Rais Samia: Mabadiliko ya Viongozi Serikalini yataendelea mpaka mstari unyooke

Comments reserved
 
Mimi mwanajamvi nimemuelewa sana Mhe. Rais. Watu wanadhani maendeleo ya nchi ni kitu hivi kimoja. Maendeleo ni multidimensional concept. Leo unaweka sawa hapa kesho pale na keshokutwa unaweza ku adjust pale nyuma ili upate mwelekeo sahihi. Kwa hiyo naamini panga pangua panga ni adjustment kufikia malengo ya maendeleo katika sekta tofauti. Huwezi kuteua leo halafu usubiri kuadjust hadi ifike mwaka 2025. 🙏🙏🙏
 
Ili kupata mstari ulionyooka hata yeye Samia anatakiwa kuondoka kwenye nafasi ya Urais, maana hadi sasa ameshindwa kuteua watu wanaojielewa badala yake anateua wapuuzi ambao wamekaa serikalini miaka na miaka na hakuna la maana waliloweza kulifanya kwa maslahi ya taifa.
 
Hawezi kunyoosha mstari ila yeye ndio watamnyoosha muda sio mrefu. Si aliwakumbatia na kuwapa pumziko ? Anawaza kingine wanawaza tofauti mwwisho wa siku scud inashindwa kulinda na missile zinagongana zenyewe na kuleta madhara!!!
 
Mbona hakuna bajeti ya Bunge la Katiba mpya au Samia anatumia ile strategy ya Kinana na kutulaghai Wapinzani.

Samia ajue maandamano makubwa ya kudai Katiba yanakuja.

Hatudanganyiki tena Watanga.
😂😂😂 Hata wewe?!!

Basi kumekaribia kukucha
 
Shida ni yeye kuamua kukaribisha vilaza kwenye Balaza la Mawaziri!
 
Big NO.....mbona waziri wa fedha hanyoshwi ili line ipatikane?
 
Mafisadi kaz kwenu, mmeambiwa mpaka mnyooke 🤣🤣🤣🤣
 
Mama alikua anazunukwa mbuyu, ngoja tuone wanaokuja kama mambo ni yaleyale.
 
Hayawezi kupatikana kama anavyotarajia kwa staili hiyo. Kikubwa awaweke watu wenye uwezo na sio kwa kuletewa vimemo au kwa mahaba au kwa ukada na ushkaji. Haya mambo yalimmaliza Kikwete hadi chama kikataka kumfia mikononi.

Awaachie uhuru na minimal control watu anaowateua wafanye kazi na wasifanye kwa kumfurahisha yeye bali kwa taratibu na maono mapana. Aepuke uchawa.

Hata kwenye kampuni au shirika huwezi kila siku ukawa unaajiri na kufukuza ukitegemea utapata mafanikio.

Atafute cv za watu, azipitie..usalama wamsaidie..aweke siasa pembeni..atapata watendaji.
 
Mbona mawaziri aliwaruhusu kula urefu wa kamba zao...kwamba draft haliwahusu eeh
Wakuu wa wilaya hawana effect kwenye jamii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…