Rais Samia mpaka sasa hujaanzisha mradi wowote wa kimkakati. Je, tuendelee kusubiri?

Bangi mbaya Sana, SASA MLITAKA MIRADI MIKUBWA KARIBU 4, AMBAYO IMEACHWA IMEACHWA NA MAREHEMU ITELEKEZWE NA AANZISHE MIPYA?, KUMBUKA RAIS WA SASA NI KIONGOZI MKUU NDANI YA AWAMU YA TANO, MIRADI ILIACHWA KATIKA HALI YA 25%,KUFIKIA KUKAMILIKA HIVYO 75% ZA UKAMILISHAJI WAKE NI LAZIMA UTEKELEZWE NA UKAMILIKE, NDIPO SASA TUANZE MIRADI MIPYA YA KIMKAKATI.
 
..uchumi wa Tz ukikua kwa 6.1% ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

..ili Watz watoke ktk lindi la umasikini uchumi wetu unatakiwa ukue kwa zaidi ya 10% kwa kipindi kirefu.

..hayo ni maoni ya wachumi waliobobea akiwemo Dr.Mpango ambaye alitoa maoni hayo wakati akiwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango.
 
Hakuna kumi bila kuanzia 1,23,...6 nk Jambo la msingi uchumi unakua.

Swali: Nini maana ya mradi wa kimkakati.
 
Hakuna kumi bila kuanzia 1,23,...6 nk Jambo la msingi uchumi unakua.

Swali: Nini maana ya mradi wa kimkakati.

..ndio maana tuko ktk mkwamo.

..mradi wa kimkakati naamini ni maneno tu ya ujanja-ujanja ya Ccm.

..tuite mradi wa reli, umeme, kilimo, etc
 
..ndio maana tuko ktk mkwamo.

..mradi wa kimkakati naamini ni maneno tu ya ujanja-ujanja ya Ccm.

..tuite mradi wa reli, umeme, kilimo, etc
Hatujakwama popote na tunasonga mbele ila speed inatakiwa kuongezeka.

Wanaotakiwa kuwa kazini ilimwapige kazi uchumi ukue na umaskini upungue zaidi eti wanaandamana kana kwamba maandamano ndio yatawapa maisha, upumbavu.
 
..wachumi wanasema ili tujikwamue lazima uchumi ukue kwa 10%++.

..wanaoandamana wanaichagiza serikali na chama tawala waje na mikakati bora zaidi ya kukuza uchumi.

..kwa miaka kadhaa sera za Ccm zimeshindwa kukuza uchumi kwa zaidi ya 7%.

..Vision 2025 ilikuwa na malengo kwamba by mwakani pato la watastani liwe usd 3000.

..waandamanaji sio wapumbavu, wana hoja za msingi.
 
Nchi haijawahi kosa Mikakati Bora,waache ujinga wa kuandamana na hoja za kipuuzi Waendelee kufanya kazi,umeme ni bwerere hakuna pa Kupeleka.

Kinachoitwa Demokrasia ni ujinga hapa Afrika,wa kufikisha hiyo vision sio Serikali Bali watu kufanya kazi badala ya mdomo mwingi na kuandamana.
 
Nchi haijawahi kosa Mikakati Bora,waache ujinga wa kuandamana na hoja za kipuuzi Waendelee kufanya kazi,umeme ni bwerere hakuna pa Kupeleka.

Kinachoitwa Demokrasia ni ujinga hapa Afrika.

..Nchi imekosa mikakati bora ndio maana uchumi wetu haujawahi kukua kwa zaidi ya 7%.

..Tanzania hakuna demokrasia, kuna kiini macho cha demokrasia.

..Mfano mdogo;kwenye demokrasia za kweli, serikali hubembeleza,na kuwanyenyekea, wabunge. Hapa Tanzania wabunge wanaipigia magoti serikali. Matokeo yake hakuna uwajibikaji.
 
Amekushambulia kihalali sababu swali lako halina msingi.
Ni miaka mitatu tu yupo madarakani akimalizia awamu ya hayati boss wake ( Magufuli). Kitendo cha kukamilisha tu hii miradi atakuwa ameacha alama, hana haja hata ya kuanzisha mingine.
 
Afrika haihitaji kubembeleza wapuuzi wanaoandamana badala ya kufanya kazi.

Mwisho Tanzania haijawahi ishiwa Mikakati Bora ni Kwa sababu watu wameendekeza mdomo badala ya kufanya kazi.
 
Mnamlaumu bure Mama wa watu!!! Miradi ya JPM pekee ilikuwa too much kwa uwezo wa nchi!! Mwacheni amalizie hiyo kwanza. Sidhani kama yeye anaongoza kwa kushindana na kutaka sifa!!!
 
Afrika haihitaji kubembeleza wapuuzi wanaoandamana badala ya kufanya kazi.

Mwisho Tanzania haijawahi ishiwa Mikakati Bora ni Kwa sababu watu wameendekeza mdomo badala ya kufanya kazi.

..Maandamano yasiyo na maana ni kama yale ya mbio za mwenge.

..Maandamano ya kupinga ugumu wa maisha, na mkwamo wa uchumi, ni jambo la kutiwa shime.

..Ni lazima Watz tuwe na ujasiri wa kuwaonyesha watawala wetu kwamba haturidhiki na utendaji wao na namna wanavyotuongoza.

..Tanzania imekwama kutokana na sera mbaya za kiuchumi za vyama vya Tanu na Ccm. Hali imekuwa hivyo toka awamu ya kwanza m
 
Sera zilizokukwamisha wewe ni zipi?

Tanzania Kuna ugumu wa Maisha? Unalinganisha na wapi kufikia hiyo conclusion?

Mnaendekeza usengerema badala ya kufanya kazi?
 
Una maana gani unaposema miaka 10 ya uongozi wake? Kulingana na Katiba iliyopo Samia hawezi kuongoza zaidi ya 2030.
 
Wakumbushe ujenzi wa barabara kwa EPC+Financing 🤣🤣
Hiyo miradi ya EPC + Financing ilikua usanii tu haipo hiyo .nimemsikiliza Waziri bashungwa anapiga blah blah tu pale bungeni.
 
Amekushambulia kihalali sababu swali lako halina msingi.
Ni miaka mitatu tu yupo madarakani akimalizia awamu ya hayati boss wake ( Magufuli). Kitendo cha kukamilisha tu hii miradi atakuwa ameacha alama, hana haja hata ya kuanzisha mingine.
Ila huoni wananchi kila wakiiona train ya umeme wanamtaja marehemu magufuli 🤣 . Mtoa mada ana hoja
 
Mnamlaumu bure Mama wa watu!!! Miradi ya JPM pekee ilikuwa too much kwa uwezo wa nchi!! Mwacheni amalizie hiyo kwanza. Sidhani kama yeye anaongoza kwa kushindana na kutaka sifa!!!
Lakini serikali ina pesa na yeye aanzishe miradi mikubwa huoni wananchi wakiona SGR wanamshangilia marehemu magufuli 🤣 mtoa mada ana hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…