Rais Samia mbona hakubali tatizo nini?

Rais Samia mbona hakubali tatizo nini?

Sa100 uwezo mdogo sana..ndio mana amezima na kuomba genge la wapiga dili waje kumsaidia kazi..ambapo tayari keshazingua wapiga dili lazima wamwangushie zigo la lawama hata amini.

Yawezekana ana malengo mazuri ila timu aliyoichagua kupiga kazi haiaminiki tena kwa watanzania.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kuanzia mskitin,kanisani,kijiweni, bar,masokoni, bodaboda uku kwetu tunamkubali kinomaaaaa.
Piga kazi mama tumecheleweshwa mnooo kama taifa. Zaidi ya miaka tulikwama tu. Kisa mtu mmoja
Apige kazi gani..ebu nionyeshe kazi hata tatu tu za msingi alizo piga mpka sasa...kama sio kutembelea reli ya jpm.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwanini watu hawasemi ukweli kuwa Samia hakubaliki Bali wanapiga propaganda tu?

Kuanzia masokoni, vijiwe vya kahawa,mitaani ,maofisini mama hakubaliki ,shida Ni nin jaman?

Juzi tukiwa ofisini karibu staff members Kama 15 ,ikawashwa redio ,mama alikuwa anahutubia ,sijui Ni Tabora hiyo, aisee staff walikuja juu ,redio izimwe ,Hakuna anachoongea Cha maana ,Walidai hivo,

Huku wakisema Wamemis sana Hotuba za Jpm ,

Hii hali niliichukulia kawaida,lkn nenda hata masokoni, mfano Mabibo sokon, manzese, nenda machinjion vingunguti, Mama anazungumzwa vibaya, anaonekana anafeli sana

Wananchi wengi wanaamini maendeleo yanaenda kwa mwendo wa Kobe,

Wanaamini wez wamerudi serikalin,

Wanaamini Jpm alikuwa mtetez wao,

Wanaamini Kuna kund limemuondoa mwendazake

Kiukweli hata wewe ulipo hapo Kama mpo 10, jaribu ufanye utafiti,uone Ni namna gan mama anakubalika ,

Utaleta majibu hapa ,

Ninachojiuliza huyu mama kwann hakubaliki ,je sio presidential material?

Au Hana maono na nchi hii Kama alivyokuwa Jpm?

Ukiangalia jins Jpm alivyotuvusha kwenye Corona , unaona KABISA angekuwa huyu mama tungekuwa wapi?

Kuna mtu huwa ananiambia msimamo wa chanjo kwa watanzania ndio Iman ya Watu kwa Jpm ,

Hadi Sasa propaganda za chanjo zimefeli , huku majority wakiendelea kuamini falsafa za Jpm ,ambazo hata Korea wameanza kuzitumia




Swali kwann huyu mama hata Hotuba zake zinapuuzwa ,?

Kipind Cha JPM watu had kwenye bodaboda wanatega masikio ,waone mwamba ataongelea mradi gan mpya, mwizi gan atatumbuliwa,

Huyu mama Hotuba zake zinapuuzwa ,kwasasa watu wapo tayari kumsikiliza haji manara na sio raisi,tatizo nn?
Sukuma gang bwana mnatapatapa Sana.
 
Apige kazi gani..ebu nionyeshe kazi hata tatu tu za msingi alizo piga mpka sasa...kama sio kutembelea reli ya jpm.

#MaendeleoHayanaChama
Tutajaza Seva bure..

Unataka kwenye sekta gani nikumiminie mambo?

Screenshot_20220328-115637.png


Screenshot_20220328-114505.png


Screenshot_20220327-172335.png


Screenshot_20220514-075608.png


Screenshot_20220517-092017.png


Screenshot_20220517-091836.png


Screenshot_20220517-220756.png


Screenshot_20220521-220800.png


Screenshot_20220521-221503.png
 
staff ya wapi hiyo? Ni bora huyu mama mara mia japo anapuyanga kuliko Jiwe.

