Rais Samia najua hautupendi watanganyika ila angalau tufanyie hili

Rais Samia najua hautupendi watanganyika ila angalau tufanyie hili

Mmmh!

Mkuu, kwanza hongera kwa mawazo mazuri tu

Mbali na mawazo haya mazuri, nimejikuta natoa machozi pale nilipobaini kwamba, kumbe sisi nchi yetu imejengwa katika mawazo ya mtu mmoja tu ambaye ni kiongozi mkuu wa nchi

Maana yake hakuna utaratibu uliowekwa kuidhibiti mamlaka hiyo, ambayo sasa ni hatari sana kwa afya ya Taifa letu

Ifike hatua sasa hii dhana itoweke tu, kila mamlaka iwe chini ya mamlaka inayosimamia sheria

Maana yake, Kitengo kinachotunga sheria na kile kinachosimamia sheria, kimlike haya kwa haraka mno

Kwa sababu haya mambo ndiyo yanayofanya Rais awe na machawa mengi kwa sababu machawa yanajua udhaifu wa viongozi hawa huku wao wakivutwa na nguvu waliyonayo ya kufanya chochote kile kitakachokuja mbele yao maana hawana zuwio lolote la shiria dhidi ya lolote watakachokiamua

Hii ikiachwa hivihivi, ndiyo tutakuwa tukiulizana humu kila leo eti awamu fulani na fulani ipi bora? Kumbe wote ni bora ama siyo bora isipokuwa tunasheria mbovu dhidi ya mamlaka ya viongozi wetu

Mungu atusaidie mh Rais Samia akubali tu mchakato wa katiba auweke ili uanze
 
Kuna siku nilipanda gari ya Shabiby kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam. Ikawekwa wimbo flani wa Konde boy kama sijakosei ilikuwa inamwimba na kumsifia Rais Samia. Kuna mama mmoja nilikaa nae kwenye kiti nilimwita yule Konda na kumwambia samahani sana naomba utowe hiyo wimbo unaniuwa kwa pressure.
Baadae nikamuuliza shida nini hadi ukisikia wimbo inayomhusu Rais Samia unaumia kiasi hicho? Akaniambia nikikusimulia pressure yangu itapanda naomba tuyaache ila nilikuja kugundua kuwa yule mama ni mkurugenzi kwenye taasisi nyeti sana hapa Tanzania kwasababu ya simu alizokuwa anapokea na kupiga pia.
 
President Samia's behavior is an analogous reflection to that of Marie Antoinette, the Queen of France before 1793.

Her being of Germanic descent, dared to mock the poor French peasants demanding BREAD. Marie Antoinette scorned, "They demand bread, why don't they eat cake ?"

President Samia, is beyond redemption and undeterred. Her heart is hardened and intoxicated by power and lavish lifestyle.

What makes you think she'll bother to listen to your advice?

#WelcomeToArabMoney
 
Una miaka 60+ kwa sasa una nguvu kiasi na una uwezo wa kufanya mambo kadhaa ila baada ya miaka 17 hautakuwa Samia huyu wa Sasa.

Pengine Kuna mambo unayafanya kwa ajili ya kizazi chako ila niamini mimi Mkwawe pindi utakapopoteza madaraka, ushawishi na nguvu hakuna chawa yeyote atayekupambania. Hakuna chawa yeyote atamkumbuka Abdul au yeyote katika uzao wako.

Magufuli alikuwa na machawa pia, Mimi nilikuwa mpenzi mkubwa wa baadhi ya sera za magufuli ila wapo ambao walikuwa ni machawa kindakindaki ambao leo wamemsahau tayari Magufuli na wameusahau uzao wake baada ya yeye kupotea.

