Rais Samia na kamati, Kuna shida ipo mahali

Rais Samia na kamati, Kuna shida ipo mahali

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Rais Samia ni kama bado yupo kwenye umakamu wa raisi.

Kuna vitu wala havihitaji kamati ila yeye anaunda kamati. Hadi sasa sijaona umuhimu wa kamati kuhusu tozo. Tozo mmeziweka wenyewe bila kushirikisha wananchi, halafu nyie tena haohao mnaunda kamati kuhusu hizo tozo.

Hapa Rais Samia unajichanganya sana, kwa nini hizo kamati usingeziweka kabla ya kuja hizo tozo? Mama Samia ukweli ni kuwa hii kazi ya uraisi inaenda kukupa wakati mgumu sana.

Kamati kamati kamati halafu kamati hizohizo zinaleta majibu ambayo wewe tayari ulikuwa ukiyataka, umuhimu wa kamati upo wapi?
Mama Samia ushasema tozo zipo palepale, Sasa Kama zipo palepale hiyo kamati unategemea itakupinga?

Watu walimshambulia mwigulu kuwa yeye ndio kaleta tozo Ila leo nadhani jibu wamelipata. Mama Samia unasema tozo ni kwa ajili ya kujenga barabara vijijini, kwani mbona watangulizi wako walijenga barabara nchi nzima bila hizo tozo? Uzuri watangulizi wako wengine wapo nenda kawaulize walipata wapi pesa za kujenga barabara na hospitali.

Hadi hapa umuhimu wa katiba mpya unaonekana wazi tu.

Ni muda ipo siku isiyo na jina mtatoka madarakani
 
Nafikiri bado yupo "repudiated" kama ndiye kiongozi wa mwisho mwenye kuhitaji kufanya maamuzi mengine kwa kujiamini. Jambo hili linamfanya kutegemea zaidi maamuzi ya kamati ama watu wengine ili kukwepa lawama.
 
Nafikiri bado yupo "repudiated" kama ndiye kiongozi wa mwisho mwenye kuhitaji kufanya maamuzi mengine kwa kujiamini. Jambo hili linamfanya kutegemea zaidi maamuzi ya kamati ama watu wengine ili kukwepa lawama.
Huyu amalize miaka yake iliyobaki aende
 
Watangulizi wake hawakujenga BARABARA nchi nzima. SI KWELI.

Ukweli ni huu.

Karibia mikoa yote imekaribia kuunganishwa na BARABARA ZA LAMI.

Anachoongelea mh.Rais SSH ni zile barabara za ndani ya wilaya kuelekea tarafani....katani....VIJIJINI....MASHAMBANI.

#KaziIendelee
#NchiKwanza
#SiempreCCM
 
Ni kwamba ile namna ya ukusanyaji wa Mapato serikalini, ya JPM imekua ni namna ngumu sana kwao (Samia and her mentors) na ikiwezekana wameshindwa kabisa kwa sababu nyingi ikiwemo kuachia ile mirija ya unyonyaji na ufujaji pesa za serikali.

Hivyo wanakuja na namna zao za ukusanyaji mapato ndio hizoo za Tozo umiza.
 
Ukitaka usimuumiza MTANZANIA kwa ATOACHO mwambie hili:

MCHANGO WA HARUSI utakaokuwa na POMBE ZA KUMWAGA NA NYAMA CHOMA MPAKA MENO YANG'OKE.

Hakika TOZO hii haijapokelewa vyema, la muhimu SERIKALI YETU SIKIVU. SERIKALI YETU SIKIVU itapokea maoni ya KAMATI HIYO na kuipunguza TOZO na kuwa NYEPESI.

MAENDELEO HAYAPATIKANI KWA KUPITIA NJIA NYEPESI NA RAHISI

MAENDELEO NI JASHO NA DAMU

#TulijengeTaifaLetuKwaUchunguMkubwa
#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Hizo barabara za lami za kuunganisha mikoa walipata
Si kazi rahisi kuiunganisha mikoa yote.

Ndio maana kwa miaka 60 haijamalizika hiyo kazi.

Awamu ya 6 imekuja na mkakati wa KUMUINUA MKULIMA....kwa kumtengenezea barabara mpaka MASHAMBANI huko ili APUNGUKIWE GHARAMA ZA USAFIRI...MUDA WA KUSAFIRISHA MAZAO YAKE.

Hapa kuna tija kubwa ITAKAYOPATIKANA.

Leo tunaona UZITO ila huko mbeleni tutakuja kuuona WEPESI NA MAFANIKIO ADHIMU
 
Mama Samia ni kama bado yupo kwenye umakamu wa raisi.
Kuna vitu Wala havihitaji kamati ila yeye anaunda kamati. Hadi sasa sijaona umuhimu wa kamati kuhusu tozo.
Tozo mmeziweka wenyewe bila kushirikisha wananchi, alafu nyie tena haohao mnaunda kamati kuhusu hizo tozo.
Hapa mama Samia unajichanganya sana, kwa nini hizo kamati usingeziweka kabla ya kuja hizo tozo?
Mama Samia ukweli ni kuwa hii kazi ya uraisi inaenda kukupa wakati mgumu sana.
Kamati kamati kamati alafu kamati hizohizo zinaleta majibu ambayo wewe tayari ulikuwa ukiyataka, umuhimu wa kamati upo wapi?
Mama Samia ushasema tozo zipo palepale, Sasa Kama zipo palepale hiyo kamati unategemea itakupinga?
Watu walimshambulia mwigulu kuwa yeye ndio kaleta tozo Ila leo nadhani jibu wamelipata.
Mama Samia unasema tozo ni kwa ajili ya kujenga barabara vijijini, kwani mbona watangulizi wako walijenga barabara nchi nzima bila hizo tozo? Uzuri watangulizi wako wengine wapo nenda kawaulize walipata wapi pesa za kujenga barabara na hospitali.
Hadi hapa umuhimu wa katiba mpya unaonekana wazi tu.
Ni muda ipo siku isiyo na jina mtatoka madarakani
Mama Samia ukweli ni kuwa hii kazi ya uraisi inaenda kukupa wakati mgumu sana.
Kamati kamati kamati alafu kamati hizohizo zinaleta majibu ambayo wewe tayari ulikuwa ukiyataka, umuhimu wa kamati upo wapi?
Mama Samia ushasema tozo zipo palepale, Sasa Kama zipo palepale hiyo kamati unategemea itakupinga?[emoji1534][emoji1548][emoji736][emoji817][emoji1534][emoji1548][emoji736][emoji817]
 
Mi huwa siwaamini wanawake kwenye baadhi ya nyadhifa za kitaifa hasa cheo kikubwa kama Urais? There must be some corrupt politicians driving this failed woman president just for their own selfish interests, Rip JPM,
 
Back
Top Bottom