Rais Samia mpaka sasa hujaanzisha mradi wowote wa kimkakati. Je, tuendelee kusubiri?

Na bado miradi ikikamilika kuna madeni makubwa ya kurejeshwa kutokana na mikopo iliyokamilisha miradi.
Kazi anayo
 
Kwa hiyo sisi tunaosema anaupiga mwingi hakuna wa mfano wake tangu Uhuru unatuambiaje
Upo sahihi,ila anaupiga mwingi kwenye yapi?.. Kuleta Chanjo iliyopingwa awamu ya5,kufukuza wamachinga mitaani,kuchoma masoko mbambali nchini,kuruhusu wizi na ufisadi+rushwa,kutumia kodi zetu kwa safari nyingi za nje + msafara mkubwa kusiko na tija,n.k.,..Una maanisha anaupiga mwingi kwenye miradi hii,au ipi?
 

Kwa maana hiyo unataka tuamini kuwa kama JPM angekuwepo bado angekuwa anaendelea na miradi hii mpaka leio na kusingekuwepo miradi mingine mipya....!!?
 
Mwenye macho haambiwi tazama.

Hauelewi maana ya "kazi iendelee"?
 
Nasubiri rais atayekuja na hii sera huyo atapata kura yangu ..
 
Nasubiri rais atayekuja na hii sera huyo atapata kura yangu ..
 
Ila we jamaa huwa ni kiazi sana.

Jamaa anakuambia uhalisia umebaki kuleta ngonjera, nchi masikini kama hii inahitaji kasi ya ukuaji wa uchumi kwa haraka.
 
Ila we jamaa huwa ni kiazi sana.

Jamaa anakuambia uhalisia umebaki kuleta ngonjera, nchi masikini kama hii inahitaji kasi ya ukuaji wa uchumi kwa haraka.
Uhalisia upi aliousema? Unaandamanana Kwa Ajili ya nini hasa?
 
Well said comrade
 
Utaanzishaje miradi mipya ilhali miradi chungu nzima uliyoikuta haijakamilika?

Vilevile msijisahaulishe ,raisi ni mama sio sawa na baba, na kwa namna aliyoingia kushika uongozi! Mbona kwa nchi zingine yangetokea machafuko!!
 
Nani kakwambia kuwa serikali ina pesa? Mngejua yanayoendelea huko kwenye serikali mngenyamaza tu kimya!!!
Mbona viongozi wanapishana tu Airport, wabunge wanakesha dodoma kwani yanayoendelea huko serikalini ni yapi?
 
Uthubutu siyo makalio ambayo kila mtu anazaliwa nayo!

Kwani wenzie hawakukuta miradi ya watangulizi wao? Mbona walianzisha ya kwao ndani ya miaka miwili ya uongozi wao!

Huyu asingekuta SGR na hiyo HEP under construction sidhani kama angekuwa hata utashi wa kuvianzisha.
 
Hata rais Magufuli alipokea miradi viporo na akanzisha miradi mikubwa mipya. Mpaka sasa Rais samia anaanza mwaka wa 4 huu Ikulu sijaona mradi wowote mkubwa ambao ameuanza.
 
Amekushambulia kihalali sababu swali lako halina msingi.
Ni miaka mitatu tu yupo madarakani akimalizia awamu ya hayati boss wake ( Magufuli). Kitendo cha kukamilisha tu hii miradi atakuwa ameacha alama, hana haja hata ya kuanzisha mingine.
Marehemu Rais magufuli alianzisha Ujenzi wa miradi hii mikubwa akiwa ana miaka mitatu ya uongozi wake huku akitekeleza miradi viporo ya watangulizi wake. Mpaka sasa Rais samia yupo kimya tunaona anazunguka tu huko duniani anasema anaenda kututafutia hela sijui huko nje kuna watu wanatoa hela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…