Rais Samia Mgeni rasmi Mashindano ya Kuhifadhi Quran tukufu

Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya dunia ya kusoma Quran Tukufu, yatakayofanyika nchini katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Februari 23, mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam, Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zuberi, amesema kuwa mashindano hayo yanatarajia kushindanisha mabara matano, Afrika, Asia, Arabu na Ulaya.

Amesema hayo ni mashindano ya kwanza kuhudhuriwa na mabara mengi, kwa kuwa inatokana na sera na juhudi za Rais Samia, kuimarisha urafiki na undugu pande zote za dunia.

Aidha alitoa wito kwa wazazi kujikita kwenye malezi bora, yakiwamo kuwaelekeza watoto kwenye elimu ya dini, ili kuwe na taifa bora na makini lenye kumuogopa Mungu, kwani dini ndio mwongozo wa maisha.

Mwakilishi wa Balozi ya Saudi Arabia, Shehe Mutab Bin Azamay Suleiman, amesema wanaushukuru uongozi wa Tanzania unaoongozwa na Rais Samia, kuwa nchi ya mfano yenye utulivu na amani hadi mashindano hayo makubwa kufanyika nchini.

mesema tayari Waziri Mkuu wa Saudi Arabia ameshasaini mikataba ya kusaidiana kati ya BAKWATA na serikali ya Saudi Arabia na matunda yameaanza kuonekana, kwa makubaliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Mwandaaji wa Mashindano hayo, Shekhe Othuman Kaporo, amesema mashindano yataongozwa na kuhudhuriwa na Imam Mkuu wa Msikiti wa Saudi Arabia wa Madina, Shekhe Abdallah Buaijan, na kwa mara ya kwanza Tanzania kupata ugeni huo.

Amesema washiriki wataweza kujinyakulia zawadi mbalimbali, zikiwamo magari, bajaji, pikipiki na tiketi za kwenda kuhiji Mji Mtakatifu ‘Mecca’.

Pia wahudhuriaji watakaofika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa wataweza kuangalia na kupima afya zao bure, kwa magonjwa yasiyoambukiza.

Source: Nipashe
Huwa nashangaa kwanini hayafanyiki kwenye nchi za kiislam!
Kuna ajenda gani?
 
Quran ni copy and paste ya Biblia.
Biblia ndio kitabu pekee ambacho Mwenyezi-Mungu anakiheshimisha mbinguni na duniani.
Kama ni copy and paste mbona Moja inasema " hawakumuua wala hawakumsulubu" kwengine wanasema walimtundika akiwa na nepi na kumcharaza mijedeli akafufuka siku ya tatu. Mafundisho ya kule nikua hajafa isipokua amepaa mbinguni atakuja kufa atakaporudi kwa mara ya pili ulimwengu utakapokaribia kumalizika.
Kuthibitisha ile kauli" KULUN NAFSI DHAAIKATUL MAUT"
= KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.
Amezaliwa chini shina la tende~amezaliwa kwenye zizi la ng'ombe
 
Hio comment ina tatizo gani mpaka utoe povu are you sick????is it serious?,there are hospitals everywhere. Don't die we still need your empty head

Nani tena kakuudhi huyo dada ake? Maana sio kawaida yako.

Anyways msahemehe bure huyo kwa sababu, .miafrika ndivyo tulivyo
 
Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya dunia ya kusoma Quran Tukufu, yatakayofanyika nchini katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Februari 23, mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam, Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zuberi, amesema kuwa mashindano hayo yanatarajia kushindanisha mabara matano, Afrika, Asia, Arabu na Ulaya.

Amesema hayo ni mashindano ya kwanza kuhudhuriwa na mabara mengi, kwa kuwa inatokana na sera na juhudi za Rais Samia, kuimarisha urafiki na undugu pande zote za dunia.

Aidha alitoa wito kwa wazazi kujikita kwenye malezi bora, yakiwamo kuwaelekeza watoto kwenye elimu ya dini, ili kuwe na taifa bora na makini lenye kumuogopa Mungu, kwani dini ndio mwongozo wa maisha.

Mwakilishi wa Balozi ya Saudi Arabia, Shehe Mutab Bin Azamay Suleiman, amesema wanaushukuru uongozi wa Tanzania unaoongozwa na Rais Samia, kuwa nchi ya mfano yenye utulivu na amani hadi mashindano hayo makubwa kufanyika nchini.

mesema tayari Waziri Mkuu wa Saudi Arabia ameshasaini mikataba ya kusaidiana kati ya BAKWATA na serikali ya Saudi Arabia na matunda yameaanza kuonekana, kwa makubaliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Mwandaaji wa Mashindano hayo, Shekhe Othuman Kaporo, amesema mashindano yataongozwa na kuhudhuriwa na Imam Mkuu wa Msikiti wa Saudi Arabia wa Madina, Shekhe Abdallah Buaijan, na kwa mara ya kwanza Tanzania kupata ugeni huo.

Amesema washiriki wataweza kujinyakulia zawadi mbalimbali, zikiwamo magari, bajaji, pikipiki na tiketi za kwenda kuhiji Mji Mtakatifu ‘Mecca’.

Pia wahudhuriaji watakaofika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa wataweza kuangalia na kupima afya zao bure, kwa magonjwa yasiyoambukiza.

Source: Nipashe
Hayati JPM katika ubinadamu wake alihudhuria mojawapo ya hizi shughuli za waislam.

Aliposalimiana na JK nakumbuka Mkwere alimtazama kwa jicho fulani la kumuona kama vile kapotea njia, lakini walikuwa marafiki wa muda mrefu.
 
Waislamu ni watanzania kama walivyo wengine.....

MFARIJI MKUU wa dola yuko nao kama alivyokuwa nao hao wengine......

Kila la heri katika mashindano haya ya "quraan il adhwimu fi lauhil mahfudhwi...."

#Rais Samia ni MFARIJI mkuu wetu !
 
Ni kitabu ambacho Allah alimteremshia Mtume wake Isa(a.s) awafikishie wana wa Israel ili kusadikisha yaliyopo katika taurat na kuwabashiria Mtume ajaye baada yake aitwae Ahmad.
issah na biblia kipi cha kwanza kuwepo ? unajua biblia imeandikwa kabla ya issah ?inasikitisha sana anyway nime kupima nimeona huna unachokijua ila unajaribu kujibu hivyo hivyo ili mradi umenijibu tu, naomba tuishie hapa naona utanipotezea tu muda wangu.
 
Unamjua Issa(a.s)?
Tuanzie kwanza hapo
 
Back
Top Bottom