Rais Samia, naona kuna haja ya kulitazama upya Fao la Kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

Rais Samia, naona kuna haja ya kulitazama upya Fao la Kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

IMG-20210318-WA0000.jpg
 
Na Mwenyezi Mungu atambariki sana mama kwa kirejesha fao hili.
 
We jamaa una akili sana hilo mimi limenigusa kwa asilimia zote pesa zangu wanazo nssf alafu tunasota mtaani
Napendekeza akimaliza suala la fao la kujitoa wafanyakazi wapate haki zao pia awaamuru watoa huduma za simu wafungulie line zote zilizofungwa kwa amri ya serikali mpaka NIDA wamalize zoezi la kutoa vitambulisho vya taifa kwa sababu watu wengi hasa vijijini wanateseka sana kwa kukosa simu.
 
Naunga mkono hoja, fao la kujitoa lirudi, kila mtu afe na chake sio mpaka usubiri ufike 55.
 
Mkuu hicho siyo cha bure. Ni jasho la mchangiaji kijana anayehitaji fedha hizo zimsaidie kuanzisha biashara baada ya kukoma kwa ajira.
Hao ndio MATAGA aka Zero Brain ,yaani anasema wazi kabisa kwamba fedha za NSSF ni za bure ,hajui hata zinapatikana vipi na ndio wao waliokuwa wanasifia UTOPOLO.
 
Nafikiri Ni uungwana wa kiafrika kusubiri maziko kwanza ndipo mwenye kumdai au kudaiwa na marehemu anatakiwa kujitokeza.
Hivyo, madai yako vuta subira kidogo tafadhali. Embu tuletee mazuri ya JPM kidogo wakati huu wa majonzi Kama itakupendeza kufanya hivyo.

Kwa mfano, aliweza kutekeleza miradi mikubwa Kama vile SGR, Mradi wa ememe was Mwl Nyerere, kuhamia Ddm, etc. Kwa Kasi na viwango tofauti na waliomtangulia.
 
Hadhi na sheria zianze kuzingatiwa kama zamani ndio nchi itarudia heshima yake vinginevyo ni maajabu tu yataendelea kutokea, wastaafu wapewe haki zao, kuna mmoja alistaafu miaka mitatu iliyopita amepewa mafao kiduchu sasa wakati anafuatilia yaliyobakia anazungushwa mara anaambiwa alete vyeti vya form four yaani tiktaka kibaaao sijui wanataka afe ili haki yake ipotee na mtu mwenyewe mgonjwa. Watu wameonewa sana na lazima mambo yarekebishwe ili taifa lipone vinginevyo hasira ya Mungu haitakoma.
 
Mheshimiwa Samia, nakuomba utakapochukua ofisi Anza na hii sheria ya kinyonyaji ya fao la kujitoa kwani sheria hii ilipitishwa makusudi ili kuwakandamiza wafanyakazi hasa wale wa sekta binafsi ambao mikataba Yao ni ya muda mfupi kwa walio wengi na pindi mkataba unapoisha anaambiwa pensheni yake atasubiri Hadi akifika miaka 60. Futa sheria hii ya kikoloni ili urejeshe furaha kwa wafanyakazi
 
Kusema ule ukweli hili la fao la kujitoa linawaumiza wengi na ni dhuluma ya moja kwa moja kwa mfanyakazi ambaye amekatwa pesa zake kwa ajili ya hifadhi ya mifuko ya jamii, sasa unakuta mtu kapata mkataba wa muda mfupi na ukiisha ndo mwisho wa ajira yake hasa kwa upande wa private sector lakini ukienda kudai hela kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii utajuta hata kwa nini umeamua kufuatilia maana unapata stress tu bila majibu ya kueleweka.Naamini Mama Samia atalifanyia kazi hili na mengine mengi.
 
kipi bora tusubirie alafu tusahau? ngoja akae Nalo kabisa ajue kilio chetu. NSSSSSSSSSF Yangu na wala sio ya kwao mbona wakibana vizuri wanaweza kupata zaidi ya hizo fedha waniambie niwabunie njia ya kuingiza fedha?
 
Back
Top Bottom