Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Wewe unaongea nini?? Sisi ndio hao wananchi sasa. Sisi wananchi hatutaki kuhadaliwa na Genge la wahuni wachache. Watoto wetu wanasoma bure kabisa na maisha yanakwenda. Leo mnataka tuwaruhusu kina mbowe waturubuni tuanze kudai vitu vya ajabu kwa maslahi yao ili wao tu waingie madarakani???

We are better than that ndugu yangu na wala hatutoingia huo mkenge
Watoto wenu wanasoma bure, aisee, ccm inaalibu Sana vipaji ,

Elewa hakuna elim bure Tz , ni Siasa, ila ata iyo mnaoita elim bure pia watoto wanatoka bure,

Mbona Nyie hampeleki watoto wenu kwenye shule izo za bure, ACHA propaganda uchwara, unaleta chakochoko za elim bure wakati hamna kitu, kipaji Chako sio Cha kukaa ccm basi tu unalazimisha, karibu CHADEMA mkuu
 
Hawa wanajifanya wehu hawa.

Dawa yao ni kwenda nao hivyo hivyo kiwehu wehu.

Yaani mama aache kushughulikia Watanzania wote wapate umeme aanze kushughulikia matakwa yao wao. Ikifika 2025 waanze kumuuliza mbona umeme hakuna????

Tutakwenda nao wanavyotaka wao

Na wehu wenyewe ndio huu👇👇👇



Chadema watasubiri sanaaaaa. Hakuna mwananchi anataka hizi mambo
 
Yaani mimi kudai katiba mpya ambayo itamzuia Samia kutamba waziwazi mbele ya Watanzania bila aibu wala haya usoni kuwa hata kama CCM itashindwa uchaguzi itaunda serikali kwa kuiba kura ni chokochoko na kuvunja amani?Huyu Mama amechanganyikiwa?!
View attachment 1845111
Kuna movie inaitwa Lord of the ring. Hiyo ring ni kama kiti cha urais cha Tanzania.
Wale waadilifu walikuwa hawakutaka kabisa kuivaa hiyo pete kwani ilikuwa ina uwezo wa kumbadirisha mwema na akawa muovu.

Taratibu namwona mama anaelekea njia ya upotevuni. Njia ya waovu.
Mama ajue UOVU HAUSHINDI.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Taifa la watu mil 60 mnatikiswa na Mdude Nyagali

Rais is playing to our fears.

Siasa na chokochoko ziko toka 1929 ilipoanzishwa TAA, mbona tuko vizuri ?

Acheni kutisha watu!

Tunataka Katiba mpya!
Hajakataa kutuletea hiyo katiba mpya alichosema tumpe muda

Twende nae taratibu vinginevo tukimzingua hashindwi kuzingua

Mtu ana miezi minne toka aanze uongozi, ana mambo mengi ya kuweka sawa kwanza

Kuna lipi gumu tunaloshindwa kumuelewa hapo? Isitoshe majadiliano zaidi kuliko mabavu

Tusimlazimishe awe dikteta kisha mwisho wa siku afanye anavojiskia kama mwenda zake na hatuna la kufanya zaidi ya kulalamika tu

Hivo tuache kumtoa mama kwenye reli kwa kelele za vurugu vinginevo tuombe hiyo katiba mpya kwa namna ya kidiplomasia kama tuna haraka nayo zaidi
 
Kudai katiba mpya ni kutaka kuharibu amani ya nchi? Ni hivi, hiyo mama urais wake ni wa urithi, hivyo sitegemei aamue lolote tofauti na genge la yule kiongozi muovu kwani ndio linalomzunguka. Hivyo wanaodai katiba mpya wasiaachie, washikilie hapo hapo maana ni madai halali.
Wanasema ukila na kipofu usimshike mkono sasa nyie mnataka kukimbia na sahani ya msosi kabisa
 
*IPO HAJA YA KUDHIBITI SUALA HILI KWA NGUVU ZOTE,WANAPIMA KINA CHA MAJI HAWA WAPUUZI KI MAKUSUDI *
Nadhani ipo haja ya SSH kua dopt baadhi strategy chache za mwenda zake,
•vikao vya ndani vya kichama iwe ruksa.
•wabunge kufanyavsiasa majimboni mwao iwe ruksa.
•kujadili mambo ndani ya kumbi ruksa.
:::VYOMBO VYA USALAMA VIAGIZWE HIVYO.
:::TUKIWACHEA NYANI TUTAVUNA MABUA.
 
