Rais Samia, naona kuna haja ya kulitazama upya Fao la Kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

Rais Samia, naona kuna haja ya kulitazama upya Fao la Kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

TUPAMBANE

Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
62
Reaction score
88
Poleni Watanzania.

Kwako Mama Samia Suluhu, nakuomba sana uturudishie haki yetu iliyopotea ghafla ya fao la kujitoa NSSF. Nakuomba sana futa sheria kandamizi dhidi ya Wafanyakazi. Mtu anaacha kazi kafanya miakaa 15 au 20 halafu unakuja kumwambia asubirie mpaka afikishe miaka 55 au 60 je hii ni sahihi? Nakuomba sana rudisha mfumo ule ule wa JK ukijitoa unapewa chako basi mambo yanaendelea.

Kumbuka mtu huyo kalipa kodi zake zote lakini siku akifukuzwa kazi anajifariji na fedha zake zilizopo NSSF lakini cha kushangaza mtu huyo unamminya na kumwambia asubirie miaka 60.

Nakuomba sana baada ya kukabidhiwa kiti anza na hili, pia piga panga Sheria kandamizi.
 
Tuko katika kipindi cha majonzi tuache kwanza kila jambo linafanyika kw kusidio kwaajil ya kujenga nchi kama mafanikio ya kujengwa kw reli,flyover, viwanda, madaraja kuongezeka kwa bajet ya mfuko wa afya kwahiyo jiongenze kw kusimamishwa hiki ni kwaajil ya kuimarisha kitu fulan ilhali tupate maendeleo na kuelekea ktk uchumi wa kati tunapokimbilia.
 
Suala hili si la kumuomba mama Samia,bali muombe Mungu.Kwani waliolileta bado wapo sana.Ogopa wasomi wenye roho mbaya,unaweza kumlaumu bure kiongozi kumbe kadanganywa.

Naamini Mungu wetu hajalala,bali atajibu kwa wakati wake.
 
Hapo umeongea chief wengine pressure zinapanda na kushuka,kisukari Khali si Khali miradi imefungwa wawekezaji CHALI Basi kidogo chetu Cha kwetu tupewe.Mzee wa Chatu hakuwa mbaya wapambe upambe umemupamba akapumbazika.

Bwana amemupenda kuliko sisi.

Amen.
 
Tuko katika kipindi cha majonzi tuache kwanza kila jambo linafanyika kw kusidio kwaajil ya kujenga nchi kama mafanikio ya kujengwa kw reli,flyover, viwanda, madaraja kuongezeka kwa bajet ya mfuko wa afya kwahiyo jiongenze kw kusimamishwa hiki ni kwaajil ya kuimarisha kitu fulan ilhali tupate maendeleo na kuelekea ktk uchumi wa kati tunapokimbilia.
Poleni wafiwa..
 
Suala hili si la kumuomba mama Samia,bali muombe Mungu.Kwani waliolileta bado wapo sana.Ogopa wasomi wenye roho mbaya,unaweza kumlaumu bure kiongozi kumbe kadanganywa.

Naamini Mungu wetu hajalala,bali atajibu kwa wakati wake.
Kama kadanganywa ina maana hasikii minong'ono mitaani au mitandaoni kila mahali watu wanalalamika.

Halafu kuna mambo huwezi kudanganywa ukiwa na akili za kawaida hivi Rais hajui kumzuia mtu aliyeachishwa kazi akiwa na miaka 30 asubiri miaka 60 ndo apewe mafao hajui kama inamuathiri hadi adanganywe? Usikute yeye ndo kapendekeza hilo ili serikali ipate fedha za kuendesha miradi huku raia wakitaabika.
 
Nalia msiba lakini nawaza hela zangu za PPF, zilishagoma kutoka, Mungu saidia sheria ya mifuko ya pension irekebishwe
 
Back
Top Bottom