labda uwezo pesa yenu ndo umefika hapo.. kiingine kumbuka mazingira ya Afrika na Europe.. unaweza ukaleta Train hapa full fiber na makolokolo kibao.... baada ta mwaka mtaikataa itakavyokuwa imechakaa kwa ustaarabu wetu wa kiafrika ... ndo maana hata kwenye magari kuna magari maalum kwa rough road .... Toyota Landcruiser V8 ni gharama na bora kuliko Land cruiser mkonga.. lakini bado porini Land cruiser mkonga ni durable kuliko V8... its all about mindset ya engineering design ametega kwenye soko lipi...
Angali mwendo kasi zilivyochoka haraka .. service magumashi magari yanawaka moto yenyewe...
Asante sana mkuu kwa mchango wako. Nikianza na mchango wako kwenye paragraph yako ya mwisho kuhusu Mabasi ya mwendo Kasi naweza tu kukuambia kwamba sijui ulikuwa ushauri wa nani na kwa madhimuni gani?
Concept ya huu mradi naiona haikuwa imetazamwa kwa kina zaidi toka mwanzo. Kuna mambo mengi ambayo yanaonyesha kuwa huu mradi toka kubuniwa kwake haukuwa na malengo ya kuleta matokeo chanya.
Sababu ya kwanza na kubwa ni kupigwa vita na matajiri wanao endesha biashara zao za usafiri kama; daladala, TAXI, Bajaji, Bodaboda na kadhalika. Hawa hawataufurahia huu mradi hata mara moja, kwani wanaona una wanyima riziki zao za kujipatia kipato kutokana na kukosekana kwa abiria ambao watakuwa wanatumia huduma hii nafuu, kama ilivyo hivibsasa jinsi SGR inavyopigwa vita na waendesha biashara ya malori na mabasi ya abiria yaendayo mikoani.
Sababu ya pili ninayo iona mimi ni concept ya miundo mbinu za barabara na vituo vya mabasi. Tatizo letu sisi watanzania na hasa wahusika wakuu wa kupanga, kuratibu na kuiendesha hiyo miradi, mara nyingi wanakosa visions na uelewa wa kufanya biashara.
Najua wengi watakuwa wamesomea namna ya kuendesha biashara ya vitega uchumi ambavyo pia ni vitoa huduma, hata hivyo wanakosa maarifa ya kujiongeza wenyewe.
Hapa namaanisha kukosa maarifa ya kuvifanya hivyo vitega uchumi vinavyo toa huduma kuviweka katika mazingira ya kuvutia ili wapate wateja wengi na confortability.
Tunajua kuwa Tanzania ni nchi ya joto, nani sasa alituzuia sisi tusivifanye hivyo vituo vya hayo mabasi na hayo mabasi yenyewe yakawa fully airconditioned? Hakuna. Ni ukosefu wa maarifa mapana tu ya waratibu na watendaji kufanya Business.
Katika kufanya hivi walitakiwa waelewe kuwa wanaleta ushindani wa kuendesha biashara kwa watoa huduma wingine, kwa kutoa huduma ambayo ni attraktiv na comfortable, kiasi kwamba watoa service wengine nao wakaongeza quality ya Services zao.
Hii ni chachu ya kuinua Standard ya maisha nchini kama tunavyoona hivi sasa watanzania wengi wanavyojitahidi kuwa na nyumba nzuri za mabati every where.
Sababu ya tatu ni vyombo vyenyewe. Kihistoria huko nyuma tulisha kuwa na usafiri wa aina hii. Tulishindwa kwa sababu ya kuto take care mabasi yetu. Yakiharibika ndiyo basi tena hakuna mtu alijihisi yeye kuwa respnsible na hilo. Waliyatekeleza mabasi na wahuni wakatoa vipuli vinavyo faa kwa ajili ya kujitafutia riziki zao.
Ushauri wangu katika hili tusinge endeleza tena usafiri huu wa mabasi badala yake tungeleta usafiri wa airconditioned trams na commuter trains na vituo vyake, ili ku make service attraktive and confortable kama ilivyo kwa wenzetu.
Trams na commuter trais zingesababisha karakana kubwa kufunguliwa na hivyo kupanua wigo wa kitechnolojia kwa vijana wetu na pia maarifa mapana ya ku-create jobs kwa vijana wetu.
Hivi ndivyo miji na watu wanavyo endelea na hivyo ku-create ajira. Dar es salaam ikianza itaenea hata huko mikoani. Aidha tunakosa watu wenye visions kama hizi au watu wenye visions hawasikilizwi na baadhi ya watandaji wenye upeo finyu wa maisha.