Rais Samia Kumhamishia Chalamila Dar es Salaam, Umelipokeaje?

Makala ameshachemsha nahisi wanafuatilia uhusika wake kushindwa kuepusha mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo

Ndani ya CCM ukiharibu unahamishiwa kwingine ukaharibu zaidi ndo wakuteme
 
Alichelewa kufanya hivyo
 
Kariakoo issue inaweza kuwa imechangia sababu kwa jana ilikuwa kama kapoteza yale mamlaka yake sababu mtu yoyote katika nafasi yoyote ikitokea siku watu unaowaongoza wakakukatalia maamuzi au maombi yake hadharani basi ni wakati wa ku step down sababu hautaweza tena kurudisha power, kimpira tunasema Manager kapoteza dressing room ndio yaliyomkuta jana, sio kwamba kiongozi mbaya ndio maana kapewa team nyingine nadhani uamuzi wa busara sana ili keshokutwa wakikutana Mkuu wa mkoa mpya atalibeba jukumu la maamuzi na hili mbele ya wafanya biashara kariakoo itaonekana kama mwanzo mpya. Good political move.
 
Kawaletea komediani
 
Exactly, unapowaambia watu nendeni Dodoma mkaongee na PM, nao wanakujibu hatuendi Dodoma PM ndie atufuate, hii maana yake Makala alishachemka.
 
Mwanza hakuna mkuu wa mkoa. Jamaa anakagua miradi usiku bila kujua je mradi unafanya kazi au taa zinawaka tuu
 
Sijawahi kumkubali Makala na style zake za kila sehemu akienda masoko yanaungua moto!
Watu wa Lango lango na Makoroboi waangalie sana!
Huyu jamaa sijui anatembeaga na moto au ndo style yake naye ya uongozi?!
Anyway kawazingua sana machinga na wafanyabiashara ndogo ndogo wa DSM.
 
Kuhusu Chalamila kuja Dsm, hapo mama kaupiga mwingi sana kwa kweli. Dsm inahitaji kiongozi "aliyechangamka" kama Chalamila.
Watu pamoja na mambo mengine, wanahitaji pia kufurahia jamani..
 
Samia anaenda kujiimarisha Kanda ya ziwa- Makalla ni mwanasiasa mwenye ushawishi ni kama anampeleka maandalizi ya uchaguzi
 
Akizingua wamlete huku Katavi
 
Hili la Kariakoo ni mojawapo lakini Makala ana laana ya kupora ardhi za masikini. Huyu Makala acha aende tu. Mkuu wa mkoa unaunda "syndicate" ya kuwapora watu ardhi kwa kisingizio cha kuondoa wavamizi. Yaani huko Mabwe, Kinondo, Malolo, Mbopo na maeneo ya jirani kuna watu masikini waliporwa ardhi zao mchana kweupe. Badalla ya kuwashirikisha wananchi ili ajue nani mvamizi kwani wavamizi wanajulikana yeye akaunda genge lake pamoja akishirikiana na afisa ardhi Kinondoni nakuanza kupora ardhi za masikini tu matajiri wanawaacha. Hakika Mungu yupo na watu wake. Gondwe alihamishwa bado hakustuka mpaka yamemkuta.

Mama Samia chonde chonde bado Afisa ardhi Kinondoni na mkurugenzi wa manispaa ya Kinondnoni. Wote hao walishirikiana na Makala kuwapora ardhi masikini badala ya kutatua migogoro.
 
Good political move ! 50 % ya k/koo ni wakinga ataelewana nao bila shaka !!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…