Rais Samia, naona kuna haja ya kulitazama upya Fao la Kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

Sheria hii ilipitishwa Kwa vile serikali ilijikopesha fedha huko na pia mifuko kufilisika Kwa kuwekeza kwenye miradi isiyo na tija kwa muda mfupi. Hali hi ilifanya washindwe kulipa mafao Kwa wanachama., Hivyo wakaona wazuie fao hilo hadi mtu afikishe 60.zuio hili lilipitishwa na wabunge kwa kishindo... Hulu wao wakijihakikishia kiinua mgongo cha mamilion kila wamalizapo kipindi Cha miaka mitano ya ubunge!!!!!!
 
Sasa hapo cha bure ni kipi mkuu? Mtu kudai haki ya mafao yake halali ni kupenda bure?
Au hujawahi kufanya kazi zenye makato ya lazima ya NSSF au mifuko ya jamii jwa ujumla.
Mkuu msamehe ....
 
Kwa vile hili halina maslahi kwa wanasiasa wala haliwezi kusaidia kuingia ikulu kirahisi au kupata ubunge kirahisi wala huwezi kuwasikia....hili ni lakupiganiwa na watanzania wote wanaoteseka sio hawa wanasiasa..

Ni vyema zikakusanywa saini kama 1000 hivi kupitia hata humu JF na wawakilishi wakaombwa kukutana na Mama....naamini mama ni msikivu hili likifika mezani kwake atalitolea maamuzi haraka..
 
Kwa hatua na uongozi mzuri wa kupenda haki wa Mh Rais Mama yetu Mpendwa SASHA
Binafsi naamini atalifanyia kazi suala hili.,

itasaidia watu kujiajiri, kuajiri wengine na kujikwamua kiuchumi
Ni namna mojawapo ya expansionary monetary policy.,kurudisha fedha stahiki kwa wananchi na kuinua uchumi
 
World wide hakuna fao la kujitoa.
Sasa utataka tuwe watu wa ajabu ktk hii dunia?
 
Wabunge ambao hatukuwachagua wataweza kulitetea hilo ? Naona wako maslahi yao pekee.....hata hakuna anaejali wafanyakazi huko.....
 
Wabunge wangejitahidi japo kidogo kuacha ubinafsi
Wao kila baada ya miaka 5 wanapewa chao
 
Count me in
 
Daaah unaongelea jasho la mtu usiyefahamu madhila yake ilhali wewe mambo safi!
 
Wabunge wangejitahidi japo kidogo kuacha ubinafsi
Wao kila baada ya miaka 5 wanapewa chao
Tunawasema vibaya Wahindi lakini hata hapa kwetu kuna kamfumo fulani ka ubaguzi na ukandamizaji...
Tumekubali kutengeneza kundi fulani special la wanasiasa... tumewapa uheshimiwa...
Wakati wenguine tunakula kwa urefu wa kamba zetu... wao hawana kamba kabisa!!
Wanatuona na kutuita wanyonge!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…