Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

johnthebaptist said:
Kama kuheshimu Vitabu tungeheshimu Vitabu Vitakatifu, mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?"

Kukiuka maagizo yalipo kwenye kitabu au vitabu vya dini kunazalisha neno DHAMBI, na mshahara wake ni ADHABU kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya dini...(hii ni kwa wale waamini)

Kwa lugha nyingine ni kwamba kwa kuwa ameona kuwa watu wanakiuka maagizo na shurti zilizopo kwenye vitabu vya dini, lakini mwisho wa dahari kuna hukumu inayongoja mwanadamu...

Mawazo yaliyopo kwenye vitabu vya dini hayakuandikwa kwa utashi wa kibinadamu hivyo hakuna nafasi ya kubadilisha chochote ili kukemea au kubadili mwenendo wa binadamu kuacha uovu kwa sasa...

Unlike katiba ya nchi, hiki ni kitabu cha muongozo wa kisheria kilichotungwa na wanadamu ili kujiongoza wenyewe juu ya ardhi au eneo husika liitwalo nchi...

Kwa kuwa maudhui yake yameundwa na binadamu, hivyo si DHAMBI endapo mwanadamu ambaye ni mtunzi akitaka kuboresha au kunyumbulisha maneno yaliyopo ndani ya kitabu hicho kwa wakati unaofaa...

Kauli ya Rais si ya kuisikia tu pasipo kuitafakari, na wala si ya kupigia mbiu za sifa kwa kuwa imebeba dhana potofu na kiukweli inahalalisha DHAMBI ya kikatiba kwa sababu tu DHAMBI ya kidini ingali inaishi...
 
Hizi ni fikra duni sana! Kwamba kwa kuwa watu wanavunja sheria na kukiuka katiba, hakuna haja ya katiba? Nchi imepatwa!!

Hivi ina maana Rais haelewi hata maana ya katiba? Katiba katika nchi ni rejea ya mambo yote ya kiutawala, miundo ya Serikali, sheria na taratibu.

Bila katiba, hakuna Serikali, hakuna bunge wala mahakama. Bila katiba, hakuna hata vyombo vya ulinzi na usalama wala teuzi.

Utamhukumu vipi mhalifu kama huna sheria inayotamka kuwa ukifanya hiki ni kosa, au umekiuka katiba ya nchi?

Mama Abdul awe anaandaliwa mambo ya kuongea mbele ya umma maana kila akitoa kauli, mara nyingi zinaudhalilisha ufahamu wake.
 
Sasa academic excellence inayokupelekea kufanya ujinga katika real life inakusaidia nini?. Hiyo ni eliimu ya makaratasi.
Unaiba hela za EPA, kodi za wananchi kufanyia kampeni chama kwenye uchaguzi ambao hakuna mpinzani wa kutisha kukitoa chama madarakani, hiyo IQ mbona haijimanifest?
 
Alisikika mlevi mmoja

Ukitaka kuujua Mwendo wa Kichaa, Mfunge Kilemba Kichwani
 
JPM alikuwa mwendawazimu akatuachia kichaa
Nashukuru kuliona hili kwani wengine humuona yeye kama malaika. Hili la ukichaa halistaajabishi kwani mtoto hufuata kichogo cha mleziwe. Usisahau kuwakumbusha wengine kwamba JPM alikuwa 'mwendawazimu' ili nao walijue hilo.
 
Huyu kapata urais kwa kupitia hicho kitabu ambacho leo anakibeza.
Kweli nyani haoni....
 
Mbele ya vichwa vyote vile, mbele ya makamera yote yale, mabalozi, vyama, teknologia...nk! Na chama chake kimeona na kusikia!! Yaani bila mabadliko ya Katiba... Tz inakuwa kama kioja gani sijui ...dah!
 
Ndo ukweli wenyewe huo…..
Kuongoza nchi hakuhitaji high IQ, just an average IQ can do!. Nyerere alikuwa high IQ, Mwinyi, average IQ sasa angalia aliyoyafanya Nyerere compared to Mwinyi na sasa yuko wapi?.

Tuje kwa Mkapa high IQ, JK average IQ, angalia aliyoyafanya Mkapa compared to JK na sasa yuko wapi?.

Njoo kwa JPM high IQ, Samia average IQ, angalia aliyoyafanya JPM compared na anachofanya Samia, na sasa yuko wapi?.

Kumbe uongozi wa juu wa Tanzania sio kupokezana tuu kwa dini, Muislamu na Mkristo, ni mpaka kupokezana kwa IQ, high IQ and average IQ, hivyo anayefuata ni high IQ, hivyo tuvumilie tuu tuvute subra, 2025 sio mbali, Mama atapumzika inaingia akili kubwa!.

Pia kuna tatizo la high IQ na longevity, hao high IQ wote tayari... average IQ wanaendea kudunda!.

P
 
Ngoja waje The Boss, The Big Show na FaizaFoxy πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯
 
Hizo "iq" walipimwa wapi na nani?
 
Mbona yeye akiambiwa na wanaccm wenzake kuwa yeye na serekali yake ni ya mpito anawahi kufungua katiba kuangalia ni wapi palipoandikwa serekali ya mpito?.

Hata wananchi tunahitaji katiba mpya kwa ajili ya kuangalia yanayofanywa na watawala kama yanaruhusiwa na katiba na wajibu wa watawala ni upi kwa wananchi wanaowaongoza.
 
Tatizo kuna watu wengine hawana uwezo wa kuchambua cha kusema na watu wa aina hii ni wale wanaoendeshwa na jazba wengine wanakuwa na inferiority complex lakini wapo pia wengine pia kwa kulazimisha waabudiwe wana kuwa na superiority complex. Wataalamu wa human resources tuambieni ni ipi hapo inferiority au superiority complex!!
 
Hatuna demokrasia. Katiba yetu ni ya kifalme
Mfalme ambaye sio mfalme. makasiriko na hasira ni sababu wana nzengo wanahoji kwanini unafanya hiki au kile. Sababu wanaruhusiwa kuhoji.
Muda unabadilika. Aliyeongoza jana asitegemee atatumia mbinu zile zile kuongoza leo au kesho. Kuna nyakati watu watataka kupewa majibu ya maswali magumu, hata kama watawala maswali hayo hayata waridhisha.
Mfano mdogo tu, imeshindikana kuifanya kesi ya uhaini sababu matokeo yake yangeleta madhara makubwa hata kwa watawala. Zamani ingewezekana. Leo ni kujivika mabomu ukisubiri yalipuke
 
Kalaghabao
 
Kalaghabao
Ndio wanavyosemaga. Mpaka meli imeanza kuzama. makasiriko kila sehemu. Hakuna hiki na kile sababu hakuna pesa. Tukishasimama sababu ya ujinga wetu, akili zitafunguka
 
Ujumbe huu Ndio anguko lako Mama!

Kwani wakati unashika kiti si ulikubaliana nao utaandika KATIBA mpya!?

MBONA kigeu geu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…