Pre GE2025 Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hiyo ni message kwa “wanyonge” wa Tz. Sio kwa wafadhili. Ndio hivyo miaka yote.

Kuna mwaka tuliambiwa profesa wa majalalani akiwa waziri wa mambo ya kigeni, “alimfokea” bila kupepesa macho wala tashwishwi, balozi wa Canada kuwa ndege yetu isipoachiwa uhusiano utatetereka! Strange affairs, indeed!

Ajabu kwenye clip ya ITV isiyo na sauti walionekana wamekaa mkao wa kidiplomasia. Utulivu mwingi, macho hayakuchomolewa, wala mapovu hayakuruka na tabasamu zilionekana kwa mbaali!
 
Kuna ubaguzi ambao nauona ajabu kwa sasa kwamba kuna kundi linalopaswa kuishi na lingine halipaswi kuishi na likiishi liishi kwa taabu.Ila Mungu bado ni Mungu atajibu maombi maana wote amewaumba yeye.
 
Huyu ndie Raisi .Raisi lazima uwe na msimamo .."hatuko hapa kuelekezwa nini cha kufanya"(Tunatumia convection ya kimataifa). MUNGU aendelee kumsimamia raisi wetu.
Msiposimama na Rais mtasimama na nani!???
 

Acha omba omba zako tuone kama utakuwa na budget ya afya mwakani
 
Nimemsikia akisema kuwa haamini kama matamko waliyoyatoa baada ya mauaji ya Kibao yanawakilisha nchi zao. Hajui kwamba wale sio chawa kama wa kwetu, wanaowakilisha nchi zao ndio maana hawawezi hata kushtakiwa. Hili limesaidia kujua watekaji na wauaji wanatumwa nà nani.
Kweli general Mbona ilikosa uzalendo kwa nchi yako
 
Kumbuka siyo wale Mabalozi wa Nyumba 10 wa chama unaowajua . Nadhani hujui kuwa wao wanawakilisha Nchi gani. Siyo Mabalozi wa Burundi au Rwanda , hawa ni zaidi ya wawakilishi.
Yes hicho ndicho,
Lazima waheshimu mila, utamaduni , desturi, katiba na sheria za nchi yetu huru,
vinginevyo wasipobadilika mabalozi hao wote watarudishwa makwao bila mbambambba yoyote
 
Jiwe alituaminisha sisi ni matajiri tutembee kifua mbele, lakini ikifika usiku Waziri wake wa fedha ananyata hadi EU, UK na US na bakuli lake kuomba chochote ili tule, tutibiwe.
 
Yawezekana unasema yanayokufurahisha, lakini yaliyo mbali na ukweli.

Nchi yoyote iwe kwa sababu au bila sababu inaweza kuvunja mahusiano ya kibalozi na nchi yoyote ile, hakuna anayeweza kulizuia hilo. Lakini tendo la kuvunja uhusiano wa kibalozi maana yake ni kutangaza uadui. Na hiyo nchi ambayo balozi wake umemfurusha, unaipa nafasi ya kuwa macho zaidi na Serikali yako.

Lakini hata ukiwafukuza mabalozi wa mataifa yote, hiyo haizuii jamii ya kimataifa kuingia nchini mwako kwa lengo la kuwalinda wanaoonekana wapo kwenye hatari ya kuuawa kwa misingi ya kibaguzi.

Kuweza kuwafukuza mabalozi wote wa nchi za Ulaya, lazima uwe punguani kichaa. Hakuna kiongozi mwenye akili timamu anaweza kulifanya hilo kwani madhara yake hayawezi kupimika. Fikiria Putin, pamoja na ubabe wake wote, pamoja na nchi za Ulaya na America kuipa silaha Ukraine, lakini Putin hajathubutu kuvunja uhusiano wa kibalozi na nchi za Ulaya, wala USA.
Halafu Kesho kiguu na njia kwenda kuomba MKOPO wa kununuua ma V8

Huyu yawezekana anakaribia kuchanganyikiwa. Leo anasema Tanzania ina KATIBA, wakati siku si nyingi alisema kuwa Katiba kwake siyo muhimu, ni kijitabu tu.
 
Kwan wao na sisi nani anamuhitaji mwenzie ??
Tunawahitaji Wao zaidi. Ulisha ona PM wa UK au Chancellor wa Germany au Rais wa France au PM wa Italy au Ureno au Spain au Belgium au Netherlands au Sweden wakija kuzurura hapa kwetu. Bongo ? Viongozi wetu je? amost every month tukiwa na Bakuli. Maovu wana haki ya kuyakemea, na ni kwa msalahi ya wananchi. Kumbuka . Uhai ni Universal Human Right, na sisi ni Signatory wa hii 1948 Convention. Wana haki ya kudai kulindwa kwa Uhai wa mwanadamu regardless ni wa wapi.
 
Ukilaza umeufikisha hadi huku?
Sasa hapa ni kipi cha maana ulich changia?
Acha nyege wewe,una tatizo la akili!?.. unataka ku-prove nini!?..nilikuumiza wapi kiasi unanifuata kila pahala na msamiati wako wa 'kilaza'!?..kuna sehemu ya mwili inakuwasha unataka nikukune!?
 
Hao anaosema kuwa wanaua watu kwenye nchi nyingine si wote wanapatikana na wanahukumiwa. Yule aliyemshoot trump si aliuwawa palepale na hao wengine wote wamepatikana na kufikishwa kama ni mahakamani au polisi. Je, hapa Tanzania nani aliyekamatwa kutokana na hayo matukio yanayoendelea?, kila siku uchunguzi unaendelea, lini uchunguzi ulikamilika ikaonekana hawa ni watuhumiwa.
 
angalizo lielekeze kwa mabalozi wasio zingatia mila,desturi na utamaduni wa host country,

vinginevyo hawatavumiliwa hata kidogo wasipozingatia sheria za kimataifa na ustaarabu wa kidiplomasia. watarejeshwa makwao mara moja 🐒
Usichanganye Mada. Wao wamekemea uvunjwaji wa Haki ya msingi ya mwanadamu, Haki ya Kuishi , ambayo ni Mungu pekee mwenye mamlaka ya kuitwaa. Tuwe fair katika kulaumu na kupongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…