Rais Samia: Mabadiliko ya Viongozi Serikalini yataendelea mpaka mstari unyooke

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema mabadiliko ndani ya Serikali (Aliyoyaita kucheza draft) yataendelea hadi pale mstari "laini" iliyokaa sawasawa itakapopatikana kwenye kila sekta nchini.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Juni 16 2023, wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni Ikulu, Chamwino.

"Bado tunacheza draft la kupanga serikali na ndivyo inavyotakiwa kwa sababu maendeleo ni 'adjustments ' ukiona mambo yanakwama hapa, "una-adjust hapa, unakwenda mpaka unapata ' line iliyokaa sawasawa. Kwa hiyo bado tutaendelea kufanya hivyo mpaka tupate line iliyokaa sawasawa katika kila sekta. - Rais Samia

---
Wanajamvi hili mnalionaje?

 
Lukuvi Waziri Mkuu Mpya
 
Ni dhahiri sasa Mama ameonesha kuwa kazi hii imemzidi uwezo! Kama angekuwa na uwezo na dira ya nini anachotaka kufanya angekuwa na watu sahihi hivi sasa, lakini inaonesha bado anabahatisha na hajui anatupeleka wapi!
 
Anawatafutia watu Ulaji
 
Labda inaweza kukaa saws kama kuna watu watapigwa chini. Sio hii danganyatoto ya kuamisha watu wizara iliyopachikwa jina ya teuzi mpya
 
Huyu rais wenu bhana!

Bado miaka 2 tu ila bado ana adjust selikali?
 
HATA UKIWABADILISHA WOTE HALI NI ILE ILE TATIZO SIO WATU BALI NI MFUMO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…