Rais Samia ni kiongozi mwenye maono sana

Rais Samia ni kiongozi mwenye maono sana

Sawa! Ila ashauriwe zijengwe shule Mpya bado wanafunzi wanatembea umbali mrefu ,shule ziwafuate
 
In short mm binafsi namkubali huyu mama. Laiti yule mtu angekuwepo mpaka sasa hii nchi ingekua tayar iko shimoni.

Piga kazi mama, wapiga kelele siku zote hawakosekani nao twawajua ni lile kundi lile.
 
Yaani we unadhani unaongea na watoto wadogo wasiojua ni jinsi gani watu huwa wanajazwa kwenye hiyo mikutano.

Ni hivi, CCM sio chama cha kizazi hiki na iko madarakani kwa sababu za kihistoria na shuruti. Hivyo namna pekee ni kulamisha watu kujaa kwenye mikutano yake, kwa rushwa, vitisho na ghiliba ila kuhadaa umma kuwa CCM inakubalika.
Ndioo CCM inakubalika ndio maana watu wanahiari kusafiri umbali mrefu kimfuata Rais wetu ili wamsikilize hasa pale wanapogundua kuwa msafara wake hautapita katika maeneo yao
 
Sawa! Ila ashauriwe zijengwe shule Mpya bado wanafunzi wanatembea umbali mrefu ,shule ziwafuate
Zitajengwa mkuu ndio hivyo kazi unaendelea kwa Kasi huku maeneo na nyanja nyingine nazo zikiwa zinaendelea kupewa kipaombele Kama vile usambazaji wa maji, ujenzi wa vituo vya afya na zahanati, n,k, kiufupi mama anaendelea kutoa matumaini kwa watanzania, Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu
 
Ndioo CCM inakubalika ndio maana watu wanahiari kusafiri umbali mrefu kimfuata Rais wetu ili wamsikilize hasa pale wanapogundua kuwa msafara wake hautapita katika maeneo yao

Thubutu, hakuna mwenye huo mda mchafu kwa mfumuko huu wa bei. Labda majobless ndio wanaweza fanya huo utoto.
 
Nimetoka kwa mchuuza matunda sasa hivi anamchukia sana Rais Samia. Ni zaidi ya mwaka sasa Rais Samia kaonesha uzaifu sana na kadhalilisha wanawake. Nafasi bado anayo ya kubadilika ila kwa huu mwendo alionao 2025 hata CCM hawatampitisha. Maana maoni huku mitaani ni ya ovyo mno! Rais Samia hana maamuzi kabisa, kila kitu anaangalia wengine wanafanyajr badala ya kusema mimi kama kiongozi wa watanzania nifanyeje
Naona umeamua kumsingizia mchuuza matunda maana hujasema analalamika Nini kwenye hayo matunda yake hayana wateja, nakama hayana wateja amejaribu kuangalia ubora na Bei za matunda take, vipi kuhusu eneo analouzia Ni eneo sahiihii au alikuwa analalamika Nini, maana makosa take hawezi akabebeshwa Rais wetu, kazi ya Rais wetu Ni kuweka mazingira mazuri ya kila mtu kufanya kazi na biashara kwa Uhuru na amani kwa kuweka Sera nzuri na rafiki,
 
Thubutu, hakuna mwenye huo mda mchafu kwa mfumuko huu wa bei. Labda majobless ndio wanaweza fanya huo utoto.
Mfumuko wa Bei Ni kwote ndugu yangu na Wala mfumuko huu haujaletwa na Rais wetu, hata hivyo Rais wetu Mama Samia anaendelea kujitahidi kuzipunguza makali yake kwa kuweka Ruzuku na kupunguza au kuondoa baadhi ya Tozo kwenye vitu muhimu vinavyo gusa maisha ya watanzania walio wengi, Hali ikitulia huko duniani utaona mfumuko wa Bei kwa baadhi ya bidhàa ukishuka wenyewe, maana solo litajibalansi
 
