Rais Samia kuingia na mlinzi wa kiume msikitini, ni jambo la kawaida. Tuache Mihemko isiyo na Tija

Rais Samia kuingia na mlinzi wa kiume msikitini, ni jambo la kawaida. Tuache Mihemko isiyo na Tija

Unaposema kawaida inalinganisha na wapi au nan

Pia watu hawashangai mwanaume kuingia msikitini ishi kwanini wamkikishe ? Ilihari wadada tunao wazur kiulinzi
 
Walatia ndio wanapata tabu , mpaka nashangaa na hawana elimu ya uislamu....Wanawake mule hawapo uchi .

Kule Mecca walinzi ni wakina sehemu zote?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa hili mkubali tyuu, kimewalambaaaa
 
[emoji3][emoji3], kwa hiyo kuvaa hijab ni kuchochea ushoga,

Mbona huko iran, Syria na mataifa mengine ya kigaidi wanaume huvaa hijab wanavyoenda kulipua sehem mbali mbali. Je nao ni mashoga [emoji848][emoji848]??
Ndyooo!!!
 
Tena wanazojitungia wenyewe?

Ila sa100 sasa kazidi maana kila analofanya linaonekana la ajabu akitoka nje ya nchi anafanya viroja akiwa ndani ya nchi anafanya viroja.
😬😬😬😬
 
Jisemee uache mihemko sio tuache.usitumie wingi wakati mwenye shida ni wewe.Watu hawajatumia mihemko ila wameona sio sawa na haikua na ulazima kuhadaa.
Mimi sina Mihemko yeyote ile.. Ila nyinyi naona mnakuza vitu ambavyo ni vya kawaida kabisa... Utafikiri huko msikitini huwa analala MUNGU
 
Rais SSH kuingia na mlinzi wa kiume mskitini ni jambo la kawaida kutokana na sababu mbali mbali , hasa kama kuna tishio la usalama au kutokana na idadi kubwa ya watu wanaokusanyika kwa pamoja.

Tujiepushe na mihemko isiyo na tija na badala yake tufikirie suluhisho zinazojenga na kuheshimu maadili ya jamii husika na kuhakikisha usalama na utulivu wa Rais.

Katika Quran, hakuna aya inayosema moja kwa moja kuwa ni marufuku kwa mwanaume kuingia sehemu ya wanawake msikitini. hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W) pamoja na mila na desturi za Kiislamu. Kwa mfano, katika hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W), kuna maelekezo yanayohimiza heshima na mipaka baina ya wanaume na wanawake wakati wa ibada ili kuepusha fitna na kudumisha heshima.( kuepusha matamanio ya kimapenzi ndani ya ibada. )

Ibn 'Umar aliripoti kwamba Mtume Muhammad (S.A.W) alisema, "Usiwazuie wanawake wa Allah kwenda kwenye misikiti ya Allah" (Sahih Muslim, Kitabu 4, Hadithi 891). Hadithi hii inaonyesha kwamba wanawake wanaruhusiwa kwenda msikitini, lakini haina amri maalum kuhusu maeneo maalum ndani ya msikiti. Kwa hiyo, mpangilio wa ndani wa msikiti kuhusu maeneo ya wanawake na wanaume unaweza kutegemea mila, desturi, na mantiki za kiutawala za msikiti huo na siyo tamko la S. A. W.

Katika mazingira ambapo kuna haja ya kuwepo na walinzi wa kiume kwa sababu za kiusalama, ni kwamba tunahakikisha hatua hizi zinachukuliwa kwa njia inayoheshimu mipaka ya kijinsia na dini, kulinda usalama bila kuvuruga utulivu wa ibada.( na hiki ndo amefanya RAIS SSH wa JMT)

Mtazamo huu unategemea hadithi kama ile inayosimuliwa na Umm Atiyyah, ambaye alisema kwamba wanawake waliokuwa kwenye hedhi waliambiwa wakae mbali na mahali pa kusalia/swalia wakati wa sala za Eid (imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim)

Surah Al-Baqarah (2:222), "Wanakuuliza habari ya hedhi. Sema: Huu ni unajisi. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi, wala msiwakaribie mpaka watwahare.( Tusilaumu sana yawezekana mlinzi wa kike alikuwa kwenye Surah Al-Baqarah 2:222 ).

Pia soma: Mlinzi wa kiume wa Rais kuvaa juba (vazi la kike) na kuketi msikitini sehemu ya wanawake ni sawa?
Sio mwanamume
 
Sasa si angeingia tu, hilo dela la nini? kumdanganya nani? Je tukihoji ndani ya dela mlimvalisha nn mtasema tunavuka mipaka?
. Ukimpata mhoji, Hakuna tabu kabisa..

. Kuingia au kutokuingua na dera/kanzu hakuna tatizo lolote lile mkuu
 
... Kwa hiyo, mpangilio wa ndani wa msikiti kuhusu maeneo ya wanawake na wanaume unaweza kutegemea mila, desturi, na mantiki za kiutawala za msikiti huo na siyo tamko la S. A. W.
Msikiti gani ambao haujawahi kufuata mila hii?
 
Mkiambiwa hii dini ni abrakadabra tu muwe mnaelewa badala ya kuja na mapovu. Hakuna utakatifu hapo na wala Mungu hayupo hapo, hiyo ni mipangilio ya wanadamu tu wala hakuna dhambi mlinzi huyo wa kiume kuingia sehemu hiyo ya wanawake kuswaliia. Labda kwa heshima na mila zetu za kiafrika tu ndio hairuhusiwi kuingiliana sehemu za faragha za jinsia tofauti
. Upo sahihi mkuu, dini ni kitu cha ziada tu kama mahitaji mengine....

. Kwa hiyo Rais anaweza kuingia mfumo wa ulinzi anaotaka au kupangwa na idara yake.
 
Back
Top Bottom