Rais Samia ni kiongozi mwenye maono sana

Simpambi Ila kazi zake zinampamba Sana pasipo hata kukupa watu wakumpamba, nisipompongeza Mimi bado watanzania wengi watasimamia kumpongeza, wanafunzi wanaokwenda kupata elimu bure kidato Cha sita watasimamia kumpongeza, wazazi watampongeza tu kwa kupunguziwa adha ya kukupa Ada kidato Cha tano na sita watampongeza tu hata kana tutasema tukae kimya, wakulima ambao Sasa wanauza mazao yao kwa Bei nzuri watampongeza tu, wafanya biashara za mahotel ya kutalii watampongeza tu kwa mafuriko ya watalii wanaendelea kufurika hapa nchini

Narudia, hizi sifa ulizomwaga hapa ni kutokana na ulaji unaopata. Hata waliokuwa wanawapamba madictator walikuwa wanamwaga sifa za aina hii hii.
 
Narudia, hizi sifa ulizomwaga hapa ni kutokana na ulaji unaopata. Hata waliokuwa wanawapamba madictator walikuwa wanamwaga sifa za aina huu hii.
Yani Hawa jamaa sijui Wana matatizo GANI kwenye bongo zao, mbona anasifiwa utendaji ni wa kawaida sana
 
Huyu hakuna kitu.

Walamba asali mnapiga debe tu lakini ukweli mnaujua kua hapa hakuna kitu.

Ndani ya mwaka mmoja inflation iko 100%+ na yeye hataki kukubali kua Serikali yake ni dhaifu anasingizia Urusi.

Urusi ndio imepandisha gharama za unga, mchele, bando, nguo hata za mtumba, makaratasi na kila kitu kwa 100%?

Huyu hajui hata anachokifanya.
 
Yani Hawa jamaa sijui Wana matatizo GANI kwenye bongo zao, mbona anasifiwa utendaji ni wa kawaida sana

Wanajaribu kutufool hata huku mitandaoni kama wanavyowajaza ujinga wananchi huko kwenye ziara zao. Utasikia kiongozi yuko kwenye ziara kuzungumza na wananchi, cha ajabu ni yeye mwenyewe na wapambe wake wanawahubiria wananchi, lakini hakuna mwananchi mwenye ruhusa ya kuuliza zaidi ya kushangilia, na ikitokea mtu akauliza, basi ujue amepangwa.
 
Hata HIVYO labda KWa ambao ni wageni na ziara hizi pale ukiona sehem flani anaenda kuhutubia jua watu wametoka almost kila wilaya kujaza vichwa, utaona watu wengi lakini sio wa sehem husika wengi hukodishiwa mpaka mabasi fika alipo,
Wakati huo unakuta week 1 au 2 kabla team chahwa wapo busy andaa watu kusifu na kupongeza,
Bila ayo kufanyika uwanjani utamkuta na watu mia ambao ni labda ni viongonzi, kwa ground, Mambo ni magum Sana KWa ccm na viongonzi wake
 
Yeye kama yeye Rais Samia ana maono ila tatizo kubwa yupo compromised by 100%. Na hili tatizo lilianzia mwa Mwinyi, Mkapa akalikwepa, alivyokuja Kikwete akawa compromised by 200% na alivyokuja Dkt Magufuli akaepuka, ila ndiyo hivyo kikundi kilichomcompromise Kikwete kikaona kimepoteza na kikatafuta mbinu na kikajua kabida akifa Dkt Magufuli basi anayefuata ni Rais Samia hivyo kikaanza kumuandaa mapema kabisa kwa ku compromise (inasemekana ndiye alikuwa anapeleka habari kwa kigogo, na mangi zile za ikulu), na baada ya kumuua Dkt Magufuli, basi kawa rais ila wanajua alivyomfitini Dkt Magufuli na serikali ambapo ni kinyume na kiapo na maadili na lazima hicho kikundi kumtumie kitakavyo. Hivyo Rais Samia hana jinsi hat kidogo, na hii mbinu inatumika sana nchi zetu za ki africa. Suluhisho huwa ni kuhakikisha wale ambao wapo compromised hawapewi nafasi kubwa serikalini, lakini hapa nchi zetu ni tofauti, unakuta mtu kama Makamba eti waziri wakati yupo compromised kinoma au Nape ambaye alikula rushwa na mil 800 sakata la cloud halafu eti waziri wa habari, na hiyo ndiyo serikali ya Mama Samia.
Kusema kuwa Rais JPM aliuwawa na kundi la watu ni kuendekeza habari za vijiweni, ni kuugeuza uongo ili uonekane kama ni ukweli. Hakuna ushahidi wa uhakika kabisa unaoweza kueleweka ukiwekwa wazi wa tukio zima la kuondoa uhai wa JPM ni minong'ono inayotokana na mapenzi yao makubwa waliyokuwa nayo kwa hayati.

