Rais Samia kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II

Rais Samia kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II

Tayari Londoni kuliwakilisha taifa
View attachment 2360034

Kwanza ni heshima kupata mwaliko na pia ni hatua nzuri sana Kwa ajili ya kuimarisha uhusiano. Juzi tu hapa filamu ya The Loyal Tour ilipondwa lkn matokeo yanaonekana. Yaani Wadau wa utalii wamezidiwa wateja. Sasa kitendo Cha Mheshimiwa Rais wetu kuhudhuria mazishi ya malkia ambaye alivalishwa ALMASI ya Pink kutoka mgodi wa Williamson Mwadui pamoja na mambo mengine basi utalii na watu wa uingereza na ulaya watakuja Tanzania kutalii. Pongezi nyingi sana Kwa MH SSH kutuwakilisha. Kazi iendelee
Loyal tour= msafara mtiifu
Royal tour= msafara wa Kifalme, a Kimalkia
Umemaanisha upi?
 
Huyu lazima ana akaunti humu JF kwa jinsi anamvyomkodelea macho bibi wa kizungu...
Halafu anakuja kuleta povu la bibi wa kizungu hakupiga makofi na kuimba mapambio....

1663455926502.png
 
Mawasiliano ya rais.
Tahrir:
Waswahili twaandika kimazoea 'Malkia' na si Malikia (ingawaje kisarufi Malikia ni sahihi zaidi). Queen Consort "Malkia Mfariji' ni jaribio zuri la tafsiri ya kimajaka ya neno hilo yasiyopatikana maana yake katika Kiswahili. Lakini halimfahamishi msomaji maana halisi. Maana halisi ni kuwa kwa vile Mfalme wa Uingereza ndiye pia kiongozi wa Kanisa Protestant, ni haramu kuachana na mwanamke aliyemwoa. Akifanya hivyo, ni yule aliyeachwa tu ndiye anayetambulika kuwa Malkia ambaye ana nafasi ya kurithi ufalme kama hakuna mtoto wa kiume, kama ilivyotokea kwa maehemu Malkia Elizabeth. Sasa, stori ya Charles na Diana inajulikana sana. Na kabla yao, Malkia Victoria alikuwa na 'Prince Consort' Albert, kwa sababu hizo hizo. Of course, huwezi kuweka maelezo yote haya katika taarifa fupi. Napendekeza neno 'Consort' ingawaje kweli linamaanisha 'mfariji' kimajaka, ila tulifasiri kifahiwa zaidi ndiyo italeta ladha. 'Malkia bila taji' itakuwa karibu zaidi. Maana hiyo 'Consort' imewekwa hapo kukumbusha kuwa huyu hana chake katika Ufalme!
Camilla Parker-Bowles: Hii ni lazima iandamane na hyphen - kwa sababu ni jina lililofanywa kuwa moja, surname. Wazungu, (wengine wasema Wakristo) wanapoolewa huchukua jina la ukoo wa mume. Lakini kuna wanawake wengi, hasa wanaotoka katika koo kubwa, au wanaotaka kuzatiti usawa wao, anapoolewa na mtu wa ukoo mdogo huona 'nongwa' kuacha jina lake 'adhimu'. Na hivyo huchagua kuchanganya yote mawili- yaani afaidi kheri za duniani na akhera pia! Ndipo unaona jina la ukoo la mke na la mume yamechanganywa: Parker-Bowles. Ingawaje unaweza kuandika bila hyphen ila italeta mkanganyiko. Mojawapo ukitaka kumwita kwa jina la ukoo wake tu huenda ukamwita Mrs Bowles. Lakini panapokuwa na hyphen, taabu hiyo haipo. Jina kama hili hujulikana kwa Kiingereza kama 'Double-barreled surname'.
Bado kuna mkanganyiko mkubwa wa kisheria katika majina kama hayo. Kama vile, jina gani litangulie katika mseto huo, la mume au la mke? Mtoto atakayezaliwa naye akiolewa na akitaka 'double-barreled' aitweje?
Imepelekea mpaka ukakuta majina kama: Beyoncé Beyoncé Giselle Knowles-Carter! Lakini katika hali ya kawaida utayakuta hivi tu: Catherine Zeta-Jones, Olivia Newton-John.
Duh! Nimetoa elimu nyingi hapo, sijui niombe tozo hukooo?
 
Kwamba ni lazima au?
Maana nchini gharama za maisha ziko juu. Yeye anakwenda msibani.
Au atatuletea zawadi ya mkopo nafuu??
We! Kuna mambo muhimu zaidi ya njaa. Pambana na njaa yako mwenyewe!
 
Mama anatupa heshima kwenye mizania ya kimataifa. Dunia hiini kuchangamana ili kufungua fursa. Mama aambiwe Mayele kapiga hatrick nyingine
 
Wivu kwani anaenda huko kwa pesa za mzee suluhu na anamuakilusha mzee Hassani?
Jitahidi na wewe uwe raisi tuone utakavyokuwa unaacha kupanda ndege na kwenda kijijini kwenu na misafara ya magari 70 huku ukibeba mafurushi ya pesa za umma kwenda kuwagawia ndg zako huku kwa mwaka ukifanya safari za ivyo more than ten times. Mimi nimeridhika na hali hii
 
Jitahidi na wewe uwe raisi tuone utakavyokuwa unaacha kupanda ndege na kwenda kijijini kwenu na misafara ya magari 70 huku ukibeba mafurushi ya pesa za umma kwenda kuwagawia ndg zako huku kwa mwaka ukifanya safari za ivyo more than ten times. Mimi nimeridhika na hali hii
Duh sijakuelewa kabisa.
 
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awasili London nchini Uingereza kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Muwakilishi wa Mfalme Charles III, Cynthia Gresham wa Uingereza pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Luton tarehe 17 Septemba, 2022 kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza yatakayofanyika tarehe 19 Septemba, 2022 Jijini London.
View attachment 2360184View attachment 2360185View attachment 2360186

Kujua Safari Nyingine za Rais Soma Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Mar 2021
Mwache azidi kutumbua tozo zetu sisi mafala
 
Wakati ukimshauri kupata "matibabu", ni wazi hapo ulipo wewe ni mhanga mkubwa anayetaka msaada huo huo, kutokana na ushabiki uliopitiliza, ni ushabiki wa kichizi!
Mimi naongea uhalisia kwa kuweka ushahidi wa mambo makubwa aliyo yafanya mh Rais yaliyoishangaza Dunia baada ya kuona matunda yake, mama yupo kazini muda wote
 
Back
Top Bottom