Rais Samia: Mikoa ya Kusini watu wanatokwa damu puani na kudondoka. Hatujui ni ugonjwa gani, uchunguzi unaendelea

Rais Samia: Mikoa ya Kusini watu wanatokwa damu puani na kudondoka. Hatujui ni ugonjwa gani, uchunguzi unaendelea

Nashauri tupunguze uchomaji mkaa, tuboreshe huduma za umeme na gas
MnavyoambiwaTanzania ni nchi maskini unafikiri mnaongopewa?
80% ya wananchi hawana huo uwezo wa kutumia umeme na gasi kupikia. Sababu kubwa ni gharama. Usikiri watu wanapenda kutumia kuni na mkaa.

Mm mwenyewe tu muajiriwa natumia gas na mkaa kwa pamoja, ili kukwepa gasi kuisha haraka. Maana kila mwezi najaza 60000. Leo useme niache kutumia mkaa Ina maana lazima kwa mwezi nijaze mara mbili hadi mara 3, ntaweza?
 
Rais Samia Hassan amesema kuna maradhi ambayo hayakuwepo siku za nyuma lakini yanajitokeza siku za karibuni kwa kuwa uharibifu wa misitu unasababisha Viumbe wa Msituni wasambae kwa Wanadamu

Amesema “Nilikuwa nazungumza na Waziri Mkuu juzi, ametoka ziara Mikoa ya Kusini (Lindi), ameniambia ameona maradhi mapya yameingia. Watu wanatokwa na damu za pua na wanadondoka chini”

Rais anaongeza "Hatujui ni kitu gani, Wanasayansi wamehamia huko kwa uchunguzi zaidi kwa kuwa ni Watu wengi wanaougua kwa mfululuzo, na yote ni kwa sababu tunaharibu makazi ya viumbe kule walikowekwa na Mungu. Tunawasogeza kwetu wanatuletea maradhi”

Rais Samia amezungumza hayo leo, Julai 12, 2022 katika Maadhimisho ya Mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika Mashariki (AMECEA)
Mbona sisi tuko kusini huku,na hajui Kama Kuna kitu Cha namna hiyo,
 
Sasa watatukimbia wanaifuata royal tour kwa maladhi.
 
Rais Samia Hassan amesema kuna maradhi ambayo hayakuwepo siku za nyuma lakini yanajitokeza siku za karibuni kwa kuwa uharibifu wa misitu unasababisha Viumbe wa Msituni wasambae kwa Wanadamu

Amesema “Nilikuwa nazungumza na Waziri Mkuu juzi, ametoka ziara Mikoa ya Kusini (Lindi), ameniambia ameona maradhi mapya yameingia. Watu wanatokwa na damu za pua na wanadondoka chini”

Rais anaongeza "Hatujui ni kitu gani, Wanasayansi wamehamia huko kwa uchunguzi zaidi kwa kuwa ni Watu wengi wanaougua kwa mfululuzo, na yote ni kwa sababu tunaharibu makazi ya viumbe kule walikowekwa na Mungu. Tunawasogeza kwetu wanatuletea maradhi”

Rais Samia amezungumza hayo leo, Julai 12, 2022 katika Maadhimisho ya Mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika Mashariki (AMECEA)
Yeye anamuamini vipi waziri mkuu ambaye kitaifa haaminiki kutokana na kauli zake kumsaliti?....atumie reference nyingine otherwise hizo ni fix za mheshimiwa PM.
 
Angesubiri wataalamu waje waseme ni ugonjwa gani. Hii itazua taharuki hata kwa wageni wanaokuja
Bora azue taharuki kuliko kuficha maradhi. Wapo walio ficha maradhi na mauti ikwaumbua
 
Huyu mama ana laana kabisa siyo bure ...RIP JPM
 
Hujui ni ugonjwa gani, unasababishwa na nini, how it infect human, umeanzia kusini kwetu au imported; lakini tayari umehitimisha chanzo chake ni kuingilia biodiversity ya wanyama pori huna supporting evidence ya virus kuruka kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Wewe nadhani ni miongoni mwa watu wachache walioelewa hotuba ya Rais.,,,,ametumia Sanaa kuwasilisha ujumbe wake.....Na walengwa watakuwa wameshamuelewa....

Huwezi kutojua Ugonjwa lakini ukajua chanzo chake.....
 
Hujui ni ugonjwa gani, unasababishwa na nini, how it infect human, umeanzia kusini kwetu au imported; lakini tayari umehitimisha chanzo chake ni kuingilia biodiversity ya wanyama pori huna supporting evidence ya virus kuruka kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Nimeshangaa sana, sasa uchunguzi wa njni?
 
Ndio kwa sababu kinachotokea ni virus ambao traditionally wanaishi kwa wanyama pori kupata new hosts (binadamu) kwa njia tofauti all of which entails kuingilia mazingira yao.
Kuwala haiwezi kuwa njia ya kupata new host..ambayo si lazima wawe virusi!!!?
 
Back
Top Bottom