Rais Samia, kwanini unatoa msaada mkubwa kwa Prof. Jay pekee wakati wa kuwasaidia wapo wengi hospitalini?

Rais Samia, kwanini unatoa msaada mkubwa kwa Prof. Jay pekee wakati wa kuwasaidia wapo wengi hospitalini?

Daah Tanzania kuwa mgonjwa mpka upone ni kudra za Mungu tuu..hapo bado hujakutana na wenye maneno wakusemeee mpk dawa ukimeza hazishuki...
 
1. Foundation hiyo tayari imezinduliwa na huna cha kuifanya. Mwamko upo na hata mimi popoma nishatuma mchango wangu

2. Foundation itachangia matibabu kwa makumi ya wagonjwa wa figo lakini pia imeshatoa na inatoa hamasa kubwa kuhusu ugonjwa huo na hivyo kuokoa mamia ya watu. Wizara ya afya ingeamua kufanya hamasa ya kuweka hii awareness unafkiri hiyo kampeni ingegharimu shilingi ngapi?

3. Prof Jay ameamua kuihudumia jamii yake katika hali zote na kwa namna zote mpaka mwisho wa uhai wake. Yeye na Sugu ndio wasanii pekee wenye hiyo crown mpaka sasa

4. Tujaribu kuheshimu sana juhudi za Prof Jay kwa jamii katika muda wake huu wa lala salama. To me,he is a super hero!

Karibuni wenye mapenzi mema tuchangie foundation yake kwa bukubuku zetu kadri tulivyojaaliwa. Watu wenye wivu na majina ya watu tuwaachie ghilba hiyo iwatese mpaka wafe!
Weka muongozo mkuu namna ya kuchangia nichangie misimbazi 15 iwe sadaka yangu. Binafsi mamuunga mkono Prof J katika hilo. Nami ningekuwa mtu maarufu ningefanya hivyo kusaidia wahitaji. Ndugu zangu, kuna watu wana shida sana humu duniani. Pondering, semeni wanaiba na kupiga pesa ila omba sana usiumwe either Cancer, Moyo, kisukari, figo n.k. Nilimuonaga mtoto mmoja ana Kansa ya jicho, Aiseeee eeeeeeeee Mungu tusaidie. Nikikumbukaga kweli hupiga magoti na kumshukuru Mungu kwa ajili ya Afya njema yangu na ya watoto alionipa.
 
Watanzania mna nogwa!!? Hiyo yote inasababishwa na ugumu wa maisha, jamani twendeleeni kutafuta pesa tuache makasiriko ya vitu vidogo vidogo.

Kama mtu uko vzr kiuchumi huwezi kuchukia jamaa yule kwa Hali aliyonayo kuanzia hiyo foundation hata kama pesa yote atakula mwenyewe.
Ni sahihi umeongea kitu kikubwa sana. Umaskini mbaya sana kwani huendana na Roho mbaya. We anzisha uzi humu usema una maisha mazuri au hata useme una gari tu kitu ambacho ni cha kawaida uone makashfa na matusi utakayo ambulia.

Umaskini ni mbaya sana mkuu. Umaskini unaendana na Roho Mbaya. Watanzania wengi ni maskini including wana JF na wana Roho Mbaya ndio maana nyuzi na comments nyingi ni za kuponda na kukashfu kila kitu.
 
Umasikini huwa unafanya MTU kuwa na roho mbaya na kutopenda kuona MTU anafanikiwa.

Prof Jay ataendelea kukaa juu kileleni Kwa mawazo yake mazuri hivyo tutachangia Sana .

Asante mama samiah Kwa UPENDO walk.
 
Watanzania mna nogwa!!? Hiyo yote inasababishwa na ugumu wa maisha, jamani twendeleeni kutafuta pesa tuache makasiriko ya vitu vidogo vidogo.

Kama mtu uko vzr kiuchumi huwezi kuchukia jamaa yule kwa Hali aliyonayo kuanzia hiyo foundation hata kama pesa yote atakula mwenyewe.
Wapumbavu hamtapungua Tanzania na JamiiForums pia.
 
1. Foundation hiyo tayari imezinduliwa na huna cha kuifanya. Mwamko upo na hata mimi popoma nishatuma mchango wangu

2. Foundation itachangia matibabu kwa makumi ya wagonjwa wa figo lakini pia imeshatoa na inatoa hamasa kubwa kuhusu ugonjwa huo na hivyo kuokoa mamia ya watu. Wizara ya afya ingeamua kufanya hamasa ya kuweka hii awareness unafkiri hiyo kampeni ingegharimu shilingi ngapi?

3. Prof Jay ameamua kuihudumia jamii yake katika hali zote na kwa namna zote mpaka mwisho wa uhai wake. Yeye na Sugu ndio wasanii pekee wenye hiyo crown mpaka sasa

4. Tujaribu kuheshimu sana juhudi za Prof Jay kwa jamii katika muda wake huu wa lala salama. To me,he is a super hero!

Karibuni wenye mapenzi mema tuchangie foundation yake kwa bukubuku zetu kadri tulivyojaaliwa. Watu wenye wivu na majina ya watu tuwaachie ghilba hiyo iwatese mpaka wafe!
Sawa changieni tu

Ova
 
Halafu hii ya Mgonjwa ambaye bado anahitaji Matibabu ya Kina kuanzisha Mfuko wake (Foundation) kwa kusema anataka Kusaidia wengine Wengi ni kutaka Kutudanganya wenye Akili Kubwa na kutufanya ni Wapumbavu (Mapopoma) na hili hatutalikubali.

