Rais Samia kukopa(tena) 1billion USD from IMF

Vipi kuhusu exchange rate kwa Magufuli hela yetu imekuwa stable sana! Magufuli was better maana alikopa na vitu vinaonekana in ground!
 
Hata tukiuzwa hakuna wakutununua.

Dunia ya Sasa Serikali kukopa haishangazi, muhimu matumizi mazuri ya hizo fedha.
Tz matumizi mazuri ni msamiati, watu wanatumia hovyo na hawafanywi kitu, refer MSD
 
Hivi kwanini hawakopi hizo 1.1 billion dollar na kuua tatizo la umeme nchi nzima, hii mikopo ya kujenga matundu ya vyoo naona kama ni kuongeza umaskini tuu, lakini msishangae unaweza kukuta hata pesa za mishahara hakuna wanatumia hii mikopo kulipa, bongo ni changamoto
 
Mimi si mtaalamu wa haya mambo ya fedha na mikopo ya hizi taasisi najaribu kujibu kienyeji.

Jibu: Watalazimisha nchi yetu ijitangaze mufilisi na tuchukue austerity measures kama Ugiriki, Cyprus na Malta miaka ya karibuni.
Hapo siye watu wa chini itakuwa kilio na wawekezaji toka nje watachukua pesa zao wataondoka.

Mifano ni European dept crisis miaka ya 2008 huko kama sikosei.

KEY POINTS from investopedia website:
  • Austerity measures refer to economic policies implemented by governments to reduce government spending in order to reduce public debt and to shrink the budget deficit.
  • Policies that are considered austerity measures include an increase in taxes, cutting back on government programs, such as healthcare services and aid to veterans, a reduction in pensions, and a reduction in salaries and wages for government employees.
  • Depending on how austerity measures are implemented, they can make life difficult for citizens due to less available social services and less disposable income.
 
Nyongeza mkuu Kalamu1.

Dalili ya athari za madeni na kupelekea austerity kutokea ni nchi kuchapisha fedha mpya kujaribu kuziba pengo.
Na sasa tumesikia tetesi humu JF nchi flani inakaribia kuchapisha pesa mpya hali ya uchumi ni tete.
 
Hiyo itakuwa ni stimulus loan kwa ajili ya kusawazisha hali ya kiuchumi.......muhimu ni hiyo mikopo kutumika kuleta tija zaidi.
Mikopo mingapi iliyoleta tija mpaka sasa?
 

1billion USD from IMF!??? Tutauzwa tunakoelekea.​

Sio unalalama tuu je, huwa unakumbuka kudai receipt unapofanya manunuzi? Au na wewe huwa unashiriki kusaidia ukwepaji wa kodi.
 
Hiyo itakuwa ni stimulus loan kwa ajili ya kusawazisha hali ya kiuchumi.......muhimu ni hiyo mikopo kutumika kuleta tija zaidi.
Watanzania bwana kwenye kulipa utasikia ni sisi wananchi kwenye kulipa wanakimbia kama panya road. Huyo ukimwambia maisha yako umelipa ngapi tax usikute zero na huduma zote anapata na kama kalipa ujuwe kapiga. Kukopa kubaya kama kwa matumizi ya kawaida lakini kwa maendeleo wala sio shida. Ni sawa wewe ukikopa Bank ukajenga poa lakini huwezi kukopa kununulia ugali ujue unashida.
 
Kwani mhe Ndungai anasemaje ??!!
 
Hivi na sisi hatuwezi kuomba direct mkopo ukija tupatiwe hapo raia moja kwa moja, nchi ishakua kama kicoba hii
 
Nakumbuka enzi zile baada ya vita vya kagera Mwalimu alisema wananchi wajifunge mikanda kwa miezi 18 lakini baadaye hayati Sokoine akasema tuendelee kufunga mikanda inawezekana ikawa ni kwa miaka 18 badala ya miezi 18 !! Tuliifunga mikanda na tuliizowea ile hali na maisha yakawa yanaenda vizuri tu !!
 
Sijawahi kuwa mfuasi wa Magufuli,never ever,siwezi kuwa mfuasi wa wajaa,mimi ni mfuasi wa Ubepari jamii yaani social democracy na sio ujamaa...

Msingi wa ujamaa ni kuua personal initiative,sifa nyingi na maneno meeengi ya kutiana matumaini wakati kwenye actual things hakuna kitu...

Ndio maana Mwendazake alikuwa anawalisha maneno,propaganda nyingi na hadithi za kufikirika.
 
Sina shida na Kukopa na nasema wakope zaidi na zaidi mikopo ya mda mrefu kwa ajili ya miradi tuu,naunga mkono hoja...

Ila kukopa kwa ajili ya kutoa ruzuku kwenye mafuta hapana, Serikali isifanye hili kuna njia nyingi za kupata pesa ya Ruzuku ya Mafuta kama tulivyochangia hapo awali..

Tanzania hii bila mikopo ya miradi ya maendeleo hatutoboi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…