Rais Samia: Muda wa siasa za uhasama umekwisha

Kwani yeye anafikiri kutakua na kukosoa?🤣 Zaidi itakua uzushi na uongo. Kama anataka wanaccm wamstahimili mwanasiasa mzandiki kama lissu, basi haitakii wema ccm na watanganyika.
 
Ni Jambo jema Sana lakini sidhani kama wateuliwa wameelewa!
MH.Rais aliwahi kuelekeza viongozi waache kufanyakazi kwenye media naona BAADHI ya wakuu wa mikoa na wilaya bado hawajaelewa ina kera Sana kiongozi anafokea watu Kwa Jambo ambalo hajalifanyia utafiti mfano aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga enzi zile,Mkuu wa Mkoa Morogoro wa sasa na Mkuu wa Mkoa wa Mara aliyepita na wa sasa.

Kukemea watumishi au taasisi isiyofanya vizuri ni Jambo jema Sana lakini uwe na utafiti wa kutosha badala ya kutoa tuhuma nzito Kwa watumishi na mwisho wa siku inabainika ni uongo lakini Pia njia za kiutumishi zifuatwe.

MH.Rais anaporuhusu kukosoana ni vizuri wakajifunza staha ya kukosoa na ujengaji wa hoja na kama Kuna ushahidi kuhusu utendaji KAZI SHERIA zipo wazi. Kama wewe hupendi kuzalilishwa inakuwaje wewe uwe mstari wa mbele kudhalilisha wenzako? Kwani hakuna Ofisi?

Kupitia Television moja nimemsikia Mkuu mmoja akiwatupia lawama viongozi mbalimbali hata kama ni Ngazi za Chini Sana lakini alitakiwa awe na source za uhakika badala ya kuchukua Maneno ya uongo KUTOKA Kwa wamiliki wa NGO wanaotumia miradi kuwaiwaibia wafadhili.
Mfano Kuna taarifa kwamba watoto zaidi ya Mia mbili walitolewa kwenye nyumba salama alafu ndani ya siku tano wakakeketwa sabini Kwanza hizo data zimejaa upotoshaji lakini kama ni kweli hizo sababu za kuwaachia hao watoto mpaka wakafanyiwa ukatili zimejificha kwenye ubadhilifu mkubwa ili chenji ibakie ya kutosha.

Hivi Mwenyekiti wa mtaa au kijiji Leo unataka akomae na kesi ambazo sheria ina matundu lukuki alafu mwisho wa siku unamtaka apate wapigakura katika msimu ujao wa uchaguzi!?

BAADHI ya viongozi wanaona ni rahisi Sana kuwatupia lawama wanaosimamia sheria bila hata Kufuatilia CHANGAMOTO na kuzitafutia ufumbuzi Jamii nyingi Nchini ZIWE ni ZILE za wakulima au wafugaji na wale wanaotii Mila na desturi zao wanahitaji Elimu ili kuondokana naila potofu au Imani potofu na siyo ZOEZI la muda mfupi wala siyo ZOEZI la tahasisi moja.

Muda ufike Polisi wasitumike kusaidia upande mmoja ufanikiwe KISIASA ni Muhimu waachwe wafanyekazi Kwa weledi bila KUINGILIWA zile kauli za mkamate muweke ndani ziendane na matakwa ya SHERIA yanayo wataka Polisi Kuchunguza Kwanza na baadaye kukamata.
 
Akiathirika Mtanzania mwenzagu na mimi nimeathirika vile vile hata kisaikolojia,Swali .Tunaposema Wakoloni walitutesa je wewe uliathirika nini na je ulikuwepo wakati huo?
 

Weee bwana Lucas Maushamba ! Teuzi haziji kwa sanaa hiyo bana !!!
 
Hebu kuwa constructive based on reality! Wewe sio ulikua unamwandikia mama asifanye makosa kukaa pamoja na opposition especially chadema?
 
