Rais Samia, naona kuna haja ya kulitazama upya Fao la Kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

Rais Samia, naona kuna haja ya kulitazama upya Fao la Kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

Binafasi sikubaliani kabisa na huu utaratibu wa sasa wa NSSF kulipa fao la kukosa ajira kwa miezi 6, pesa ni zangu kwanini nisipewe zote kwa mkupuo ili niweze kupanga mambo yangu ya maendeleo ? Hiii sheria imekua kandamizi sana

Ajira za makapuni binafsi nyingi sio za uhakika na asilimia kubwa ni za mikataba, mmiliki wa kampuni muda wowote anaweza akaamua kufunga biashara zake na kurudi nchini kwake au asikuongeze mkataba hasa hasa kwa hawa wawekezaji wa kigeni.

Kwanini tuzungushane wakati lile ni jasho langu ? Inamana hii mifuko ya hifadhi ya jamii imelenga kutufanya tuwe watu wa kutegemea tu kuajiriwa miaka yote ? What if kama nataka pesa zangu niende nikajiajiri ?

Tunaomba muheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan amulike hizi sheria kandamizi na ikiwezekana azifanyie marekebisho na kurudisha fao la kujitoa.
Sheria hii ilipitishwa Kwa vile serikali ilijikopesha fedha huko na pia mifuko kufilisika Kwa kuwekeza kwenye miradi isiyo na tija kwa muda mfupi. Hali hi ilifanya washindwe kulipa mafao Kwa wanachama., Hivyo wakaona wazuie fao hilo hadi mtu afikishe 60.zuio hili lilipitishwa na wabunge kwa kishindo... Hulu wao wakijihakikishia kiinua mgongo cha mamilion kila wamalizapo kipindi Cha miaka mitano ya ubunge!!!!!!
 
Sasa hapo cha bure ni kipi mkuu? Mtu kudai haki ya mafao yake halali ni kupenda bure?
Au hujawahi kufanya kazi zenye makato ya lazima ya NSSF au mifuko ya jamii jwa ujumla.
Mkuu msamehe ....
 
Kwa vile hili halina maslahi kwa wanasiasa wala haliwezi kusaidia kuingia ikulu kirahisi au kupata ubunge kirahisi wala huwezi kuwasikia....hili ni lakupiganiwa na watanzania wote wanaoteseka sio hawa wanasiasa..

Ni vyema zikakusanywa saini kama 1000 hivi kupitia hata humu JF na wawakilishi wakaombwa kukutana na Mama....naamini mama ni msikivu hili likifika mezani kwake atalitolea maamuzi haraka..
 
Kwa hatua na uongozi mzuri wa kupenda haki wa Mh Rais Mama yetu Mpendwa SASHA
Binafsi naamini atalifanyia kazi suala hili.,

itasaidia watu kujiajiri, kuajiri wengine na kujikwamua kiuchumi
Ni namna mojawapo ya expansionary monetary policy.,kurudisha fedha stahiki kwa wananchi na kuinua uchumi
 
Poleni Watanzania.

Kwako Mama Samia Suluhu, nakuomba sana uturudishie haki yetu iliyopotea ghafla ya fao la kujitoa NSSF. Nakuomba sana futa sheria kandamizi dhidi ya Wafanyakazi. Mtu anaacha kazi kafanya miakaa 15 au 20 halafu unakuja kumwambia asubirie mpaka afikishe miaka 55 au 60 je hii ni sahihi? Nakuomba sana rudisha mfumo ule ule wa JK ukijitoa unapewa chako basi mambo yanaendelea.

Kumbuka mtu huyo kalipa kodi zake zote lakini siku akifukuzwa kazi anajifariji na fedha zake zilizopo NSSF lakini cha kushangaza mtu huyo unamminya na kumwambia asubirie miaka 60.

Nakuomba sana baada ya kukabidhiwa kiti anza na hili, pia piga panga Sheria kandamizi.
World wide hakuna fao la kujitoa.
Sasa utataka tuwe watu wa ajabu ktk hii dunia?
 
Wabunge ambao hatukuwachagua wataweza kulitetea hilo ? Naona wako maslahi yao pekee.....hata hakuna anaejali wafanyakazi huko.....
 
Kwa vile hili halina maslahi kwa wanasiasa wala haliwezi kusaidia kuingia ikulu kirahisi au kupata ubunge kirahisi wala huwezi kuwasikia....hili ni lakupiganiwa na watanzania wote wanaoteseka sio hawa wanasiasa..

Ni vyema zikakusanywa saini kama 1000 hivi kupitia hata humu JF na wawakilishi wakaombwa kukutana na Mama....naamini mama ni msikivu hili likifika mezani kwake atalitolea maamuzi haraka..
Wabunge wangejitahidi japo kidogo kuacha ubinafsi
Wao kila baada ya miaka 5 wanapewa chao
 
Count me in
 
Tuko katika kipindi cha majonzi tuache kwanza kila jambo linafanyika kw kusidio kwaajil ya kujenga nchi kama mafanikio ya kujengwa kw reli,flyover, viwanda, madaraja kuongezeka kwa bajet ya mfuko wa afya kwahiyo jiongenze kw kusimamishwa hiki ni kwaajil ya kuimarisha kitu fulan ilhali tupate maendeleo na kuelekea ktk uchumi wa kati tunapokimbilia.
Daaah unaongelea jasho la mtu usiyefahamu madhila yake ilhali wewe mambo safi!
 
Wabunge wangejitahidi japo kidogo kuacha ubinafsi
Wao kila baada ya miaka 5 wanapewa chao
Tunawasema vibaya Wahindi lakini hata hapa kwetu kuna kamfumo fulani ka ubaguzi na ukandamizaji...
Tumekubali kutengeneza kundi fulani special la wanasiasa... tumewapa uheshimiwa...
Wakati wenguine tunakula kwa urefu wa kamba zetu... wao hawana kamba kabisa!!
Wanatuona na kutuita wanyonge!
 
Back
Top Bottom