Rais Samia ni kiongozi mwenye maono sana

Inasikitisha sana, yaani mnaona kabisa Rais Samia anavyovurunda na mnajidai kumpa moyo. Ngoja aondoke madarakani yaani nina kuhakikishia atachambwq, kutukanwa na kukejeliwa zaidi ya marais wote, kile alichokiachia kikatokea kwa Dkt Magufuli kitakuwa mara kumi. Na kwa ufupi hakuna anayetaka kumsikiliza kwenye hotuba zake, yaani watu wanazima TV na redio, yaani kwa ufupi Rais Samia hapendwi!
 
Hakuna rais asiyechambwa anapoondoka madarakani. Alichambwa Mkapa ambaye ndiye aliyemuibua JPM sembuse Samia!!.

Alichambwa JK wakisema muda wote yupo angani kumbe alikuwa anatengeneza mazingira ya JKCI pale Muhimbili, na mazingira ya uwekezaji wa Mwendokasi, sembuse Samia!

Samia anajenga shule na mahospitali huko mikoani kwa kasi kubwa, anamalizia miradi yote aliyoachiwa na hayati JPM. Kwake kuja kuchambwa haitakuwa ajabu, utakuwa ni muendelezo tu wa hulka zetu za kinafiki za kitanzania.
 
Hakuna anayeweza kukulazimisha uone kama anafaa, ni mawazo yako na unayo haki ya kuwa nayo.

Tozo ni za kuendesha nchi, hata USA na Uk zipo tozo tena nyingi tu. Hakuna maisha rahisi rahisi ukiwa juuya uso wa dunia.
Binafsi sio mnafiki , na sijawai kuwa mnafiki, pale panapobidi huntetea yoyote bila kujali itikadi ya chama so far nikiona hatendewi haki nitakutetea,
But KWA SSH ukweli ndo huu,
KWENYE kiti kile anapwaya Sana na tena Sana, ni bora ajue hili kuliko kumpaka mafuta kwa Mgongo wa Chupa, hawezi japo anajikongoja , Hili Hata nyie CCM mnajua ila hamuwezi kusema, ila si wanaccm wote bali wale tu CCM Halisi, wengine tupa kule, KWA sifa mnazomwagia, nae anaamini Sasa kiti amekifit kumbe sio , ndo maana unaona bado amekua na shauku ya kugombea tena , KWA kuaminishwa eti anaupiga Mwinyi, mwambieni ukweli,WENDA akaona wapi ajirekebishe, KWA nini anapwaya, why hastahili kutoendelea, full stop,lakin mkikaa sifia tu, Hata agombee 2025 hapati, na akilazimisha atajijua naishia hapa
 
Lazima apongezwe na kutiwa moyo maana wangapi wanapewa kazi ya kusimamia pesa za imma ili zifanye kazi kwenye miradi fulani lakini wanaishia kuzitafuna na kujenga majengo yao binafsi au kwenda kuficha kwenye mabenk ya nje, umesahau akina mabutu seseko aliyejenga majengo ya kifahari huko ufaransa, mh Mama Samia suluhu Hassan anastahili pongezi sana
 
Wewe je unajua tangu awe pale kaisha fanya mangapi yake binafsi na kwa faida ya familia yake binafsi? We sifia upendavyo ni haki yako mengine usijaribu kuyagusa yaache yalivyo tu naishia hapo, wewe unaona Iyo sauti kwamba ndo msafi kuliko viongonzi wengine ndani ya CCM ,hakuna kitu Kama hicho naye anatafuna KWA urefu wa kamba yake
 
Mama kila afanyalo ni kwa maslahi ya watanzania tuu, angalia namna ambavyo mama amekuwa muwazi kwa kila sent ipatikanayo, amekuwa muwazi Hadi kwenye matumizi ya pesa za imma namna zinavyotumika na zinakokwenda kutumika, kwa Sasa kila mtanzania anajuwa anajuwa Nini kinaendelea katika nchi yetu kutokanaa na namna serikali ya mama yetu kipenzi mama Samia anavyoendesha nchi kwa uwazi, kazi iendeleeee, Tumuunge mkono mama yetu mpendwa
 
Kwako sawa. Si maono, matarajio, makengo, mafanikio, maisha na yote upendayo si unayapata through her!!? Ni lazima uone hivyo. Sisi 10,000 unapata Lita 2 ya petrol au mchele, sukari kg 3 Unataka kutuambia nini?!
Suala la mafuta mh Rais anaendelea kulishughulikia ikiwepo kutoa Ruzuku karibu billion Mia moja Hadi Hali itakapo kuwa sawa katika soko la dunia,siyo kwamba serikali ndio imepandisha Bei, Bali ni Hali iliyosababishwa na Vita vya ukrein
 
Wewe ni wale wale tu pinga pinga. Kwa akili za kitanzania rais anayefaa siku zote hayupo, tunapenda mno kulialia.

Unalalamika upo hapa Dar yanayoendelea huko mikoani huna habari nayo. Mapinduzi ya kilimo yanayosimamiwa na serikali ya awamu ya sita huyaelewi, ujenzi mkubwa wa miundo mbinu unaoendelea huna habari nao.

Hakuna wa kukubadilisha misimamo yako.
 
Mwendazake hakufaa kuwa Rais ,huu ni ukweli mchungu,yule alitakiwa kuishia kuwa Waziri au PM Ili aweze kudhibitiwa..

Kumuacha mtu mwenye mihemko na anayeweweseka kwa sifa na kuzitafuta sifa na kulazimisha huku akikataa kukosolewa ni hatari sana kwa Nchi..

Pamoja na kufanya aliyofanya na kujifisia na wapambe wake ila alileta disaster kubwa kwenye uchumi kiasi kwamba angewndelea awamu hii saizi tungekuwa tunajuta.
 
Ujumbe,ni mmoja Rais wetu kwenye kiti kile anapwaya, full stop , wewe unaangalia katika ujenzi wa wamiradi mikubwa tu kwamba ndo nguzo tu ya kiongozi bora? Kiongozi bora hapimwi na kujenga miundobinu mkuu, hivyo ni vitu vya kawaida Sana so far hutoi pesa YAKO mfukoni, namanisha nini nasema labda akibadilika nitakuja kutengua maneno yangu mwenyewe, kwamba angalau but KWa Sasa bado , huwezi nibadilisha maana binadam hufikili tofauti na ndo maana wewe unaona ujenzi wa Miradi ndo KILA kitu KWa kiongozi wa nchi,.
 
Kazi inaendelea kama kawaida, walalamikaji humu ndani ni sehemu ya kutolea dukuduku na kupunguzia hasira.

Kazi inaendelea nchi nzima kwa sasa, maoni hayo ni ya binafsi na yanaruhusiwa. Tena inafanyika nchi nzima ikiwa na amani kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…