Rais Samia kufanya ziara ya siku mbili Nchini Kenya kuanzia 04|05|2021

Ukiusoma huu uzi kwa makini unaweza kugundua akili za mataga bado hazija move -on.
 
Shida ni pale mama anapoona mtangulizi wake hakuwa sahihi kwa kila kitu na sasa hivi anafumua mpaka visivyostahili Kenya akiwachekea atajutia badaye jamaa wanafiki sana mama Mungu akupe maarifa uwe shujaa
Magufuli alikuwa kichaaa, muache mama SSH afumue kila kitu.

Unaanzaje kuwekeana bifu za KIJINGA na nchi mnapakana kwa kilometres zaidi ya 1,000, nchi ambayo Ina zaidi ya makampuni 200 yamewekeza nchini kwako?

Yule pimbi Mwendazake ndiyo maana Mungu kampoteza mapema maana tungefika hata 2023 Tanzania ingekuwa nchi ya HOVYO sana.

Unahitaji kutokuwa na akili kunipinga
 
......Na wakenya wataigharamia ziara hiyo..........
 
JK aliwahi kusema ni mjinga tu asiyeweza kuona faida za ushirikiano kati ya Kenya na Tanzania. Alipoingia JPM hakutaka kuchezewa, walipoleta dharau za ile list ya mataifa yenye kuingia nchini mwao mwaka jana kuhusu corona, TCAA ikawapa jibu la jeuri ikizifungia ndege zao pia.

Natumaini Rais Samia hatakubali uungwana wetu ututukanishe huko tuendako.
 
Nimesoma comment zenu nyingiiii sana wengi wanaona kama SSH amekurupuka kwenda kenya kwa sabb wakenya ni wajuaji sana lkn mm nasema hapana kwa sabb wanasema kubali wito kataa ujumbe mm naona tumpe nafasi tu mama then tumpe muda tuone results.....!!
 
Ambacho hukijui ni kwamba raisi lazima asafiri. Raisi asiyesafir huyo ni mshamba na aliyepitwa na wakati.
Soma vizur Economic diplomacy mzee.
 
hahah. kenyatta noma sana alimtumia samia suluhu mama Amini ambae pia anavaa hijabu ili amlegeze samia
 
M
Magufuli aliwadhibiti vizuri sana Manyang'au..
Samia asilegeze
Mkuu, mie kiukweli siwapendi hawa jamaa kwa tabia yao ya kudandia kila kilicho chetu kiuchumi kukifanya kuwa chao. Siku moja nilikuwa nasikiliza radio moja ya nje ya kimataifa nikamsikia mzungu mmoja akihojiwa kuhusu uelewa wake kwa nchi ya Tanzania, akasema yeye alikuwa akiifaham Tanzania kama ni sehemu ya Kenya.
Kama mie ningekuwa Raisi wa nchi hii ningeielekeza nchi yetu ijikite sana na nchi zilizomo SADC. Wametulia hawana makandokando hata amani ni ya hali ya juu.
 
Shida ni pale mama anapoona mtangulizi wake hakuwa sahihi kwa kila kitu na sasa hivi anafumua mpaka visivyostahili Kenya akiwachekea atajutia badaye jamaa wanafiki sana mama Mungu akupe maarifa uwe shujaa
Ziara hii ni nafasi kwetu kujua yeye ni kiongozi wa namna gani.

Naona amaamua kujipambanua kungali mapema sana.

Tunasubiri kuona.
 
Nadhani haya mambo hayataki jazba, sisi na Kenya sio maadui ila wahasimu wa mambo ya nani bora ambalo ni jambo zuri kama litaleta faida za kiushindani lakini sisi sio maadui kabisa. Simba na Yanga sio maadui wahasimu tu ndio kama sisi na Kenya. Kenya ndio nchi inayoongoza uwekezaji mkubwa kwetu ni number moja sasa huyo sio adui, nakumbuka maneno ya Kikwete aliyaongea hata yeye ni kichaa tu anaweza kuvunja uhusiano sababu tumeshikana sana kiuchumi sasa Mama anarekebisha tu tulipokosea mambo binafsi ya urafiki na Odinga hayana tija na sisi maslahi ya nchi mbele. Kenya wanatuhitaji na sisi tunawahitaji. Mama weka mambo sawa leo hakuna hata bus linaenda Kenya au kuja huku biashara zitaendaje.
 