Rais wangu Samia ninakichukia chama chako cha CCM kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu lakini ninapenda yeyote aliye katika haki hata kama ni wa CCM. hata kama ninaichukia CCM ukweli ulio wazi ni kwamba CCM ndiyo wanaoshika mustakabali wa maisha ya Tanzania ya sasa na ijayo hivyo wewe ukiwa kama rais na mwenyekiti wa chama tawala jaribu kuwa na dira ndogo tu, jambo lolote unalolifanya hovyo hovyo wakati huu litatuathiri watanganyika kwa sasa lakini hata wazanzibari hawataachwa salama nyakati zijazo, hata akina Abdul watakulaumu, watatelekezwa na chawa wako, watoto wako watakuwa na maisha magumu. Kipindi ambacho utakuwa umepoteza nguvu au pengine umekufa kizazi chako kitateseka sana hapa duniani. Haijalishi ni kiwango gani cha fedha utachowatafutia kwa sasa ila hawatoachwa salama

Rais wetu hata kama unatuchukia watanzania wa Tanganyika ila Kuna vitu tunaomba utuachie tu kama vilivyo. Najua kuna kauli nyingi za utata unazozitoa kwenye hotuba zako ziletazo migongani ya kihisia kwetu watanganyika kauli zinazohusu rasilimali na ulinzi na usalama na ulipaji Kodi kandamizi na utawala usio bora najua unajua usemacho ila siku zote ubaya ni sawa na kuunoa mkuki utakaokudunga mwenyewe

Kwa ajili ya miaka yako michache hapa duniani tunaomba usiingie mikataba mibovu na mirefu
Kwa ajili ya maisha ya baadaye ya kizazi chako wapatanishe wanao na watanganyika, machawa watakulekezea tu hao watoto wakabidhi wanao wawe na mahusiano mema na watanzania kwa ujumla

Ukiusoma ujumbe huu ujue ni kuwa watanzania tunapenda sana amani ila wanasiasa wanataka kuibomoa amani iliyo

UZALENDO HUANZA NA KIONGOZI
Duuu, sijui kama ataelewa, CHURA KIZIWI 🐸🐸🐸🐸
 
President Samia's behavior is an analogous reflection to that of Marie Antoinette, the Queen of France before 1793.

Her being of Germanic descent, dared to mock the poor French peasants were demanding BREAD. Marie Antoinette scorned, "They demand bread, why don't they eat cake ?"

President Samia, is beyond redemption and undeterred. Her heart is hardened and intoxicated by power and lavish lifestyle.

What makes you think she'll bother to listen to your advice?

#WelcomeToArabMoney
Sio MJERUMANI, alizaliwa Vienna Austria.
Ni masahihisho madogo, all in all andiko liko poa 🙏🙏
 
Ni bida'a kwa mwanamke kuwa kiongozi ila cha ajabu hakuna kiongozi wa dini yeyote hususani aliyopo aliyewahi kukemea hili hadharani
Mkuu subiri watakavyojitokeza baada ya huyu kupita.
 
Mmmh!

Mkuu, kwanza hongera kwa mawazo mazuri tu

Mbali na mawazo haya mazuri, nimejikuta natoa machozi pale nilipobaini kwamba, kumbe sisi nchi yetu imejengwa katika mawazo ya mtu mmoja tu ambaye ni kiongozi mkuu wa nchi

Maana yake hakuna utaratibu uliowekwa kuidhibiti mamlaka hiyo, ambayo sasa ni hatari sana kwa afya ya Taifa letu

Ifike hatua sasa hii dhana itoweke tu, kila mamlaka iwe chini ya mamlaka inayosimamia sheria

Maana yake, Kitengo kinachotunga sheria na kile kinachosimamia sheria, kimlike haya kwa haraka mno

Kwa sababu haya mambo ndiyo yanayofanya Rais awe na machawa mengi kwa sababu machawa yanajua udhaifu wa viongozi hawa huku wao wakivutwa na nguvu waliyonayo ya kufanya chochote kile kitakachokuja mbele yao maana hawana zuwio lolote la shiria dhidi ya lolote watakachokiamua