Hakuna mwenye tatizo na msimamo wake, na sisi msimamo wetu tutaendelea kuidai kila siku, maana katiba sio yake bali ni ya wananchi. Hatutakaa kimya mpaka siku yeye na chama Chake watake.
Kwahiyo tunaonyeshana makali???

Dr. Shika alale pema. Hahaahahahaha
 
Mama hoja za akina Mbowe zimemshinda aisee

Mama hoja ya Katiba Mpya ishamuwehusha

Mama akae na team yake wenye akili timamu wasolve hii issue ya Katiba,otherwise ataanza kuongea vituko sasa hivi

Amuulize Kikwete,Katiba Mpya mziki hata yeye ulimshinda kukwepa

Utakwepa kwa hoja gani?Hakuna

Hoja eti ya hovyo kama eti nataka nifanye maendeleo kwanza ni laini kama mlenda na ilishindwa siku ile ile

Mama aache kupaniki,asolve hili tatizo kama expert,wape Katiba Mpya wananchi,no way out of this!
Kama halipo kwenye ilani ya chama sahau
 
Hii issue kwa jinsi alivyoanza nayo tayari inaonekana hataweza.

Ni bora akutane na Wapinzani awape time line ya jinsi gani atatoa katiba mpya. Wote tunajua anavuta muda kwa ajili ya second term.
Imekula kwenu nyambaf nyie.

Tulishawaambia humu na tunaendelea kuwaambia, rais hana muda mchafu. Ana majukumu ya kuyatekeleza. Akutane na wapinzani ili iweje?
 
Mh.Rais yuko SAHIHI....

MBOWE ana majumba ARABUNI....
MBOWE ana makazi LONDON.....
MBOWE ana makazi MAREKANI....

Haya mwenzangu mimi KINGALU litakapotokea sijui utajificha milima ya uluguru?!!!!

#KaziIendelee
Kingalu😀😀😀😀😀
 
"MAZINGIRA" ya utawala wa mh.SSH umeshajiisha KESI ZA WATU ZIENDESHWE haraka na kutolewa uamuzi....

Leo UAMSHO wako nje wanajipigia UROJO ,SHOKISHOKI na AL KASUS kule Stone Town na Chokocho....
Leo MDUDE NYAGALI anakula maparachichi uraiani.....
Leo MH.MBOWE yuko uraiani pamoja na kurudishiwa zile milioni 300......
Leo HARBINDER SINGH SETH anakula biriani baada ya PLEA BARGAIN......
Leo baadhi ya "viongozi" wenye makandokando wako katika mikono ya sheria.....
Leo TRA imeacha zile "TASK FORCE" za makusanyo ya nguvu ya KODI.....
Leo tunapambana na janga la CORONA kivitendo kwa kukiri kuwa IPO NA TUENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI ....
Leo ametufutia ile tozo ya RETENTION ya 6% pale HESLB....
Leo wameajiriwa vijana wenzetu 8000 baada ya kukosekana ajira kwa takribani miaka 6......
Hawa wehu hawayaoni haya
 
Mama Samia ni vizuri akaamua uoande wa kusimama. Anataka kusimama upandewake au upande wa mtekaji na muuaji. Asiwe "si moto si baridi".

Kama anasimama upande wa haki, aukane utawala dhalimu uliopita.

Kama anasimama na utawala dhalimu wa awamu ya tano, anene wazi, ili watu wapambane naye rasmi.

Marehemu alitumia kauli kali na za vitisho, watu hawakuogopa.

Aliteka, aliwapoteza, aliua, watu hawakuogopa.

Alishambulia watu kwa risasi, hawakuogopa.

Mwishowe aliishia kudharaulika, na kulaaniwa na Dunia.

Sishani kama Samia atafanya kitu kipya akiamua kufuata nadharia ya mtangulizi wake.
Mama hafundishwi na mtu kama wewe
 
Back
Top Bottom