Rais Samia najua hautupendi watanganyika ila angalau tufanyie hili

Rais Samia najua hautupendi watanganyika ila angalau tufanyie hili

Ni w
Kuna siku nilipanda gari ya Shabiby kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam. Ikawekwa wimbo flani wa Konde boy kama sijakosei ilikuwa inamwimba na kumsifia Rais Samia. Kuna mama mmoja nilikaa nae kwenye kiti nilimwita yule Konda na kumwambia samahani sana naomba utowe hiyo wimbo unaniuwa kwa pressure.
Baadae nikamuuliza shida nini hadi ukisikia wimbo inayomhusu Rais Samia unaumia kiasi hicho? Akaniambia nikikusimulia pressure yangu itapanda naomba tuyaache ila nilikuja kugundua kuwa yule mama ni mkurugenzi kwenye taasisi nyeti sana hapa Tanzania kwasababu ya simu alizokuwa anapokea na kupiga pia.
Ni wengi mno hawampendi ,ila tunacho ambiwa na kuona na kusikia hailingani.
 
Una miaka 60+ kwa sasa una nguvu kiasi na una uwezo wa kufanya mambo kadhaa ila baada ya miaka 17 hautakuwa Samia huyu wa Sasa.

Pengine Kuna mambo unayafanya kwa ajili ya kizazi chako ila niamini mimi Mkwawe pindi utakapopoteza madaraka, ushawishi na nguvu hakuna chawa yeyote atayekupambania. Hakuna chawa yeyote atamkumbuka Abdul au yeyote katika uzao wako.

Magufuli alikuwa na machawa pia, Mimi nilikuwa mpenzi mkubwa wa baadhi ya sera za magufuli ila wapo ambao walikuwa ni machawa kindakindaki ambao leo wamemsahau tayari Magufuli na wameusahau uzao wake baada ya yeye kupotea.

Rais wangu Samia ninakichukia chama chako cha CCM kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu lakini ninapenda yeyote aliye katika haki hata kama ni wa CCM. hata kama ninaichukia CCM ukweli ulio wazi ni kwamba CCM ndiyo wanaoshika mustakabali wa maisha ya Tanzania ya sasa na ijayo hivyo wewe ukiwa kama rais na mwenyekiti wa chama tawala jaribu kuwa na dira ndogo tu, jambo lolote unalolifanya hovyo hovyo wakati huu litatuathiri watanganyika kwa sasa lakini hata wazanzibari hawataachwa salama nyakati zijazo, hata akina Abdul watakulaumu, watatelekezwa na chawa wako, watoto wako watakuwa na maisha magumu. Kipindi ambacho utakuwa umepoteza nguvu au pengine umekufa kizazi chako kitateseka sana hapa duniani. Haijalishi ni kiwango gani cha fedha utachowatafutia kwa sasa ila hawatoachwa salama

Rais wetu hata kama unatuchukia watanzania wa Tanganyika ila Kuna vitu tunaomba utuachie tu kama vilivyo. Najua kuna kauli nyingi za utata unazozitoa kwenye hotuba zako ziletazo migongani ya kihisia kwetu watanganyika kauli zinazohusu rasilimali na ulinzi na usalama na ulipaji Kodi kandamizi na utawala usio bora najua unajua usemacho ila siku zote ubaya ni sawa na kuunoa mkuki utakaokudunga mwenyewe

Kwa ajili ya miaka yako michache hapa duniani tunaomba usiingie mikataba mibovu na mirefu
Kwa ajili ya maisha ya baadaye ya kizazi chako wapatanishe wanao na watanganyika, machawa watakulekezea tu hao watoto wakabidhi wanao wawe na mahusiano mema na watanzania kwa ujumla

Ukiusoma ujumbe huu ujue ni kuwa watanzania tunapenda sana amani ila wanasiasa wanataka kuibomoa amani iliyo

UZALENDO HUANZA NA KIONGOZI
Rais Sane kuongoza Tanzania alikuwa Benjamin Mkapa, waliomfuatia ni wapiga deal watupu. JPM kidogoo alijitahidi kujitofauisha na majizi menzake ila naye ndio humo humo tu
 
Katiba inazungumzia kubadilishana Urais pekee, ni mangapi yalikuwepo kwenye Katiba mfano mgombe huru yakavunjwa watu waliposhitaki mahakama ikabadilisha proactively ?

Nimesema katiba ni sheria na nchi / watu wenye utamaduni wa kutofuata sheria huo utakuwa ni muendelezo wa kuongeza mambo ya kuvunjwa nadhani umenielewa Katiba haifanyi automatically watu kufuata sheria bali inabidi watu tuwe na utamaduni wa kufuata na kutii sheria bila shuruti (hata hizi zilizopo sasa)
Mimi sikukuzwa na kulelewa kulalamika

I am problem solver

Kuandika katiba mpya Hl ndo the best soln ya matatizo yetu,

We utaumia nini tukiandika katiba
Tupe soln basi

over 75% problems za nchi hii ni katiba labda 25% ndo mambo mengine kama unayosema
 