Hii ikiachwa hivihivi, ndiyo tutakuwa tukiulizana humu kila leo eti awamu fulani na fulani ipi bora? Kumbe wote ni bora ama siyo bora isipokuwa tunasheria mbovu dhidi ya mamlaka ya viongozi wetu

Mungu atusaidie mh Rais Samia akubali tu mchakato wa katiba auweke ili uanze
Asante kiongozi
Wazo la katiba mpya ni jema lakini kamwe lisingekuwa hoja ya msingi kama hata kwa kutumia katiba iliyopo rais angeheshimu walau nusu ya kilichopo lakini ikiwa hii katiba mbovu na dhaifu inavunjwa unadhani kutakuwa na utayari wa kuitekeleza katiba mpya?
Ndo maana naamini shida ya kwanza kabisa sio katiba Bali kiongozi kutoheshimu katiba
 
Tutamsamehe? 😂
Kuna watu huwa hamna akili, hapo umebeba hadi maamuzi ya wengine. Kwa nn usiseme "nitamsamehe"?

Alafu hata usipomsamehe nini kitatokea?
Unadhani wote walio kwenye mfumo wanamuelewa Samia!
Ndo maana anasema pengine tutamsamehe
 
Nchi isiyoheshimu Sheria Katiba ni kama Jarida tu katika Maktaba au kanuni watu wanazojisemea katika maongezi yao....
Haswaaaa hata mimi ndicho ninachokisema
Katiba bila utawala bora na uzalendo wa kweli ni kabrasha tu
 
Nchi isiyoheshimu Sheria Katiba ni kama Jarida tu katika Maktaba au kanuni watu wanazojisemea katika maongezi yao....
Kwa sababu huyu huyu Rais alishawahi kusema katiba ni "kijitabu" tu
 
Umeongea vizuri Sana. Hakika kuna mikataba ameingia itatugharimu watanganyika. Niwe muwazi simpendi huyu mama kwa moyo wangu wote
Nasikia Abdul ndiye Ridhiwani mpya Sasa. Ukiona mambo Yako hayaendi, muone yeye TU.
 
Kuna siku nilipanda gari ya Shabiby kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam. Ikawekwa wimbo flani wa Konde boy kama sijakosei ilikuwa inamwimba na kumsifia Rais Samia. Kuna mama mmoja nilikaa nae kwenye kiti nilimwita yule Konda na kumwambia samahani sana naomba utowe hiyo wimbo unaniuwa kwa pressure.
Baadae nikamuuliza shida nini hadi ukisikia wimbo inayomhusu Rais Samia unaumia kiasi hicho? Akaniambia nikikusimulia pressure yangu itapanda naomba tuyaache ila nilikuja kugundua kuwa yule mama ni mkurugenzi kwenye taasisi nyeti sana hapa Tanzania kwasababu ya simu alizokuwa anapokea na kupiga pia.
Mkurugenzi.... Samia.... Kukerekwa...taasisi nyeti
Natamani kujua kitu mkuu
 
Kwa sababu huyu huyu Rais alishawahi kusema katiba ni "kijitabu" tu
Katiba ni makubaliano a social contract, Katiba ni Sheria lakini kama Sheria haifuatwi sio kakijitabu tu bali ni kitabu hata kisichosomwa ingawa tungekuwa tunafuata Sheria hata bila hicho kitabu tungekuwa tuna Katiba (social contract)
 
President Samia's behavior is an analogous reflection to that of Marie Antoinette, the Queen of France before 1793.

Her being of Germanic descent, dared to mock the poor French peasants were demanding BREAD. Marie Antoinette scorned, "They demand bread, why don't they eat cake ?"

President Samia, is beyond redemption and undeterred. Her heart is hardened and intoxicated by power and lavish lifestyle.

What makes you think she'll bother to listen to your advice?

#WelcomeToArabMoney
So what was Marie Antoinette's destiny!?

Will Arab money shield her?
 
Back
Top Bottom