Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 73,773
- 102,126
johnthebaptist said:Kama kuheshimu Vitabu tungeheshimu Vitabu Vitakatifu, mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?"
Kukiuka maagizo yalipo kwenye kitabu au vitabu vya dini kunazalisha neno DHAMBI, na mshahara wake ni ADHABU kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya dini...(hii ni kwa wale waamini)
Kwa lugha nyingine ni kwamba kwa kuwa ameona kuwa watu wanakiuka maagizo na shurti zilizopo kwenye vitabu vya dini, lakini mwisho wa dahari kuna hukumu inayongoja mwanadamu...
Mawazo yaliyopo kwenye vitabu vya dini hayakuandikwa kwa utashi wa kibinadamu hivyo hakuna nafasi ya kubadilisha chochote ili kukemea au kubadili mwenendo wa binadamu kuacha uovu kwa sasa...
Unlike katiba ya nchi, hiki ni kitabu cha muongozo wa kisheria kilichotungwa na wanadamu ili kujiongoza wenyewe juu ya ardhi au eneo husika liitwalo nchi...
Kwa kuwa maudhui yake yameundwa na binadamu, hivyo si DHAMBI endapo mwanadamu ambaye ni mtunzi akitaka kuboresha au kunyumbulisha maneno yaliyopo ndani ya kitabu hicho kwa wakati unaofaa...
Kauli ya Rais si ya kuisikia tu pasipo kuitafakari, na wala si ya kupigia mbiu za sifa kwa kuwa imebeba dhana potofu na kiukweli inahalalisha DHAMBI ya kikatiba kwa sababu tu DHAMBI ya kidini ingali inaishi...