Rais Samia, kuna mtu mmoja tu hapa Tanzania anaweza kukusaidia kuuvuka huu mtihani wa DP World na TEC - muite, ongea nae, msikilize, ufanye atachosema

Pamoja na huyu unayemsema hapa kuna chuma hiki kina roho wa Mungu na hakina udhehebu wala udini bali hunena maagizo ya yeye aliye juu akiite kitamuambia yampasayo kufanya nacho si kingine bali ni Mwl. Christopher Mwakasege. Azingatie sana hili maana aendapo kuna giza totoro kwake na ni hakika asipokuwa makini akiendelea kuendekeza machawa basi ataandika historia mbaya sana. Itakuwa heri endapo akilisikia neno hili la Mungu.
 
Mwandosya apeleke ushauri mwenyewe, asisubiri kuitwa
Huyo Huyo Mwandosya ambaye amekuwa mtetezi na mlinzinwa Katiba Mbovu na Mifumo mibaya Nchini?

Au kwa kuwa sasa hivi katemwa na serikali mnamtafutia ugali.
 
Mzee wa kukusanya Mbegu ya sadaka tu hana lolote.

Hakuna mtumishi pale.

Nchi inaangamia kwa maovu na dhambi yeye yuko bize na
1. kupanda mbegu
2. mzaliwa wa kwanza
3. Sadaka
4.maono
5. Lango.
 
Hili ndio jambo gumu kwa ccm
 
Haaminiki tena.
Ndo tatizo ambalo nchi yetu imefikia sasa huwezi kumuamini yoyote yule ambae amepewa dhamana ya kuongoza.

Viongozi wala kwa kamba zao (kwa ruhusa ya raisi, na pia watumishi wa umma wote ni wezi wakiiba mapato ya serikali na fedha za miradi mbalimbali.

Kama ni usafi nchi hii yahitaji "cleaning".
 
Mh Rais nakushauri muite Mungu wa mbinguni Asabuhi, Mchana na Jioni maana yeye pekee ndie mshauri wa ajabu, komandoo na jemedari wa vita na uovu atakuskia, nena nae taratibu bila kuchoka, atakushika mkono na atakuonyesha njia, na hili nalo litapita...
 
Sijui hayo mengine ila uliposema eti kagame alitaka kumpiga kikwete ikabidi kikwete amuite mwandosya amsaidie umeongopa mkuu.
Sipendi kubishana na watu wasiojua kwa sababu ni kujitia ujinga, maana hata sijui unachobisha hapa ni nini. Ni kwa sababu ya watu kama wewe niliona ngoja niondoke JF. Unajikuta unabishana na mtu hajui, na hajui kama hajui, na kwa sababu hajui anabisha tu kama mjinga fulani hivi

Soma hizi post hapa chini za 2013 na 2021, ili uone wewe ni mtu wa aina gani, maana huenda ulikuwa unacheza uchi haya ya Nitampiga Kikwete yalipotokea



 
Kama ulitoka sababu hizi JF asee we toka tu. Huna cha maana zaidi ya kujiona unajua kumbe huna lolote

Sasa katika hayo uliyoambatanisha hapo ni wapi umeonesha kikwete alimtuma mwandosya akamsaidie kwa kagame?

Acha undezi basi. Usidhani unajua saaaaaana kumbe Potoma tu
 
Tatizo watu mnarukia propaganda chafu za watu waliokuwa wakimchafua Prof. Mwandosya na mnajitoa akili kabisa. Kumbuka ni watu walipoona propaganda zao hazifanikiwi waliamua kumnywesha sumu ikabidi akae hospitali India miezi karibu sita.

Kama unafikiri Prof. Mwandosya ni mtu ambae angeweza kuhongwa "scholarship" ya mtoto wake ili auze shirika la umma basi huna akili za kukufanya uweze kufikiri. Na kumbuka sponsorship waliyoisema ni pale mtoto wake alienda South Africa study tour, wiki mbili sijui. Kwamba Mwondosya angeshindwa kumgharamia ticket ya economy na kukaa South kwa wiki mbili, ikiwa watoto wake wengine alikuwa akiwasomesha nje ya nchi kwa hela yake? Does it make sense to you?

Japo sina hela kama ya Prof. Mwandosya na mie sio waziri, ili kukuondoa ujinga ningeweza kukukatia ticket ya ndege kwenda South Africa ukakae wiki mbili unakula na kulala tu, ili siku nyingine usiamini kila unachoambiwa, na kukuonyesha kwamba kwenda South Afrika na kukaa wiki mbili ni kitu kidogo sana hata mfanyakazi wa kawaida anaweza kukimudu. Epuka dhana ya kuona ili upande ndege kwenda mahali kama South Africa lazima uwe tajiri kama Dewji na waziri hawezi ku-afford kumlipia mtoto wake safari ya South Africa inabidi ahongwe kuuza shirika ili mtoto wake aende South Africa study tour.
 

Mbona hujauliza ni wapi Mkapa alimtuma Mwandosya? Yaani ulitaka Kikwete atangaze kwamba "jamaani eeeh, namtuma Mwandosya kwenda kusuluhisha ugomvi wangu na Kagame" ili magazeti yaandike?

Hebu tumia akili wewe. Unafikiri mie ningeandika kitu ambacho Samia hajui au hawezi kuuliza, na nikijua Kikwete pia anaweza kusoma? Nitatumiaje point kumshawishi Samia ambazo atajua sio za kweli? Kwamba umeshindwa hata kuwaza hili basi hufai hata kujibishana na mie katika hili. Ukiweza nenda kamuulize Kikwete, au muulize Kagame basi. Au muulize Samia basi, je ni kweli Mwandosya alifanya hili?

Na kuzidi kukuonyesha hujui, angalia hapa chini. Unaelewa kwa nini imeandikwa Mwandosya alitumwa "to learn on how Rwanda plans and implements social and economic services"? Popoma nani sasa?

 
Huu mkataba unapita tu hata asipomtafuta. Ukikaa kusikiliza watu sana yako hayataenda.
 

Ushauri wako ni mzuri, kama mtu ana nia ya kushauriwa. Kuna watu ukiwashauri, wanaona kama unawaendesha au unawaamrisha nini cha kufanya. Ila kama kweli mtu anahitaji ushauri, huyo mtu ukimshauri anapokea ushauri.
 
Hapo ulipoandika kuna MTU MMOJA TU
Yaani Tanzania nzima yenye watu zaidi ya milioni sitini kuna mtu mmoja tu

Ndugu yangu Synthesizer ule uamuzi wa kutokuleta nyuzi hapa endelea nao mana mawazo yako yanakaribia kugota

Yeye kaona huyo mmoja ndo maana kamweka hapa. Kama kuna mwingine unayemjua au kama kuna mtu mwingine anamfahamu mtu ambaye anaweza kumshauri Rais, basi ni ruksa kuweka maoni yako hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…