Asante Mama 🙏 umekomaa kisiasa sasa
 
Atwambie muda upi ulikuwa wa siasa uhasama
Awamu ya tano, read between the lines. Inamaana mambo yabadilike kutoka kwa yale aliyoyapokea kutoka kwa mtangulizi wake wa kiti cha uraisi.
 
Wewe nawe una akili kweli. na Ujinga wako.. Kwani tuko Shuleni hapa.!

Kama jibu lako tu la ajabu ajabu tu.
Liko wazi wazi tu. Nilitegemea.
 
Wewe nawe una akili kweli. na Ujinga wako.. Kwani tuko Shuleni hapa.!

Kama jibu lako tu la ajabu ajabu tu.
Liko wazi wazi tu. Nilitegemea.
Kuna ushahidi wa Maneno,Mkichague Mbunge MPINZANI sileti maendeleo jimboni kwenu,Mkurugenzi gari nikupe mimi,mshahara nikulipe mimi halafu mpinzani ashinde utanitambua,Wapinzani walichelewesha maendeleo.Ushahidi wa Matukio muda wote wa utawala wake MAFISADI aliokuwa anawaongelea ni wapinzani hasa hasa CHADEMA na karibia wale wote wenye ushawishi waliishia kusweka jela na kupigwa ,Tukio la Tundu Lisu Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halijawahi tokea Tanzania tangu nchi ipate uhuru na hata kabla ya uhuru ila limetokea kwa shetani wa Chato.Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 haujawahi fanywa vile tangu nchi ipate uhuru na kabla ya uhuru.Sijawahi ona Uchaguzi Mkuu ukuisimamiwa na wanaccm,vifaru na wanajeshi kama uchaguzi wa 2020.

Kwa hiyo kama familia yako ni wajinga na wapumbavu endelevu ambao huzimishwa kwa maneno ya viyisho mimi siyo saizi hiyo niliyoyaona maovu ya Magufuri na wewe umeyaona sema tu ulikuwa upande wake.Akija mwingine kutoka Kanda nyingine na akaamuwa kuwatendea ubaya watu wa kanda yenu na kabila lenu hata asipokufunga wewe lakini macho yako na masikio yakiwa yanashuhudia hutafurahia hata siku moja.Tunapomsema Magufuri kwa ubaya siyo kwa sababu tunamchukia mbona zamani alikuwa Waziri wa kuigwa kila wizara aliyoisimamia ilifanya vizuri.Sisi tunachukia matendo aliyoyaleta Tanzania ambayo hayakuwahi kutokea hata kipindi cha mkoloni.

Siku hizi Kesi za UCHOCHEZI unazisikia???Na kama huzisikii zimeenda wapi wakati polisi ni wale wale waliokuwa wanatekeleza amri yake?Zamani ilikuwa ni rahisi kwa Mkubwa au mwenye mamlaka kudanganya wadogo.Hata sisi mama zetu wakijifungua tulikuwa tunaambiwa na wazazi kuwa Mtoto amenunuliwa sokoni na tukaamini kama vile wewe Magufuri alivyokuaminisha kuwa ADUI wa maendeleo Tanzania nia CHADEMA au Vyama vyama vya upinzani,Mafisadi,Wavivu,Wezi,Vibaraka wa Mabebru,Mashoga,Omba omba wanapatikana Upinzani.

Kua basi huu ni mwaka 2023 badilika leo CCM imebaki pekee yake ushuhudie jinsi Maendeleo yatakavyopaa na yakipaa kwa kasi yenu tutawakubali maana Wapinzani walichelewesha Maendeleo.Mkishindwa tutawasema kama tunavyomsema Magufuri baada ya kuleta siasa za Machafuko nchini Tanzania enzi za utawala wake.Tanzania ni yetu na hatuna mahali pa kwenda zaidi ya Tanzania,Ndoto ya mtu mmoja isitufanye kuwa sisi hatufai kuishi Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…