli kwa sababu haijawahi kuwatokea. Ikitokea wanashtuka imekuwaje ?
Imenibidi nicheke tu [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nchi hii natamani kuhama, sema nimewekeza mabilion mengi kwenye nchi hii hivyo ni ngumu kuhama
 
Harmonize ana hadhi gani mpaka rais ahudhurie uzinduzi wa albam yake?
Jambo kama hili linatia kichefuchefu sana, sijui Ikulu hii ya siku hizi imekumbwa jinamizi gani!!!!??? Hivi inawezekana vipi Rais wa nchi ahudhurie kwenye mikusanyiko ya kipuuzi ya namna hii???!???? Hivi ni Watu gani hasa ambao wamekuwa wakimshauri Rais kufanya mambo ya kijinga kama haya???? Nina mashaka makubwa Sana juu ya Watu wa karibu ambao wanafanya kazi Ikulu katikà Ofisi ya Rais, hawamshauri vizuri Rais kiasi Cha kumfanya Rais huyo aonekane kama kituko mbele ya jamii. Very sad indeed!
 
Back
Top Bottom