Uchumi gani ulioimarika wakati wa jiwe la mwashi? Mfumuko wa bei za bidhaa na bei kubwa za bidhaa za petrol sio suala la Mwigulu au Samia. Ni global regeneration economic phenomenon ambayo hutokea kila baada ya miaka kadhaa kunakosababishwa na kuyumba iwa global supply chains. Ilitokea hivyo miaka ya 1930s, ilitokea hivyo miaka ya 1970s, so siajabu kutokea sasa.
In the event like these, monetary policy inaishiwa uwezo wake na fiscal policy inakuwa weak ku-respond na pasipo umakini nchi inaingia kwenye total failure. Kwanini? Kwasababu hakuna ajuaye lini sababu za kupanga bei vitu zitakuwa zimekoma, na fiscal policy katika hili kazi yake kubwa ni kupungua/kukata kodi na kupunguza matumizi yake. Shida ni kwamba, so far hakuna matumizi ya kupunguza maana matumizi yote ni kama ya msingi tu (mishahara, miradi ya afya iliyoongezeka, miradi ya elimu bure, miradi ya ujenzi ambayo ni muhimu kwa uchumi). Je ikipunguza kodi then vipi italipia matumizi hayo ya msingi. Tumeshuhudia maeeo mengi kilio cha maisha magumu na hali ya kupanda kwa bidhaa. Watu wataishia kuandamana na kuondoa viongozi wa kisiasa lakini kinachoendelea kinahitaji high level of "fiscal balance" ili kipindi kipite salama.
Kwa sisi wachumi, so far Samia and Mwigulu are doing great job, hususan kwa kuongeza bajeti kwenye sekta zenye watu wengi (Kilimo) na sekta ya maji na umeme ili kufanya watu wajikite zaidi kwenye uzalishaji ikiwemo short to mid. Acheni blablah, uchumi si jambo jepesi.