Tahrir:
Waswahili twaandika kimazoea 'Malkia' na si Malikia (ingawaje kisarufi Malikia ni sahihi zaidi). Queen Consort "Malkia Mfariji' ni jaribio zuri la tafsiri ya kimajaka ya neno hilo yasiyopatikana maana yake katika Kiswahili. Lakini halimfahamishi msomaji maana halisi. Maana halisi ni kuwa kwa vile Mfalme wa Uingereza ndiye pia kiongozi wa Kanisa Protestant, ni haramu kuachana na mwanamke aliyemwoa. Akifanya hivyo, ni yule aliyeachwa tu ndiye anayetambulika kuwa Malkia ambaye ana nafasi ya kurithi ufalme kama hakuna mtoto wa kiume, kama ilivyotokea kwa maehemu Malkia Elizabeth. Sasa, stori ya Charles na Diana inajulikana sana. Na kabla yao, Malkia Victoria alikuwa na 'Prince Consort' Albert, kwa sababu hizo hizo. Of course, huwezi kuweka maelezo yote haya katika taarifa fupi. Napendekeza neno 'Consort' ingawaje kweli linamaanisha 'mfariji' kimajaka, ila tulifasiri kifahiwa zaidi ndiyo italeta ladha. 'Malkia bila taji' itakuwa karibu zaidi. Maana hiyo 'Consort' imewekwa hapo kukumbusha kuwa huyu hana chake katika Ufalme!
Camilla Parker-Bowles: Hii ni lazima iandamane na hyphen - kwa sababu ni jina lililofanywa kuwa moja, surname. Wazungu, (wengine wasema Wakristo) wanapoolewa huchukua jina la ukoo wa mume. Lakini kuna wanawake wengi, hasa wanaotoka katika koo kubwa, au wanaotaka kuzatiti usawa wao, anapoolewa na mtu wa ukoo mdogo huona 'nongwa' kuacha jina lake 'adhimu'. Na hivyo huchagua kuchanganya yote mawili- yaani afaidi kheri za duniani na akhera pia! Ndipo unaona jina la ukoo la mke na la mume yamechanganywa: Parker-Bowles. Ingawaje unaweza kuandika bila hyphen ila italeta mkanganyiko. Mojawapo ukitaka kumwita kwa jina la ukoo wake tu huenda ukamwita Mrs Bowles. Lakini panapokuwa na hyphen, taabu hiyo haipo. Jina kama hili hujulikana kwa Kiingereza kama 'Double-barreled surname'.
Bado kuna mkanganyiko mkubwa wa kisheria katika majina kama hayo. Kama vile, jina gani litangulie katika mseto huo, la mume au la mke? Mtoto atakayezaliwa naye akiolewa na akitaka 'double-barreled' aitweje?
Imepelekea mpaka ukakuta majina kama: Beyoncé Beyoncé Giselle Knowles-Carter! Lakini katika hali ya kawaida utayakuta hivi tu: Catherine Zeta-Jones, Olivia Newton-John.
Duh! Nimetoa elimu nyingi hapo, sijui niombe tozo hukooo?