Hakuna rais mwenye jeuri ya kumfurahisha kila mtanzania huyo hayupo. Pia hakuna rais mwenye kuchukiwa na kila mtanzania, huyo hayupo. SSH anafanya mengi ambayo hayati hakuweza kuyafanya. JPM alifanya mengi ambayo SSH hata ndotoni mwake hawezi kuja kuyafanya.

Wote wawili ni nafsi zilizotoka kwa muumba, hivyo kwa namna moja au nyingine zinatufaa katika suala zima la uongozi.
 
Narudia, hizi sifa ulizomwaga hapa ni kutokana na ulaji unaopata. Hata waliokuwa wanawapamba madictator walikuwa wanamwaga sifa za aina hii hii.
Hapana Sina ulaji wowote nap upata kwa mh Rais zaidi ya kazi njema na yakutukuka anayoifanya kwa nchi yetu, mama anashugulika na matatizo ya watu kwa Kasi ya ajabu, mama ana sikia sauti zote zipazwazo na watanzania na kujibu kwa matendo bila kuacha mashaka, Tuna kila sababu ya kumtia moyo kwa kazi kubwa anayo ifanya katika Taifa Hilo, Tuungane watanzania kuijenga nchi yetu ambayo my Rais anashindwa hata kupata usingizi akiwawaza watanzania Namna ya kutukwamua kiuchumi katikati ya matatizo yaliyotikisa uchumi wa Dunia yote,majanga Kama vile Corona iliyosababisha kufungwa kwa shughuli za uzalishaji na pia Vita inayoendelea ukrein na Urussi iliyopelekea mfumuko wa Bei wa bidhàa Kama mafuta ambayo Ni injini ya uchumi katika nchi, hata hivyo mh Rais anaendelea kushugulika na suala Hilo kwa kuweka Ruzuku ya billioni moja kupunguza makali hayo ya bei
 
Kusema kuwa Rais JPM aliuwawa na kundi la watu ni kuendekeza habari za vijiweni, ni kuugeuza uongo ili uonekane kama ni ukweli. Hakuna ushahidi wa uhakika kabisa unaoweza kueleweka ukiwekwa wazi wa tukio zima la kuondoa uhai wa JPM ni minong'ono inayotokana na mapenzi yao makubwa waliyokuwa nayo kwa hayati.

Hakuna rais mwenye jeuri ya kumfurahisha kila mtanzania huyo hayupo. Pia hakuna rais mwenye kuchukiwa na kila mtanzania, huyo hayupo. SSH anafanya mengi ambayo hayati hakuweza kuyafanya. JPM alifanya mengi ambayo SSH hata ndotoni mwake hawezi kuja kuyafanya.

Wote wawili ni nafsi zilizotoka kwa muumba, hivyo kwa namna moja au nyingine zinatufaa katika suala zima la uongozi.
Tuwe wakweli, gharama ya maisha imekuwa juu sana. Rais Samia amechangia kwa kiwango kikubwa huu mfumuko kwa sababu ya washauri wanaomuweka angle ili achukiwe.
 
Gharama za maisha zimepanda dunia nzima. Wa kulaumu ni watu kama Putin na wababe wengine wanaofikiria ya kwao tu bila hata kujiuliza madhara ya maamuzi yao.

Kingine cha kulaumu ni maradhi kama Covid19, yametesa na kuumiza dunia nzima. JPM pia alileta maumivu mengi kwa watu wasio na hatia na kwa maoni yao alifanya hivyo kwa kiburi tu cha kibinadamu.

Hakuna rais mkamilifu kwani kwa bahati mbaya anakuwa na mtandao wa kundi la watu wake wenye ukaribu nae ni hao wanaosababisha rais apendwe au achukiwe na watu wa mtaani.
 