Ndugu zangu Jana katika ziara ya mh Rais wetu inayo endelea huko mkoani mbeya tumemsikia Rais wetu akisema kuwa serikari unakwenda kujenga vyumba vya madarasa Zaid ya elfu nane, kwa ajiri ya wanafunzi wa kidato Cha kwanza hapo mwakani mwezi wa kwanza, ndugu zangu huko nyuma tulizoea kuona maneno haya yakitamkwa mwezi wa kumi na mbili ndio hela heka za ujenzi wa madarasa ulikuwa unaanza ambapo Hadi watanzania wakijuwa wanashangaa iweje kazi ianze saiz ya kukimbizana na ujenzi wakati tulikuwa tunajuwa wanafunzi wangapi wanamaliza la Saba, tuliona namna ma Rc na DC wakishindana kushinda site ili kukamilisha Madara huku mvua nazo zikinyesha, wakati mwingine hata ubora wa madarasa ulikuwa unatoa Shaka kutokanaa na uharaka wa kukimbizana na muda, lakini kwa kuwa Mh Rais Ni kiongozi mwenye maono na dira tayari ameshaliona Hilo na kuliwekea mikakati na Wala hatutaona wanafunzi wakikaa majumbani kusubiri madarasa, maana tayari Rais wetu ameshaweka mikakati ya ujenzi wa madarasa mapema kabisa, Rai yangu Ni kwa wasaidizi wake hasa ma Rc, DC, Ras,Das, Ded na madiwani kusimamia ipasavyo kazi hii na kushirikiana vyema katika maeneo yao bila mivutano na migogoro itakayorudisha nyuma juhudi za mh Rais wetu kipenzi Cha watanzania,Asante mh Rais, Kazi iendeleee
Kwako sawa. Si maono, matarajio, makengo, mafanikio, maisha na yote upendayo si unayapata through her!!? Ni lazima uone hivyo. Sisi 10,000 unapata Lita 2 ya petrol au mchele, sukari kg 3 Unataka kutuambia nini?!
 
Ndugu zangu Jana katika ziara ya mh Rais wetu inayo endelea huko mkoani mbeya tumemsikia Rais wetu akisema kuwa serikari unakwenda kujenga vyumba vya madarasa Zaid ya elfu nane, kwa ajiri ya wanafunzi wa kidato Cha kwanza hapo mwakani mwezi wa kwanza, ndugu zangu huko nyuma tulizoea kuona maneno haya yakitamkwa mwezi wa kumi na mbili ndio hela heka za ujenzi wa madarasa ulikuwa unaanza ambapo Hadi watanzania wakijuwa wanashangaa iweje kazi ianze saiz ya kukimbizana na ujenzi wakati tulikuwa tunajuwa wanafunzi wangapi wanamaliza la Saba, tuliona namna ma Rc na DC wakishindana kushinda site ili kukamilisha Madara huku mvua nazo zikinyesha, wakati mwingine hata ubora wa madarasa ulikuwa unatoa Shaka kutokanaa na uharaka wa kukimbizana na muda, lakini kwa kuwa Mh Rais Ni kiongozi mwenye maono na dira tayari ameshaliona Hilo na kuliwekea mikakati na Wala hatutaona wanafunzi wakikaa majumbani kusubiri madarasa, maana tayari Rais wetu ameshaweka mikakati ya ujenzi wa madarasa mapema kabisa, Rai yangu Ni kwa wasaidizi wake hasa ma Rc, DC, Ras,Das, Ded na madiwani kusimamia ipasavyo kazi hii na kushirikiana vyema katika maeneo yao bila mivutano na migogoro itakayorudisha nyuma juhudi za mh Rais wetu kipenzi Cha watanzania,Asante mh Rais, Kazi iendeleee
Ficha upunguani wako, maana unasifia hata pasipo stahili sifa. Maono pekee aliyonayo ni kusafiri, kengua na kuteua.
 
