Rais Samia ndani ya Dubai EXPO 2020 kutangaza fursa za biashara na uwekezaji Tanzania

Kuamua kujitegemea ni suala zuri. Lakini tangu uhuru tunapiga hizi blah blah kila mwaka. Mzungu anapochota mali zetu ni kwamba kapewa upenyo na sisi wazalendo wenyewe.

Huwa sipendi kumlaumu mzungu kwa makosa yetu ya kila siku. Walioiba pesa ya EPA ni waswahili wenzetu wakishirikiana na wafanyabiashara wa kihindi. Waliopa pesa ya GAPCO awamu ya kwanza ni waswahili wenzetu.

Wizi wote unaofanyika serikalini wahusika wakuu ni wajomba na shangazi zetu. Na ni hawa hawa baadhi yao wanakuja humu jukwaani na falsafa za kujitegemea, wanamlaumu SSH wakati wamechangia kuharibu uchumi tangu 1961.
 
Tangu uhuru nchi inaongozwa na wazalendo waliozaliwa hapa hapa Tanzania. Wameshindwa vipi kuja na mawazo kama ya kwako?.

Awamu ya Mkapa ilibinafsisha mashirika mengi ya umma yaliyoanzishwa na wazalendo wenye akili kama hizi hizi za uzawa kwanza.

Tumuache SSH afanye anavyoona naamini anayo nia njema ya kutafuta wawekezaji huko nje.
 
Kama ilikuwa na lengo hilo ulilosema basi ni vyema na haki. SSH ameshasema kuwa mpango ni ule ule wa awamu ya tano wa win win situation.
 
Ndio Maana nimesema kujitegea tunaweza nisuala la utashi tu, tatizo viongozi wetu waliisha jiaminisha kuwa hatuwezi kupasua pasipo mzungu, niujinga mtupu Samia sasahivi anacho fanya ni Kama mchuuzi tu, hawezi pata mwekezaji wa maana Sanasana matapeli aliokuwa amewapata Kikwete.Kujitegemea inawezekana.
 
Ugumu wa kujitegemea unapendwa na mzungu na siku zote anatuwekea vizingiti ili kukwaza kujitegemea kwetu. Anajua atubane wapi ili tusipumue.
 
Kama ilikuwa na lengo hilo ulilosema basi ni vyema na haki. SSH ameshasema kuwa mpango ni ule ule wa awamu ya tano wa win win situation.
Mpango siyo ule ule, awamu ya tano haikuwa inafata wawekezaji kwa staili hiyo ya sasa, ukiamua kuwafata kwanza tengeneza au andaa wawekezaji wa ndani..taifa gani halina muda wa kujifunza na kurekebisha mapungufu, kila siku mapambio ya kutafuta wawekezaji, matokeo tunapata wezi tu!
 
Una uhakika wawekezaji wa ndani hawapo?. Serikali inaongozwa na watu waliokwenda vyuoni na wakafaulu, ni lile tabaka la juu lililofaulu vyema huko mashuleni.

Wanajua wanachokifanya.
 
Tumuache afanye anayoona ndio nini..kwa hiyo mambo ya dowans yarudi tena...nyinyi ndio mnaleta keleke kusifia sifia hata yssiyostahili kusifiwa, duniani hapa kuheshimiwa kunatokana na kujitegemea tu! nje ya hapo ni ujinga na kudharauliwa hata na wasiostahili kukudharau.
 
Una uhakika wawekezaji wa ndani hawapo?. Serikali inaongozwa na watu waliokwenda vyuoni na wakafaulu, ni lile tabaka la juu lililofaulu vyema huko mashuleni.

Wanajua wanachokifanya.
Wapo!
Kupiga kengele kuita wawekezaji hucho ndio wanachojua...toka wameanza wana cha kuonyesha..
Kufaulu chuo siyo warrant ya kujua unachofanya, unaweza kufaulu kwenye makaratasi tu lakini ujinga haujatoka bado!
 
Kurudi kwa Dowans ni wasiwasi wako mkuu. Hiyo EXPO inakwenda kuwasaidia watanzania wenzetu kama mimi na wewe hatuoni umuhimu wake.