Hapana mh Rais hajachangia huu mfumuko wa Bei Bali ni Hali iliyoikumba Dunia nzima, Kila mmoja kwa nchi take anajitahidi kuweka juhudi za kusaidiaa nchi take, katika juhudi hizo Mh Rais wetu amekuwa mstari wa mbele juu ya kupambana na mfumuko wa Bei hasa kwenye mafuta, lakini pia kupitia serikali yake amekuwa akiangalia tozo zisizo na ulazima katika baadhi ya vitu kuzipunguza au kuziondoa ili kuleta ahueni ya Bei, Tuna kila sababu ya Kuendelea kumuunga mkono Rais wetu mpendwa mwenye baraka zote za watanzania wapenda maendeleo na wazalendo wa nchi hii
 
Hata HIVYO labda KWa ambao ni wageni na ziara hizi pale ukiona sehem flani anaenda kuhutubia jua watu wametoka almost kila wilaya kujaza vichwa, utaona watu wengi lakini sio wa sehem husika wengi hukodishiwa mpaka mabasi fika alipo,
Wakati huo unakuta week 1 au 2 kabla team chahwa wapo busy andaa watu kusifu na kupongeza,
Bila ayo kufanyika uwanjani utamkuta na watu mia ambao ni labda ni viongonzi, kwa ground, Mambo ni magum Sana KWa ccm na viongonzi wake
Hakuna kitu Kama hicho Bali watanzania wanakwenda kwa mafuriko kumlaki Rais wetu kwa kufurahishwa na utendaji wake unaoacha Alama, Rais ukienda kila eneo utakufa mikono take katika uwekezaji wa pesa ili kuboresha huduma au kuweka miundombinu, Nenda kwenye elimu,Afya,maji N,k utakufa na kuona namna Rais wetu anavyochapa kazi katika kutoa majibu kwa maswali ya watanzania
 
Kusema kuwa Rais JPM aliuwawa na kundi la watu ni kuendekeza habari za vijiweni, ni kuugeuza uongo ili uonekane kama ni ukweli. Hakuna ushahidi wa uhakika kabisa unaoweza kueleweka ukiwekwa wazi wa tukio zima la kuondoa uhai wa JPM ni minong'ono inayotokana na mapenzi yao makubwa waliyokuwa nayo kwa hayati.

Hakuna rais mwenye jeuri ya kumfurahisha kila mtanzania huyo hayupo. Pia hakuna rais mwenye kuchukiwa na kila mtanzania, huyo hayupo. SSH anafanya mengi ambayo hayati hakuweza kuyafanya. JPM alifanya mengi ambayo SSH hata ndotoni mwake hawezi kuja kuyafanya.

Wote wawili ni nafsi zilizotoka kwa muumba, hivyo kwa namna moja au nyingine zinatufaa katika suala zima la uongozi.
Sasa SSH anafanya nini, ? We sema kuongeza tozo, ziara Kama zote, royal tour ambayo wanaofaidika ni wachache kuliko nchi, teua tengua huku nyuma wapambe wapo anaupiga sijui mwingi, tofauti na hapo hakuna jipya,
Kama ni kukopa endeleza miradi anakopa Kama kipindi Cha mwendazake

Tatizo ni Kwamba Ccm mnawahalibu Sana viongonzi watokanao na chama chenu, mnawajaza kichwa KWa sifa uchwara, nao kujiona wanaweza na wanafanya vizuri kumbe sivyo, Ili mpige vizuri, lakini ukweli kwenye nafasi hii uyu kiongonzi anapwaya Sana, ila so far yuko pale hamna namna lakini hata kwenye kolido huko juu wanajua tu
 
Yani Hawa jamaa sijui Wana matatizo GANI kwenye bongo zao, mbona anasifiwa utendaji ni wa kawaida sana
Utendaji wa Rais Ni mkubwa Sanaa na siyo Kama unavyosema kuwa Ni wakawaida, kila eneo unakuta Alama za mh mama Samia suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kuona nchi hii inasonga mbele kwa Kasi kubwa, Tumpe pongezi mh Rais wetu, Tumuunge mkono Rais wetu, Tumpe ushirikiano Rais wetu na Tuzidi kumwombea ili mwenyezi Mungu aendelee kumlinda na kumpigania
 
