Rais Samia: Muda wa siasa za uhasama umekwisha

Na utakoselewa kweli kwa sababu watu wako wakuu wa mikoa wilaya wabunge mawaziri madiwani walio wengi ni mizigo

Mpaka sisi watu wachini tunaona kuwa hapa hela ipigwa lakini mkuu wa wilaya wala mbunge haoni hilo mfano hizi barabala zinazo kwanguliwa kipindi chote kila mwaka hazina mtalo mvua ikinyesha inazoa udongo wote mwakani wanakwangua huo kama sio wizi nini subili mikutano ianze uone ukweli ulivio
 
Siasa za uhasama, wa kweli na wa kutunga, ni ajira kwa baadhi ya watu. Kama zitaondoka kuna wengi watakosa ajira.
Kipo kitengo rasmi kazi yake ni kuwatengenezea kashfa wanaowaona sio wenzao !! Wataacha ?! Tusubiri tuone !!
 
1. Ashukuriwe Bwana Mungu aliyekuchagua (raisi Samia) ili kuponya taifa. 2. Ashukuriwe bwana Mbowe, kwa busara kubwa ya kutaka maridhiano (pamoja na wafuasi wako kutokuelewa mwanzoni). 3. Abarikiwe raisi SAMIA kwa hekima kubwa ya kuongoza wa-tz. Sasa wasiojulikana hatuwasikii tena. Ni heri kutumia hekima na kufanikiwa. Kutoka moyoni nakupongeza sana.
 
Katika hili namuunga mkono. Ila tu asisahau pia kuwakemea baadhi ya polisi wanaotumiwa na wakuu wa Mikoa/Wilaya, kuwanyanyasa wapinzani.

Maana jukumu lao kubwa ni kulinda usalama wa raia, na siyo kutumika kama mbwa wa wanasiasa wasio fahamu maana halisi ya demokrasia.
 
Kumbe wewe, unakubali miongoni mwenu mlikua mashabiki wa siasa uchwara, huku mkihubiri upendo na mshikamano but huku mumeficha bunduki kwenye makoti, siasa zile zilikua si za kisomi bali za kinyama kabsaa. Huyu Rais kama anayohubiri hayatatekwa na kundi maslahi basi huyu ndy ataunganisha Taifa liliovunjwa vunjwa na mtu fulani. Mungu ibariki Tanzania!!
 
Tunakaa na ndugu nyumba moja wengine Simba wengine Yanga miaka nenda rudi baada ya mpira tunakaa meza moja tunalenga mawe sinia la ubwabwa
Simba na Yanga ule sio uhasama bali ni Utani tu lakini kwenye siasa ni Uhasama mbaya sana watu wapo tayari kukutoa roho wakikuona wewe ni tishio kwa Chama chao tena kwa sababu ya kukosoa tu !!
 
Tatizo lake la msingi bado moja tu mama yetu. Anatufundisha jinsi ya kumkosoa kwa kujificha kwenye kichaka cha utamaduni sijui mila. Yeye asisitize watu kufuata sheria tu sio maoni yake. Ila vijana hawa wa UVCCM waliokua wanaona kutukana ndio njia ya kupata vyeo sijui kama wanamwelewa. UVCCM ya kweli ilikufa kipindi cha Mkapa.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…