Mkwawe
JF-Expert Member
- Jun 10, 2016
- 3,132
- 5,508
Una miaka 60+ kwa sasa una nguvu kiasi na una uwezo wa kufanya mambo kadhaa ila baada ya miaka 17 hautakuwa Samia huyu wa Sasa.
Pengine Kuna mambo unayafanya kwa ajili ya kizazi chako ila niamini mimi Mkwawe pindi utakapopoteza madaraka, ushawishi na nguvu hakuna chawa yeyote atayekupambania. Hakuna chawa yeyote atamkumbuka Abdul au yeyote katika uzao wako.
Magufuli alikuwa na machawa pia, Mimi nilikuwa mpenzi mkubwa wa baadhi ya sera za magufuli ila wapo ambao walikuwa ni machawa kindakindaki ambao leo wamemsahau tayari Magufuli na wameusahau uzao wake baada ya yeye kupotea.
Rais wangu Samia ninakichukia chama chako cha CCM kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu lakini ninapenda yeyote aliye katika haki hata kama ni wa CCM. hata kama ninaichukia CCM ukweli ulio wazi ni kwamba CCM ndiyo wanaoshika mustakabali wa maisha ya Tanzania ya sasa na ijayo hivyo wewe ukiwa kama rais na mwenyekiti wa chama tawala jaribu kuwa na dira ndogo tu, jambo lolote unalolifanya hovyo hovyo wakati huu litatuathiri watanganyika kwa sasa lakini hata wazanzibari hawataachwa salama nyakati zijazo, hata akina Abdul watakulaumu, watatelekezwa na chawa wako, watoto wako watakuwa na maisha magumu. Kipindi ambacho utakuwa umepoteza nguvu au pengine umekufa kizazi chako kitateseka sana hapa duniani. Haijalishi ni kiwango gani cha fedha utachowatafutia kwa sasa ila hawatoachwa salama
Rais wetu hata kama unatuchukia watanzania wa Tanganyika ila Kuna vitu tunaomba utuachie tu kama vilivyo. Najua kuna kauli nyingi za utata unazozitoa kwenye hotuba zako ziletazo migongani ya kihisia kwetu watanganyika kauli zinazohusu rasilimali na ulinzi na usalama na ulipaji Kodi kandamizi na utawala usio bora najua unajua usemacho ila siku zote ubaya ni sawa na kuunoa mkuki utakaokudunga mwenyewe
Kwa ajili ya miaka yako michache hapa duniani tunaomba usiingie mikataba mibovu na mirefu
Kwa ajili ya maisha ya baadaye ya kizazi chako wapatanishe wanao na watanganyika, machawa watakulekezea tu hao watoto wakabidhi wanao wawe na mahusiano mema na watanzania kwa ujumla
Ukiusoma ujumbe huu ujue ni kuwa watanzania tunapenda sana amani ila wanasiasa wanataka kuibomoa amani iliyo
UZALENDO HUANZA NA KIONGOZI