Kwan kuna rais TOKA ccm hajawai kuwa na maono, mnasifia mpaka aibu
Asanteeeeeee, Hii ndioo sababu unaona CCM unaendelea kuaminiwa kuongoza nchi hii, ndio maana CCM unaendelea kuwa Tumaini la watanzania katika kuwaongoza na kuwaletea maendeleo, Ndio maana CCM imeendelea kuwa chama kiongozi katika ukanda huu Africa na hata duniani, Imani hii Ni kutokanaa na kwamba CCM unajibu maswali ya wananchi bila shida kwa kutoa utumishi ulio tukuka
 
Sasa SSH anafanya nini, ? We sema kuongeza tozo, ziara Kama zote, royal tour ambayo wanaofaidika ni wachache kuliko nchi, teua tengua huku nyuma wapambe wapo anaupiga sijui mwingi, tofauti na hapo hakuna jipya,
Kama ni kukopa endeleza miradi anakopa Kama kipindi Cha mwendazake

Tatizo ni Kwamba Ccm mnawahalibu Sana viongonzi watokanao na chama chenu, mnawajaza kichwa KWa sifa uchwara, nao kujiona wanaweza na wanafanya vizuri kumbe sivyo, Ili mpige vizuri, lakini ukweli kwenye nafasi hii uyu kiongonzi anapwaya Sana, ila so far yuko pale hamna namna lakini hata kwenye kolido huko juu wanajua tu
Hapana mh Rais wetu Mama Samia anakubalika na watanzania walio wengi sannaaa, amepokea nchi Kama Rais katika kipindi kigumu Sanaa kutokanaa na kuzolota kwa uchumi wa Dunia yote, lakini mama ameibeba vyema Tanzania katika mabega yake, Ameendelea kutoa matumaini kwa watanzania kila uchao, Ameendelea kuwa kiongozi wa mfano hapa Afrika kwa Sasa, hakuna mwenye Shaka na mh Rais juu ya dhamira yake njema katika kuijenga nchi hii kufikia Tanzania yenye kudondosha asali katika kila Kaya, kila mtu atakula keki ya Taifa letu ilimradi tu achape kazi
 
Gharama za maisha zimepanda dunia nzima. Wa kulaumu ni watu kama Putin na wababe wengine wanaofikiria ya kwao tu bila hata kujiuliza madhara ya maamuzi yao.

Kingine cha kulaumu ni maradhi kama Covid19, yametesa na kuumiza dunia nzima. JPM pia alileta maumivu mengi kwa watu wasio na hatia na kwa maoni yao alifanya hivyo kwa kiburi tu cha kibinadamu.

Hakuna rais mkamilifu kwani kwa bahati mbaya anakuwa na mtandao wa kundi la watu wake wenye ukaribu nae ni hao wanaosababisha rais apendwe au achukiwe na watu wa mtaani.
Hapo ndipo mnakosea sana. Yaani wewe kama ndiye upo karibu na Mh. Rais na ndiye mshauri wake basi mnampotosha sana. Ushahidi wa wazi ni kuhusu COVID-19 ambapo Dkt Magufuli alisimama tofauti na hicho unachodai ni kila sehemu na tulivuka salama bila kuathiri maisha yetu ya kawaida. Na ndivyo ilivyo kwa sasa, Uongozi wa Mh. Rais Samia unachukiwa mno si kwa sababu umehamashisha na unaendelea kuhamasisha gharama za maisha kupanda kama wewe unavyoamini. Hivi kama leo mafuta ni 3500 je baada ya miezi kadhaa inayo hatutanunua mafuta kwa 6000????
 
Hapana mh Rais wetu Mama Samia anakubalika na watanzania walio wengi sannaaa, amepokea nchi Kama Rais katika kipindi kigumu Sanaa kutokanaa na kuzolota kwa uchumi wa Dunia yote, lakini mama ameibeba vyema Tanzania katika mabega yake, Ameendelea kutoa matumaini kwa watanzania kila uchao, Ameendelea kuwa kiongozi wa mfano hapa Afrika kwa Sasa, hakuna mwenye Shaka na mh Rais juu ya dhamira yake njema katika kuijenga nchi hii kufikia Tanzania yenye kudondosha asali katika kila Kaya, kila mtu atakula keki ya Taifa letu ilimradi tu achape kazi
Nimetoka kwa mchuuza matunda sasa hivi anamchukia sana Rais Samia. Ni zaidi ya mwaka sasa Rais Samia kaonesha uzaifu sana na kadhalilisha wanawake. Nafasi bado anayo ya kubadilika ila kwa huu mwendo alionao 2025 hata CCM hawatampitisha. Maana maoni huku mitaani ni ya ovyo mno! Rais Samia hana maamuzi kabisa, kila kitu anaangalia wengine wanafanyajr badala ya kusema mimi kama kiongozi wa watanzania nifanyeje
 
