Rais Samia mpaka sasa hujaanzisha mradi wowote wa kimkakati. Je, tuendelee kusubiri?

Rais Samia mpaka sasa hujaanzisha mradi wowote wa kimkakati. Je, tuendelee kusubiri?

Mnamlaumu bure Mama wa watu!!! Miradi ya JPM pekee ilikuwa too much kwa uwezo wa nchi!! Mwacheni amalizie hiyo kwanza. Sidhani kama yeye anaongoza kwa kushindana na kutaka sifa!!!
Maendeleo ya nchi siyo kutaka sifa ni kuleta maisha bora. Unaposema miradi ya JPM ilikua too much kwa uwezo wa nchi unatumia kipimo gani kupima uwezo wa nchi? Mbona Rais anatembea na kundi la wafanyabiashara kuzunguka nchi mbalimbali huko duniani anasema anakwenda kututafutia pesa au akienda hazipati anarudi mikono mitupu?
 
Nawatakia heri wafanyakazi wote.

Mh. Rais nachukua fursa hii kukumbusha tu tangu uingie madarakani baada ya kifo cha Rais John Pombe Magufuli haujaanzisha mradi wowote mkubwa wa kimkakati. Kazi inaendelea kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na marehemu Magufuli ambayo ni ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme SGR , Bwawa la umeme la mwalimu Nyerere, Ujenzi wa vivuko, madaraja pamoja na miradi mingine midogo midogo.

Nakukumbusha tu kuwa mpaka sasa unatembelea nyota ya marehemu John Pombe Joseph Magufuli. Unahitaji kuweka alama yako. Aidha nikupongeze kwa kuwaongezea watumishi mishahara, kujenga madarasa, kuongeza vifaa tiba na ujenzi wa vituo vya afya. Watanzania bado tunakusubiri.

Nakutakia utekelezaji mwema.
Mfano, mumeo akianzisha mradi wa familia bahati mbaya akafariki.
Wewe utaamua kuuacha uanzishe wako ilimradi tu uwaambie majirani kuwa umeanzisha mradi wako.

Pevuka jombaaa.
 
Anaanzisha miradi ya familia yake tu, unadhani anatuwazia waTanzania kweli huyo..?
 
Mwenye macho haambiwi tazama.

Hauelewi maana ya "kazi iendelee"?
Tukitazama hatuoni hiyo miradi mikubwa ya kimkakati kama ya mtangulizi wake. Leo hii watanzania ikipita train ya mwendokasi wanamshangilia Magufuli. Kumbe JPM alikua na vision kubwa Je samia yeye hatamani akiondoka akumbukwe kwa kuwaachia watanzania Miradi mikubwa mikubwa ya kimaendeleo? Siyo miradi ya kujenga vyoo na madarasa au kununua dawa za malaria.
 
Mfano, mumeo akianzisha mradi wa familia bahati mbaya akafariki.
Wewe utaamua kuuacha uanzishe wako ilimradi tu uwaambie majirani kuwa umeanzisha mradi wako.

Pevuka jombaaa.
Hii topic imekuzidi uwezo waachie wenye akili wajadili.
 
Nchi haijawahi kosa Mikakati Bora,waache ujinga wa kuandamana na hoja za kipuuzi Waendelee kufanya kazi,umeme ni bwerere hakuna pa Kupeleka.

Kinachoitwa Demokrasia ni ujinga hapa Afrika,wa kufikisha hiyo vision sio Serikali Bali watu kufanya kazi badala ya mdomo mwingi na kuandamana.
Dah! bila shaka uko mahali pema sana kwa kweli; sio kwa dharau hizo. Yaani serikali ihodhi na kufuja fedha za umma kwa matumizi ya ovyo na ufisadi. Inatunga na kusimamia sheria kandamizi. Halafu unadai ni jukumu la wananchi “kufanya kazi badala ya mdomo mwingi” ili kutimiza vision ya maendeleo ya nchi? Unaona mazingira ya kazi na maisha ya wafanyakazi yako vyema kabisa? Kwamba tatizo lao ni mdomo?

I had some respect for you guy kwa jinsi unavyowasilisha taarifa detailed. Lakini sasa naona you’re just part of the bigger problem of this country. Tuna utawala wa kilaghai usiojali kabisa mustakabali wa nchi na watu wake. Wenye jeuri ya kuwasemea ovyo Watanzania. A self-serving ruling clique!
 
Back
Top Bottom