Mwisho GENTAMYCINE natoa RAI kwa wengine kuwa kama unajua bado una Shida, huna Hela au una Madeni mengi ya Hospitalini au Kwingineko (katika Jamii usitumie njia ndefu ya kutaka kujipatia/kuomba Pesa bali sema tu wazi wazi kuwa Umepigika Kimaisha kama GENTAMYCINE hivyo unaomba Msaada ili Watanzania wakusaidie tu na siyo kutumia Usanii Usanii na Mbwembwe nyingi.

Na Foundations nyingi huwa zinaanzishwa na zinanoga pia kama tu Mlengwa akiwa ameshatangulia mbele za Haki (yaani Kafa/ Kafariki) au Kapona kabisa tatizo lake ila siyo Mgonjwa kuanzisha Mfuko wake.

Wengine (GENTAMYCINE nikiwemo) ni kama Bahari ambayo kamwe huwa haikai na haitokaa na Uchafu wowote ule hivyo tukiona kuna tatizo au upuuzi wowote ule mahala fulani siwezi/hatuwezi Kunyamaza au Kulinyamazia.

Mzanaki, Myao na Mtutsi nimemaliza.
Anafanya PR stunt tu! Wapo mafukara wengi kama Prof J, ila hawana umaarufu wa kuuza sura kama wa Prof J! Samia anamtumia tu just for popularity! Jitu limekaa bungeni kwa miaka 5! Mshahara M11+, kila siku posho 250K, kiinua mgongo 350M! Lakini anaugua anakosa pesa ya kulipia matibsbu!
 
Hiyo foundation ikifanya kazi kwa kusaidia wengine nahama hii nchi, watu wanajivika utajiri kwa kisingizio cha Foundation
Muogopeni Mungu

Hali aliyonayo Prof. J nadhani si muda kwake wa kutafuta utajiri.

Maumivu aliyopitia mimi na wewe hatuyajui, na nini anajisikia ndani yake dhidi ya watu wanaopitia maswahibu kama aliyopitia hilo nalo anajua yeye.
 
Anafanya PR stunt tu! Wapo mafukara wengi kama Prof J, ila hawana umaarufu wa kuuza sura kama wa Prof J! Samia anamtumia tu just for popularity! Jitu limekaa bungeni kwa miaka 5! Mshahara M11+, kila siku posho 250K, kiinua mgongo 350M! Lakini anaugua anakosa pesa ya kulipia matibsbu!
Aisee
Mkuu, tema mate chini

Kumbuka ukiugua unakuwa unatumia, hauingizi.

Na kwenye wimbo wake wa shukrani kwa Mungu ameweka wazi gharama za matibabu zilivyokuwa .

Maradhi yanaweza kukutoa kwenye ukwasi hadi kuwa fukara wa kutupwa.. na mbaya zaidi yanakuja pale usipotarajia.

Kama wewe ni mzima mshukuru tu Mungu, kuliko kuanza kubeza wagonjwa.

Prof J Mungu kamjaalia jina,
Acha alitumie kukusanya fedha za kusaidia wanaotaabika wengi wakiwemo hao mafukara unaowasema.
 
Na wewe wasaidie hao wengine,kupanga ni kuchagua,acha kumpangia Rais matumizi ya pesa yake
Kabisa, Kila 1 ana Uhuru wake wa nani anampata pesa, pia kama foundation kitu rahisi anzisha . Na huwezi kutoa malalamiko mleta mada kbl hujaona matokeo ya uanzishaji wake. Tusubiri tuone itafanya Nini? Na karudie kusoma malengo yake. Binafsi naona itasaidia wale waliopata na madhila na hawana msaada, japo maombi ya kusaidiwa ni mengi.
 
Anafanya PR stunt tu! Wapo mafukara wengi kama Prof J, ila hawana umaarufu wa kuuza sura kama wa Prof J! Samia anamtumia tu just for popularity! Jitu limekaa bungeni kwa miaka 5! Mshahara M11+, kila siku posho 250K, kiinua mgongo 350M! Lakini anaugua anakosa pesa ya kulipia matibsbu!
Sema Wewe Mkuu nikisema Mimi naambiwa nina Chuki Binafsi na ninaowasiliba hapa JamiiForums.
 
Mmmh umeamua kumtolea uvivu mgonjwa hakika una tatizo la akili

Anyway mam j aachane na mradi wanguruwe amuuguze mume kwanza
 
Anafanya PR stunt tu! Wapo mafukara wengi kama Prof J, ila hawana umaarufu wa kuuza sura kama wa Prof J! Samia anamtumia tu just for popularity! Jitu limekaa bungeni kwa miaka 5! Mshahara M11+, kila siku posho 250K, kiinua mgongo 350M! Lakini anaugua anakosa pesa ya kulipia matibsbu!
Achaloa mbali Ana pesa za kosota mm huwa nadhani Kuna watu Wana uhitaji mkubwa mno hawan umaarufu wowte wale watu waguzwe jmn Hawa kina proof embu wapige simu mbili tatu tu taayari Yuko India Sasa m.mtu wa ihumwa mapinduzi Hadi nisikike lini jmn ,huo ogonjwa nauogopa mno ila Sasa kwa pro levels zake siyo wa kulia Sanaa

Anyway achangiwe tu na wenye mihoyo hyo
 
Back
Top Bottom