Hakuna kitu Kama hicho Bali watanzania wanakwenda kwa mafuriko kumlaki Rais wetu kwa kufurahishwa na utendaji wake unaoacha Alama, Rais ukienda kila eneo utakufa mikono take katika uwekezaji wa pesa ili kuboresha huduma au kuweka miundombinu, Nenda kwenye elimu,Afya,maji N,k utakufa na kuona namna Rais wetu anavyochapa kazi katika kutoa majibu kwa maswali ya watanzania
Huo ni upambe , ila ukweli ndivyo ilivyo ,huko aliko kwenye ziara zake, huko Mbeya mda huu kupitia kamati ya maandalizi Kama yupo mmoja wao hapa moyoni anajisemea ,nimewapiga na kitu kizito, utakuta mkutato wake asilimia 75% sio wa pale wamebebwa na mabasi ,malori kuja ongeza vichwa, na akisha toka utashangaa watu wanavyoangaika paramia usafili

Hii uratibiwa na mkoa husika onesha mapokezi ni ya kishindo kumbe sivyo Ili kuficha aibu ya mkoa KWa mfalme, na hii hufanyiaka kila mahala ,
Sasa chukua mtu mfano Kama Mbowe aseme anafanya mkutano popote tz utashangaa watu wanatoka wapi ambao sio wa mchongo,
Ndo hutajua kupendwa na wa watu ni karama kutoka kwa Mungu, ila wa mchongo utawapata so far una pesa , au watu kujipendekeza wapate kile wanataka toka kwako basi, ndo maana mtu anaweza kusimama, kuongea mbele ya Rais , katika speech yake atataja mh rais Mara 50 kidogo, kwani akitaja mh rais 1 na akaendelea ongea na akamalizia mh rais KWa kushukuru mwishoni ina shida GANI, ? Tafsiri fupi nikujipendekeza tu, yani KILA maneno mawili mh rais,mpaka kero
 
Hakuna anayebebwa kwenda kumlaki mh Rais, Rais wetu anapendwaa Sanaa na hakuna ubaya wowote mtu alikuwa kuwa Rais anakwenda katika eneo lake kwenda kumlaki, Sasa wewe unataka watu wasiende kumlaki Rais wetu au unataka Kama Rais yupo mbali na walipo wasipande magarii, Kama watu wapo tayari kusafiri kwenda kumlaki Rais wetu kwanini usijuwe kuwa Rais wetu anapendwaa Sana na watanzania na Wana matumaini Naye makubwa, Kama hapendwi watu wangekwendaje kumlaki, Rais wetu Mama Samia suluhu Hassan Ataendelea kuwa Rais wa mfano ukanda huu na hata akistaafu Ataendelea kuwa mshauri Bora Sana kwa mrithi wake, Mh mama Samia Ni kiongozi kwa kuzaliwa,
 
Hakuna kitu Kama hicho Bali watanzania wanakwenda kwa mafuriko kumlaki Rais wetu kwa kufurahishwa na utendaji wake unaoacha Alama, Rais ukienda kila eneo utakufa mikono take katika uwekezaji wa pesa ili kuboresha huduma au kuweka miundombinu, Nenda kwenye elimu,Afya,maji N,k utakufa na kuona namna Rais wetu anavyochapa kazi katika kutoa majibu kwa maswali ya watanzania

Yaani we unadhani unaongea na watoto wadogo wasiojua ni jinsi gani watu huwa wanajazwa kwenye hiyo mikutano.

Ni hivi, CCM sio chama cha kizazi hiki na iko madarakani kwa sababu za kihistoria na shuruti. Hivyo namna pekee ni kulamisha watu kujaa kwenye mikutano yake, kwa rushwa, vitisho na ghiliba ila kuhadaa umma kuwa CCM inakubalika.
 
Back
Top Bottom