Ficha upunguani wako, maana unasifia hata pasipo stahili sifa. Maono pekee aliyonayo ni kusafiri, kengua na kuteua.
Anasafiri kwa madhumuni maalumu na hawezi akakaa humu ndani Kama kwamba Tanzania Ni kisiwa, lazima ukutane na viongozi wenzio, lazima pia ujuwe kuwa diplomasia yetu Ni juu ya uchumi kwanza, hivyo ili kufikia lengo Hilo la kuvutia wawekezaji lazima ujenge ushawishii kwa wawekezaji wakubwa kwa kuwashawishi namna ambavyo Sera za nchi yako Ni nzuri, wewe unafikiri Tanzania ipo peke take duniani, unafikiri hakuna nchi inayohitaji watalii na wawekezaji wakubwa, unazani Kuna nchi ambayo haihitaji kuona inazalisha ajira nyingi kwa watu wake kupitia secta binafsi, unazani Kuna nchi haipebdi kuona bidhàa zote zinazalishwa katika viwanda vya ndani, Sasa wewe unafikiri utawavuta vipi wawekezaji wake kwako Kama usipokwenda kuzungumza nao bkwa maslahi ya nchi yako, au unafikiri wanakujaa tu hata Kama hawajuwi mazingira ya kibiashara na kiuwekezaji kisera na hata kisheria, simama Anza kumuunga mkono Rais wetu maaana mama ndio habari ya mjini kwa Sasa, Kama huamini karibu kuangalia ziara take huko mkoani mbeya namna watu wanavyofurika kumlaki Rais wetu, nikachelewa Anza Sasa maana utakonda kwa mawazo yakuona namna watanzania walivyo na upendo kwa Rais wetuu
 
Hakuna anayebebwa kwenda kumlaki mh Rais, Rais wetu anapendwaa Sanaa na hakuna ubaya wowote mtu alikuwa kuwa Rais anakwenda katika eneo lake kwenda kumlaki, Sasa wewe unataka watu wasiende kumlaki Rais wetu au unataka Kama Rais yupo mbali na walipo wasipande magarii, Kama watu wapo tayari kusafiri kwenda kumlaki Rais wetu kwanini usijuwe kuwa Rais wetu anapendwaa Sana na watanzania na Wana matumaini Naye makubwa, Kama hapendwi watu wangekwendaje kumlaki, Rais wetu Mama Samia suluhu Hassan Ataendelea kuwa Rais wa mfano ukanda huu na hata akistaafu Ataendelea kuwa mshauri Bora Sana kwa mrithi wake, Mh mama Samia Ni kiongozi kwa kuzaliwa,
Wewe ni ngumu, kuelewa, KWA sababu ni team worship,mapambio , CCM ni chama ambacho kila mwanachama yupo pale kwa ajili ya fulsa Wala sio kukitumikia chama, na Ndo maana CCM ipo hapo kwa kubebwa na wizi wa kura tofauti na hapo hakuna chama,
Nakwambia Kama hamna chochote hakuna mwanaccm atapanda gari eti kwa hiari na mapenzi ya chama kutoka mbalali kwenda Tukuyu eti kumlaki mwenyekiti wako, LAZIMA pawepo na fulsa, labda tu wale wenye tuvyeo anzia wilaya lakini sio mwanacha wa kawaida,
Kama kweli hu mwanaccm kindakindaki nafikili Hili unalijua Sana tu ,na moyo unakusuta ila LAZIMA utetee, hakuna namna ila ukweli Ndo huo
 
Watanzania hawahitaji wasafirishwe kwa shuruti kwenda kwa Rais wao, Bali huenda kwa hiari yao kwa kuvutiwa na utekelezaji wa mipango mikakati ya kimaendeleo inayoasisiwa na kusimamiwa na mh Rais wetu
 
Watanzania hawahitaji wasafirishwe kwa shuruti kwenda kwa Rais wao, Bali huenda kwa hiari yao kwa kuvutiwa na utekelezaji wa mipango mikakati ya kimaendeleo inayoasisiwa na kusimamiwa na mh Rais wetu
Ipi Iyo , Kama sio anaendeleza Miradi iliyoanzishwa na mwendazake, hata ivyo Iyo pesa hatoi mfukoni mwake, hizo pesa za watanzania yeye yupo pale kuzisimamia KWA niaba yao, iwe kukopa watalipa watanzania, iwe ni tozo wanalipa watz, iwe ni kutoka madin, utalii ,ni mali za watanzania, hivyo
SSH hatoi pesa kama msemavyo ,bali Serikali Ndo hutoa pesa ,ikiidhinishwa na kiongonzi mkuu ambaye ni Rais, KWA niaba ya wananchi,
 
CCM ndio iliyounda serikali,. Hivyo Rais wetu Mama Samia suluhu Hassan anasimamia ilani yetu ya uchaguzi
 
