Rais Samia Kumhamishia Chalamila Dar es Salaam, Umelipokeaje?

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Usiku wakati tarehe 15 Mei 2023 ikielekea ukingoni Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu iliachia "PDF" ya Mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa ambapo wakuu wa mikoa minne waliguswa na mabadiliko aliyoyafanya Rais Samia Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akitoka Dar es Salaam, Adam Kighoma Malima amehamishiwa, Morogoro akitoka Mwanza, Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa Kagera

Stori kubwa ni Mzee wa "kadansee", "mzee wa kuleni bia" Albert John Chalamila kuhamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam akitokea Kagera.

Chalamila ana matukio mengi sana akiwa kwenye nafasi ya Mkuu wa Mkoa katika sehemu tofauti tofauti, vipi mwanajamvi unaouonaje uamuzi wa Rais Samia kumleta jijini Dar es Salaam, ataliweza jiji la Dar?
 
Unasema kuwa CHALAMILA ana matukio mengi. Matukiao mengi yapi? Tufafanulie basi na sisi tutafafanua matukio makubwa ya MAKALA kubwa la machawa
 
Kumleta karibu na breweries maana kagera ni full of local gongo haijafanyiwa utafiti ila pia the guy is vocal anaweza kuwapiga siasa kuliko huyo mwingine
 
Tunashukuru kwamba sasa Bar zote zilizofungiwa zitaanza kufunguliwa bila faini

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Umeshasema Mze wa kadansee, sasa kaenda jiji la kula raha ili akakadensike huko na machangu wa Dar akisahau wajibu wake wa kulitumikia taifa.
 
Chalamila anafaa, yule nikimtazama vizuri ana uchizi fulani unaofaa kuliongoza hili jiji, Dsm haimtaki kiongozi laini, inamtaka mtu msumbufu atakayeendana na usumbufu wa wakazi wa hili jiji.

Yule Makala issue ya Kariakoo ndio imemuondoa, wale wafanyabiashara walimmudu sana, na alitakiwa kupelekwa mikoa kama Rukwa huko isiyo na mambo mengi, lakini sio Mwanza, siku machinga wa Mwanza nao wakiamka watamuondosha ofisini.
 
Huyu jamaa huwa simkubali hata kidogo cjui kwa nn anapewa nafas km hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…