Tuzidi kumuombea kwa Mola wetu, amzidishie hekima, busara na maarifa katika kufanya maamuzi yenye kuzingatia haki katika kipindi chote aiongozapo taasisi nyeti ya urais. Maamuzi hayo yajikite katika maslahi ya Tanzania kwanza, kisha ndipo yaje ya chama chake.
Abadilishe salamu yake aliyoiasisi ya kulitanguliza sifa ya jina la JMT, jamhuri ambayo yeye ndiye anayeiongoza. Badala ajishushe chini kwa utii na heshima, katika salamu yake atangulize sifa ya jina la Mola wake ambaye ndiye pekee anayemuongoza.
Sent from my Nokia 2.3 using
JamiiForums mobile app