Kama mimi na wewe akili zetu zinaishia kulalamika tu humu jukwaani. Kumbuka muda huu kuna watu wanazitumia hizi hizi fursa ambazo wewe unazipigia kelele na zinawatajirisha.
 
Fursa gani, zitaje...nani anufaike, hakuna lolote! Hatulalamiki, tunawaambia hayo wanayofanya kutumia kodi zetu kusafiri kutafuta wawekezaji hatutaki!
 
Fursa gani, zitaje...nani anufaike, hakuna lolote! Hatulalamiki, tunawaambia hayo wanayofanya kutumia kodi zetu kusafiri kutafuta wawekezaji hatutaki!
Fusa zipo nyingi mkuu. Kuna mafuta kule ukumbuke hilo. Ndio maana nimesema kwa wenye akili kubwa wanajiandaa kufaidika na hii ziara, sisi wenye akili ndogo tuendelee kuanzisha mada JF za malalamiko.
 
Ugumu wa kujitegemea unapendwa na mzungu na siku zote anatuwekea vizingiti ili kukwaza kujitegemea kwetu. Anajua atubane wapi ili tusipum

Fursa gani, zitaje...nani anufaike, hakuna lolote! Hatulalamiki, tunawaambia hayo wanayofanya kutumia kodi zetu kusafiri kutafuta wawekezaji hatutaki!
Huyu Samia anakwenda kuokota wahuni tu barabarani na kutuletea eti ni wawekezaji, Sijui kwanini viongozi wetu hawajifunzi kwa waliowatangulia,madini yetu yote yamesombwa na hao wanaoitwa wawekezaji uchwala, kuanzia Alumas na Zahabu,sijawahi watanzania tulichonufaika nacho kupitia hao wawekezaji, sana sana kuachia wananchi umasikini na magonjwa huku hao wawekezaji wakijenga majumba huko ulaya.Watanzania hatuitaji wawekezaji tunaitaji kiongozi mwenye vision,wa kuondoa mentality ya kujiona hawezi,na kuwaambia wachape kazi kwa bidii,uku serikali ikiweka miundombinu wezeshi na masoko ya bidhaa zao,sio mwekezaji akija anapumnguziwa mikodi huku mwekezaji mzawa anarundikiwa mikodi kibao
 
Fusa zipo nyingi mkuu. Kuna mafuta kule ukumbuke hilo. Ndio maana nimesema kwa wenye akili kubwa wanajiandaa kufaidika na hii ziara, sisi wenye akili ndogo tuendelee kuanzisha mada JF za malalamiko.
Akili kubwa kwenda expo dubai? That's an adolescence outlook!
 
Hizi zako ni akili zile zile za kichoyo na kibaguzi. Umaskini siku zote ni changamoto ya mtu au watu kuutafuta utajiri kwa udi na uvumba.

Huwezi kuendelea kwa kukwepa changamoto, hili kwanza kabisa ulijue na likukae kichwani mwako. Mchina asingeendelea kama asingetaka kuyatumia maendeleo ya wengine kama changamoto.

Anayelala tu akijifariji kwa utajiri wake wa asili atambue kuwa huo utajiri wake ni umaskini wake wa leo na kesho.

Ni rahisi kupiga kelele humu jukwaani lakini ni ngumu kuendelea kwa kujifungia ndani tu.
 
Jaribu kuelewa suala si kujifungia ndani, kwanza tengeneza yanayohitajika ndani ili ajenda ya uwekezaji ifanikiwe kabla ya kutoka nje, pili wawekezaji hawatafutwi hivyo, unaweza ishia kupata matapeli tu, au basi vile umewafata wnakulazimisha ufanye wanavyotaka wao ili waitike mwaliko wako, hata km ni kwa gharama ya kuumiza watu wako!
 
Sio EXPO pekee yake, popote pale penye kuibuka fursa za kidunia.
Kwa kweli ningesifu safari za aina ya dubai expo kama Rais angeenda kuonana na wawekezaji ambao wana track record nzuri yenye mafanikio kwenye eneo fulani walilowekeza na hivyo anawashawishi waje Tanzania pia wafanye kama walivyofanya sehemu nyingine..lakini si kwa staili hii ya dubai expo au ile ya ufaransa na ubelgiji..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…