Mimi sikukuzwa na kulelewa kulalamika
Anayelalamika ni nani mimi kuelezea shida iliyopo ni kulalamika au kusema hakuna shida wakati shida ipo ndio sio kulalamika
I am problem solver
Aisee kama hata unashindwa kuelewa tatizo au kusoma nilichoandika hizo problem utazosema unasolve si utasolve kitu ambacho hakipo ? Nimekwambia tatizo kubwa la jamii zetu hususan sasa ni kutokutii sheria hata ambazo zipo wazi zinavunjwa wala hazikemewi na watu wanaona sifa vitu kama rushwa tunajua kabisa ni jambo baya ila watu wanafanya na jamii inaona ni sawa hivyo bila utamaduni wa kufuata sheria na watu kama jamii kukemea uvunjaji wa sheria utakuwa ni muendelezo wa kuvunja sheria yoyote ile hata hii sheria mama
Kuandika katiba mpya Hl ndo the best soln ya matatizo yetu,
Na kumbe wewe issue ni upya na sio uzuri wala bora..., na unadhani katika ndio mwarobaini wa matatizo yako (kweli tuna safari ndefu sana) Inabidi kila kitu kirekebishwe na kiwe bora hata Katiba iwe bora yenye kumlinda mwananchi na above all else ifuatwe na tuwe na tamaduni na taasisi imara za kuwawashibisha wote wavunja sheria ikiwemo Katiba
We utaumia nini tukiandika katiba
Tupe soln basi

over 75% problems za nchi hii ni katiba labda 25% ndo mambo mengine kama unayosema
Aisee nani kasema Katiba isiandikwe unasema asilimia 75% ya matatizo ni Katiba hata kama ungesema 99% alafu lile moja ni kutokufuata sheria / kuheshimu katiba sasa huoni hizo 99 hazitafanya kazi kama tuna utamaduni wa kujifanyia tunachojifanyia na wananchi kuona ni sawa ?
 
Kujenga miundo mbinu ya migodi huko kwenye hifadhi zenu Watanganyika huko. Kuripua miamba...na kujenga makazi ya wafanyakazi. Sijui kama mtakuwa na hifadhi tena. Wajukuu na vitukuu vyenu vitakuta mashimo tu na hadithi...na waliochimba na kufaidika na hayo madini walishasepa zao. Poor Tanganyika!

View attachment 3047996
Kaulitz ya ajabu sana
 
Una miaka 60+ kwa sasa una nguvu kiasi na una uwezo wa kufanya mambo kadhaa ila baada ya miaka 17 hautakuwa Samia huyu wa Sasa.

Pengine Kuna mambo unayafanya kwa ajili ya kizazi chako ila niamini mimi Mkwawe pindi utakapopoteza madaraka, ushawishi na nguvu hakuna chawa yeyote atayekupambania. Hakuna chawa yeyote atamkumbuka Abdul au yeyote katika uzao wako.

Magufuli alikuwa na machawa pia, Mimi nilikuwa mpenzi mkubwa wa baadhi ya sera za magufuli ila wapo ambao walikuwa ni machawa kindakindaki ambao leo wamemsahau tayari Magufuli na wameusahau uzao wake baada ya yeye kupotea.

Rais wangu Samia ninakichukia chama chako cha CCM kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu lakini ninapenda yeyote aliye katika haki hata kama ni wa CCM. hata kama ninaichukia CCM ukweli ulio wazi ni kwamba CCM ndiyo wanaoshika mustakabali wa maisha ya Tanzania ya sasa na ijayo hivyo wewe ukiwa kama rais na mwenyekiti wa chama tawala jaribu kuwa na dira ndogo tu, jambo lolote unalolifanya hovyo hovyo wakati huu litatuathiri watanganyika kwa sasa lakini hata wazanzibari hawataachwa salama nyakati zijazo, hata akina Abdul watakulaumu, watatelekezwa na chawa wako, watoto wako watakuwa na maisha magumu. Kipindi ambacho utakuwa umepoteza nguvu au pengine umekufa kizazi chako kitateseka sana hapa duniani. Haijalishi ni kiwango gani cha fedha utachowatafutia kwa sasa ila hawatoachwa salama

Rais wetu hata kama unatuchukia watanzania wa Tanganyika ila Kuna vitu tunaomba utuachie tu kama vilivyo. Najua kuna kauli nyingi za utata unazozitoa kwenye hotuba zako ziletazo migongani ya kihisia kwetu watanganyika kauli zinazohusu rasilimali na ulinzi na usalama na ulipaji Kodi kandamizi na utawala usio bora najua unajua usemacho ila siku zote ubaya ni sawa na kuunoa mkuki utakaokudunga mwenyewe

Kwa ajili ya miaka yako michache hapa duniani tunaomba usiingie mikataba mibovu na mirefu
Kwa ajili ya maisha ya baadaye ya kizazi chako wapatanishe wanao na watanganyika, machawa watakulekezea tu hao watoto wakabidhi wanao wawe na mahusiano mema na watanzania kwa ujumla

Ukiusoma ujumbe huu ujue ni kuwa watanzania tunapenda sana amani ila wanasiasa wanataka kuibomoa amani iliyo

UZALENDO HUANZA NA KIONGOZI
Ujumbe mzuri sanaa
 
Back
Top Bottom