Uhuru tu wa kufanya mambo yangu bila hofu ya kutekwa inatosha, mama dhibiti vibaka tu na hawa panya road kura tutakupa
Husibishe SSH, anafanya vzr kuzidi Jiwe,lakn katika kukubalika hakubaliki,Hadi mwwnyewe nashangaa
 
Kuna Ka Ukweli Kidogo!
1. Hotuba zake 2.Anatakiwa aachane na yake aliyoyafanya Magufuli 3. Aachane na Wapambe wanao force kumtukuza!(hili linawafanya wengi wamwone na yeye kama yule aliemtangulia)4. Aje na ufumbuzi wenye maana na sio Brabra kwenye ajira(inawezekana tena kwa yeye anaweza kwa 100%)5.Aje na Ufumbuzi wa kupanda kwa garama za maisha ambazo zitaendelea ongezeka zaidi miezi inayokuja(pia hili analiweza)6. Aongeze matumizi ya Ges yetu asilia kwenye shughuli za uchumi hapa Tanzania (kuokoa pesa 7.Aje na Solution za kudumu kwa Machingazi na Boda boda nchi nzima( hili ni Time Bomb-soon litalipuka kama hatua staiki azitochukuliwa) 8. Watanzania wa Leo sio wale wa kuwagawai T shirt na Ubwabwa ili wakupe Kura, Au wale wa kumchaguwa Kiongozi kwa Propaganda na kupiga kelele kwenye Media ANATAKIWA AJE NA MBINU MPYA KAMA ATATAKA USHINDI WA KISHINDO NA. WA HAKI NA HALAL 2025!! Tanzania ya Leo sio ile ya Nyerere,Mwinyi,Mkapa au JK: Mindset za Watanzania zinagrow kila kukicha- mfano Kesi ya Mbowe na Wenzake imeitangaza Chadema kuliko kuifukia,Social Media sio za kuzipuuza tena. Habari na Matukio yanasambaa kwa haraka mno na state control ya Media kama zamani(Kukontrol nini kitangazwe Redioni au Magazetini Aipo kwenye Internet) Watanzania tena wale watakaokuwa kwa mara ya kwanza ni wapiga kura 2025 awatokuwa wale wanaoshawishika kumpa kura kiongozi kwa maneno Tuu! KUNA AJA KUJIPANGA NA KUFANYA MENGI YEYE KULETA NAFUU YA KIUCHUMI KWA WATANZANIA WOTE NA KURUDISHA FURAHA
 
Samia anafanya vzr Sana kuliko Jiwe,lakn ukweli wananchi hawamkubali
Achana nao hao.Wengi wa wanaoonesha chuki kwa SSH ni masikini.Hawa walikuwa wanafurahia matajiri,wafanyabiashara na watumishi wa umma kuumizwa na kufanyiwa dhulma.Kwa akili zao nyembamba walidhani hayo makundi yakifanyiwa udhalimu ndiyo watalingana nao kuuishi ufukara.Akili za kimasikini kama mpendwa wao jiwe!Tell them to go to hell!
 
Anapelekeshwa na nani?Na ni kuhusu nini?Maana uswahilini mkikaa mnajitungia maneno tu ili mradi yasindikizie togwa mnazokunywa.
Kuwa makini na hizo ID zingine unazozijibu, yani zinang'ata kote kote kama konokono.

Zipo kama zaidi ya 100 na ushee, kuna namna humponda Rais kwa uongozi wake mbovu, pia wakati huo huo humsifia Rais kwa ID hizo hizo [emoji23]
 
Husibishe SSH, anafanya vzr kuzidi Jiwe,lakn katika kukubalika hakubaliki,Hadi mwwnyewe nashangaa
Chuki binafsi zimewazidi hao mbwa wa Sukuma gang..

Sekta yeyote unayoijua wewe hapa Tanzania kuanzia Kilimo hadi Barabara na habari Samia kafunika...

Unfortunately hakuna mgombea atamshinda Samia kwa namna yeyote,kama wanaye waambie wamuweke hapa .

Ona hapa kwenye sekta ya Habari 👇

Screenshot_20220521-215809.png


Screenshot_20220521-215733.png


Screenshot_20220521-215651.png


Screenshot_20220521-215605.png


Screenshot_20220521-215536.png


Screenshot_20220521-215443.png


Screenshot_20220521-215409.png


Screenshot_20220521-215328.png


Screenshot_20220521-215312.png


Screenshot_20220521-215243.png


Screenshot_20220521-215206.png


Screenshot_20220521-215109.png


Screenshot_20220521-215025.png


Screenshot_20220521-213837.png
 
Back
Top Bottom