Ntatofautiana na wanaobeza hii ziara kwa wakenya, mimi naunga mkono asilimia 100 Kenya ni muhimu sana kwa uchumi wetu na sisi ni muhimu sana kwa uchumi wao.
Bahati mbaya watu hawaelewi investment ya wa Kenya hapa kwetu wanaongoza Africa. Sisi sio maadui ila tunashindana kwa maendeleo ni jambo zuri na Mama anaenda kuweka mambo sawa cross border business lazima irudi kama kawaida tulikuwa na ndege za Kenya 6 times a day leo sijui mara 3 kwa wiki na uhakika tutaanza kuona biashara tena kwa wingi na sote tunahitajiana sana tu.
 
Nani kashabikia kujifungia.
Kwani Kenya ndio dunia pekee? DRC, Malawai, Zambia, Mozambique, Uganda, Rwanda, Burundi, Comoro, na kwingineko, huko hakuna dunia?
Hizo nchi zote ulizozitaja wamewekeza nini hapa kwetu kwenye Foregn direct investment? Kenya wamewekeza kiasi kikubwa hapa kuliko nchi yoyote ya Africa. Mama kesho anaenda kuweka mambo sawa biashara irudi wewe labda unaongelea wale wanunuzi wa Kariakoo. Hawa wana inject FDI nchini ndio kipimo cha uchumi kukua. Kikwete alishasema haya ni kichaa tu anaweza kuharibu uhusiano huu. Mama yuko vizuri anajuwa waliteleza wapi. Kumbuka Nairobi ni hub ya mashirika yote makubwa wana office zao pale huwezi kudharau hilo ukaenda Lilongwe au kucheza ndombolo Kinshansa.
 
Nimekusoma kwa taratibu nikuelewe vizuri.

Sasa ni hivi, na napenda hata wewe unielewe ninachoamini mimi.

Kenya na sisi ni majirani, hakuna chochote tunachoweza kufanya juu ya hilo, daima tutakuwa majirani.

Majirani wanaweza kuwa majirani wema na wakaelewana na kutakiana mema; hata kama hapawezi kukosekana mikwaruzo ya hapa na pale, kama ilivyo kwa ndugu wanaoishi nyumba moja.
Hili nalo linaeleweka.

Kama majirani, na hata bila kuwa majirani, tunaweza kufanya biashara kati yetu kwa misingi ya kibiashara bila kujali tu marafiki au sio marafiki. Natumaini hili nalo hata wewe unalielewa.
Ndiyo, katika biashara kuna ushindani, kama ilivyo katika michezo, kama hiyo ya Simba na Yanga uliyo itolea mfano. Lakini, katika hilo la ushindani ndipo panapoweza kuanzia tatizo. Kuna kufanyiana mambo mabaya ili ushinde. Kuna washindani wa namna hiyo, na kama kweli unaamini hili haliwezekani, basi hapa ndipo tofauti yako inapoanzia.

Nchi zetuhizi, kihistoria ina mitizamo kinzani toka zamani, sijui kama ni tabia za watu au vipi? Kisiasa pia tunatofautiana sana kati yetu na hawa majirani zetu. Huwezi kufumba macho na akili kabisa usizione tofauti hizo kati yetu.
Sisi hatukuwa na tabia ya kunyang'anyana, hadi hivi karibuni, na ukabila haukuwa tatizo kwetu, haya mambo kwa upande wa pili ni hali ya kawaida sana.

Siwezi kuorodhesha tofauti zote zinazotutofautisha kati yetu, lakini kama una msimamo wa wazi huwezi kukosa kuzijua tofauti hizo.

Kwa hiyo, naomba unielewe, sikatai tufanye biashara, biashara kama itanoga, tutaanzia hapo kujengeana imani na hayo mengine ya udugu na urafiki.

Huwezi kuniita ndugu au rafiki huku ukitafuta njia za kuniangusha. Kama wewe huoni mbinu hizo, usidhani wengine nao hawazioni.
 
Sasa hili la kuwekeza naona limekutoa akili kwelikweli.
Kwa hiyo kwa vile amewekeza unataka sasa tufanyeje, si hivyo kumbe anafanya biashara?
Sasa unalilia nini hapa. Tufanye nini cha ziada?

Sasa angalia usivyokuwa na ufahamu. Kwa hiyo hizo nchi nyingine tuendelee kuziweka pembeni kwa vile hawawekezi? Hii ni akili ya namna gani hii!

Huyo anayewekeza, mbona juzi kayakataa mahindi yetu kwa kisingizio tu cha kuwa na sumu. Umejaribu kulifikiria hilo? Hawa wakulima wetu huwaonei huruma, wewe unaangalia 'investment' pekee? Huo ndio uhusiano unaoutafuta hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…