Rais Samia kupokea ripoti ya miezi mitatu (Januari-Machi) ya Benki Kuu kutoka kwa CAG

Rais Samia kupokea ripoti ya miezi mitatu (Januari-Machi) ya Benki Kuu kutoka kwa CAG

Rais Samia amesema CAG ameshakamilisha ripoti ya CAG kuhusu Benki kuu kwa kipindi cha kuanzia January hadi March 2021 na ataikabidhi kwake siku ya Jumatano au Alhamisi.

Umma utaelezwa yaliyomo ndani ya ripoti hiyo, amesisitiza Rais Samia.

Chanzo: ITV
Imeshaeditiwa hiyo. Katelephone na Ntibazonkiza hawawezi kukosa. Basi tuletewe hiyo hiyo kanyaboya ripoti
 
Wale mnaojiandaa siku ya katiba day, mjiandae pia kupokea ripoti ya CAG ya miezi mitatu Jan-Mach 2021 ya BOT kwasababu Raisi ameshasema kuwa itawasilishwa kati ya Jumatano na Alhamis.
 
Katiba mpya ndio agenda ya kudumu ya watanzania kwa sasa, hakuna namna unaweza kuzima harakati za kudai katiba mpya kwa matukio nk.

Magufuli alijaribu kuzima harakati hizo kwa mtutu wa bunduki bila mafanikio. Na yeye hakuwa wa kwanza, mzee Samweli Sita alijaribu kufanya uhuni pia wa kuchakachua maoni ya wananchi kwa gharama ya kodi za wananchi. Kilichofuata sote tunakijua.
 
Mapendekezo ya hiyo ripoti ni vyema yafanyiwe kazi, isiwe kusomewa tu halafu yakawekwe kabatini, wakishamaliza hiyo kazi kinachofuata ni Katiba Mpya ya watanzania.
 
Tunaimani na mama hiyo katiba mpya kaiandikieni kwenye majumba yenu maana mnataka tugeuza watanzania wajinga sasa

Mkiona hamna agenda mama anaupiga mwingi mnaanza porojo zenu na mkae mkijua mitaa ikimuelewa mama hizo kelele za Katiba mpya mtazipiga peke yenu
 
Back
Top Bottom