Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Ingekuwa nchi za watu wanaojitambua hii kauli ingetosha kumtimua Samia kwenye urais
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kiongozi wa kuchaguliwa na kiongozi aliyekaimishwa madaraka kwa mujibu wa katiba.

Pamoja na mapungufu ya katiba ya 1977 iliyotoa mianya ya uvunjaji sheria na uporaji haki kwa wananchi, bado viongozi wanaaminika walichaguliwa bado waliheshimu katiba ya nchi, hawakuwahi kuikejeli.

Nini kimekipata chama hiki CCM kutoa zao la katiba kuwa kejeli kwa katiba hiyo,huku wapambe wakishangilia na simanzi kubwa kwa wazee wa Taifa hili.

Je, ni ulevi wa madaraka au kuyazoea madaraka na kuwapima wananchi ukomo wa mamlaka yao?

Kwenye kongamano la vyama vya siasa na wadau wa demokrasia kauli za kuidharau katiba inayotambua uwepo wa taasisi zao Kuna pelela ujumbe gani kwao.

Ni kweli katiba iliyoitwa kitabu haileti maendeleo katika nchi na kama haileti kulikuwa na haja gani ya kuwa na katiba?

Je, ni kweli kitabu hiki ni kwa ajili ya ethics na mambo mengine isipokuwa maendeleo ,na kama ndivyo hivyo kwani alikubali madaraka yaliyotokana na hicho kitabu.

Kama Rais haamini katika katiba, anakosa uhalali wa urais wake maana kapatikana kwa zao la katiba hiyo hiyo.

Ndiyo maana kwa hata mikataba tunayoingia kama nchi inaukiukwaji Mkubwa wa katiba yetu.

Kwa hili Rais anapaswa kujitafakari kama anastahili kuendelea kuwa Rais.
 
Nadhani kuna mahali kakengeuka kwakuwa katiba ndio imemfanya awe hapo alipo... Nachelea kusema rais amezingwa na msongo mkubwa wa mawazo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni tafsiri tu ya kile alichokisema...

Mh.Rais anaiheshimu katiba ila haijiendeshi.....inatafsiriwa na BINADAMU na inasimamiwa nao....

Katiba ni jengo ambalo ndani yake kuna shughuli na Maisha ya watu.....

MAENDELEO hufanywa humo ndani ya nyumba na hao binadamu.....

Si katiba itakayoleta hayo MAENDELEO bali ni hao wakazi wa hiyo nyumba.....

Binafsi nimemuelewa mh.Rais SSH [emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwani yule Mkuu wa Majeshi anashindwa kwenda Ikulu kumwambia huyu Mama aachie ngazi maana naona kachanganyikiwa,Kuna siku mtakuja kumkuta anakimbia uch* feri!
 
🤣🤣

..nadhani amechanganyikiwa.

..hayuko sawasawa huyu.
 
Au Waingereza wangekataa kutupa Uhuru kwasababu hatuna elimu ya Uhuru na kujitawala ingekuwaje!
Kweli kabisa! Hebu imagine kiongozi kusema hivyo. Mfano alipotoa hotuba kwani alianza kuwapa watu elimu ili waelewe atakachozungumza na kwamba kama wasingeelewa then asingeweza kutoa hotuba? Au vitabu vya dini kuandikwa, kwani vilisubiri mpaka watu wapewe elimu kwanza?
 
Shida yetu ni sisi wananchi kutokuwa wamoja... Utofauti wetu kimawazo ndio unaopelekea tudharauliwe na wanasiasa. Wananchi hawajui nini wanataka, wanaona makosa yanatendeka na bado wanaenda kumchagua huyo huyo kiongozi, kwa sababu tu anatoka CCM.

Nchi zilizoendelea kidemokrasia hazichagui rais kutokana na chama, zinachagua rais kutokana na uwezo wake binafsi.

Sasa hapa watu wameshaona Rais hafati kauli za wananchi na bado 2025 wataenda kumchagua. Kisha wataanza kulia tena 2026.
 
Rais kafika mbali sana kwamba katiba ya nchi ni kitabu, maana yake anachoamua kipo na nguvu kuliko katiba ya nchi ,

Aisee nimeogopa sana, kwamba tasisi , zote, wananchi wate wachukulie katiba ni kitabu, haisee , tuliombee taifa
 
Actually, msingi wa kuwa na katiba nzuri ni kupata sheria nzuri zitakazowalinda wananchi na mali zao na rasilimali za nchi. Katiba ya sasa imejaa 'clawbacks' ambazo zinafanya haki zilizotolewa zinyang'anywe tena na pia ilitungwa wakati wa mfumo wa chama kimoja na ndiyo maana hata pale vyama vingine vina haki ya kufanya mikutano yao inaingiliwa kwa sababu unakuta sheria iliyotungwa inakuwa na nguvu zaidi kuliko katiba yenyewe. Polisi akizuia jambo hata kama amefanya hivyo kimakosa anaonekana alichokifanya ni amri au agizo "halali" (alilolifanya with the authority of the law). Sasa kama hatupati katiba inayoweza kuweka msingi mzuri wa sheria zetu wananchi wataendelea kukosa haki zao za msingi na kuumizwa hata pale wanapokuwa na haki ya kufanya jambo ambalo wanakatazwa wasifanye.
 
Bwashee wewe Katiba unaielewaje? Ni nini?
Katiba pia itasaidia kuwawajibisha wale viongozi wasiotimiza wajibu wao wakaishia kula rushwa. Jambo hilo linaweza kuchochea maendeleo. Tungekuwa tuna sheria kama za china mla rushwa haijalishi ni waziri ananyongwa, kiwango cha ufisadi bila shaka kingepungua maana mtu anajua akikamatwa wanalala na kichwa chake.
 
chadema wanataka kuligawa taifa kwa vitabu tumewashitukia hongera mama kwa kutengua huu mtego mbaya kabisa.

tuko na wewe bega kwa bega
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…