CCM ndio iliyounda serikali,. Hivyo Rais wetu Mama Samia suluhu Hassan anasimamia ilani yetu ya uchaguzi
Sijakataa, ndio anasimamia ,KWA niaba ya wananchi kuanzia kodi zao na kadhalika but Iyo pesa inayaoenda kwenye Miradi bila kujali mnatekeleza ilani, ni kodi za watanzania wote na hatoi mfukoni mwake ,
So hayo mapambio ya sijui Rais Katia,sh flan, rais ametupatia sh.flani yafe Mara MOJA, Rais pesa za kuwapa watanzania anazitoa wapi, Serikali Ndo inatoa pesa sio Rais,
 
Rais atakayeacha alama ni yule atakayeleta katiba mpya bora ya wananchi.
Huyu ndio Rais atakayeacha alama kwenye maisha ya watu wengi hapa Tanzania..

Na Mungu hajamuweka hapo kwa bahati mbaya..

Nasubiria kwa hamu Sana kuona mapinduzi ya kijani na Utalii wa Tanzania..

Achana na mambo ya kuona mapinduzi ya Elimu na kufuta shida ya Maji Tanzania hayo naona ni mambo madogo kwangu..

Takwimu huwa hazidanganyi [emoji116]
 
Sasa SSH anafanya nini, ? We sema kuongeza tozo, ziara Kama zote, royal tour ambayo wanaofaidika ni wachache kuliko nchi, teua tengua huku nyuma wapambe wapo anaupiga sijui mwingi, tofauti na hapo hakuna jipya,
Kama ni kukopa endeleza miradi anakopa Kama kipindi Cha mwendazake

Tatizo ni Kwamba Ccm mnawahalibu Sana viongonzi watokanao na chama chenu, mnawajaza kichwa KWa sifa uchwara, nao kujiona wanaweza na wanafanya vizuri kumbe sivyo, Ili mpige vizuri, lakini ukweli kwenye nafasi hii uyu kiongonzi anapwaya Sana, ila so far yuko pale hamna namna lakini hata kwenye kolido huko juu wanajua tu
Hakuna anayeweza kukulazimisha uone kama anafaa, ni mawazo yako na unayo haki ya kuwa nayo.

Tozo ni za kuendesha nchi, hata USA na Uk zipo tozo tena nyingi tu. Hakuna maisha rahisi rahisi ukiwa juuya uso wa dunia.
 
Hapo ndipo mnakosea sana. Yaani wewe kama ndiye upo karibu na Mh. Rais na ndiye mshauri wake basi mnampotosha sana. Ushahidi wa wazi ni kuhusu COVID-19 ambapo Dkt Magufuli alisimama tofauti na hicho unachodai ni kila sehemu na tulivuka salama bila kuathiri maisha yetu ya kawaida. Na ndivyo ilivyo kwa sasa, Uongozi wa Mh. Rais Samia unachukiwa mno si kwa sababu umehamashisha na unaendelea kuhamasisha gharama za maisha kupanda kama wewe unavyoamini. Hivi kama leo mafuta ni 3500 je baada ya miezi kadhaa inayo hatutanunua mafuta kwa 6000????
Unajua JPM alikufa kifo cha aina gani?. Unajua bei ya mafuta hapo nchi jirani tu?. JPM alisema matajiri wataishi kama mashetani, nadhani unajua kuwa Mo Dewji au Bakhresa anapoteseka wanaoumia ni maelfu ya wafanyakazi wake.

JPM ameshaundoka na hatarudi tena. Aliyepo tuendelee kuishi nae bila ya kurudisha akili na kukumbuka siku tunazodhani zilikuwa njema kumbe kwa baadhi yetu zilikuwa ni ngumu,
 
Dkt Magufuli alisitiza usawa ktk maendeleo, matajiri walizoea kuiba na kudhulumu
 
Dkt Magufuli alisitiza usawa ktk maendeleo, matajiri walizoea kuiba na kudhulumu
Nii kama alishindwa kuwa na mipaka katika kuiweka sawa nchi. SSH anaongea lugha ya kistaarabu na miradi yote aliyoiacha JPM inakwenda kwa kasi ambayo haikutarajiwa.

Tupunguze chuki kwa uanamke na uzanzibari wa SSH, hatukufunzwa na wazee wetu kina Nyerere haya masuala ya chuki na ukabila.
 
Back
Top Bottom