Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Ewalaa sasa hapo tatizo sio nyerere ila wenye dhamana ambao wananufaika na mfumo mbovu aliotuachia Nyerere, sasa sisi inabidi tu dili na hawa waliopo tuanze na mama samia.
Nyerere hawezi kukwepa hizo lawama. Kuna waliompinga na mfumo wake mbovu ila alitaka kutawala kidikteta. Nyerere ametupitisha njia mbaya.

 
Unaenda uwanja wa vita kwa mapambano wakati bado hujamjua adui ni nani!?
Vita itakapoanza ndio utashabgaa adui ni yule ambaye ulikuwa upande wako na msaada wako ndio yule ambaye umeelekeza silaha zako kwake.

2025 is around the corner
Amekwishapoteza mwelekeo. Anachofanya sasa hivi ni kujaribu kuwaharibia wengine.
 
Mi nashauri bendi ya muziki ianzishwe rasmi,iitwe 'Samia praise and worship band',na nyimbo za hiyo bendi ziwe zinapigwa kila redio na kila televisheni nchini,kutwa mara tatu.

Isiishie hapo to,mabalozi wote wanaowakilisha nchi nje,wahakikishe wanapata nyimbo za hiyo bendi,haraka iwezekanavyo.

Kwa hali hiyo, KAZI ITAENDELEA kama inavyotakiwa.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake...
Hii iko hivyo hivyo DUNIA NZIMA!!! Hata marekani... Kwani 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 nafikiria tu!!
 
Mimi nina shida neno UPINZANI nalipinga sana. Maana wenyewe ni kuipinga tu serikali. Liwe jambo jema au siyo jema, wenyewe ni kupinga tu. Nadhani ni vyema tukataza upya muktadha na mantiki ya upinzani. Bora tungetumia neno M'BADALA.
Zaidi ya kupinga kwa maneno tu, huwa wanafanya nini kingine? Kwanini maneno tu mnayachukulia ubaya kiasi hicho kuliko ninyi wenye dola mnaofanya "vitendo" kabisa ambavyo vingi ni vya hovyo.

Kwanini mnaogopa kupingwa, mtu akikupinga anakusababishia nini?
 
"Nikijua wewe ni dhidi yangu, siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar"
Hii ni kauli ya kusikitisha kutoka kwa rais wa nchi.

Hivi sheria za kimataifa zinapingana na sheria za ndani, au anayo maana ya sheria zake mwenyewe anazotunga rais na mahakama yake?

Ana maana kwamba sheria za ndani ni zile zinazokubaliana na yeye wakati wote? Au anamaana atapindisha sheria za ndani zikidhi mahitaji yake!

Samia sasa anawaeleza akina Mbowe na CHADEMA yote ukweli mtupu.
Sasa sijui kama bado watakuwa hawmuelewi tena.

Wakati huo huo, na katika pumzi ileile, kiongozi huyo pia anatamka yafuatayo:

" Hakuna nchi inayoendelea bila kuheshimu utawala wa sheria na Haki za Binaadam."

Sasa kiongozi wa aina hii watu watamuelewa vipi?
 
Nyerere kweli alichemka kutuachia huo mfumo wakidikteta ila anaetakiwa kubadilisha ni sisi yeye si tushamzika.
Kenya ni nchi ya kibepari tangu mwanzo, tena ina katiba mpya,, wale kila nyumba ina umeme, maji, na kiwango cha elimu ni 99.9%😂.

Kila kijana ana ajira rasmi,, moi kajitahidi sana kuijenga kenya🤷🏾‍♂️
 
"Nikijua wewe ni dhidi yangu, siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar"
Hii ni kauli ya kusikitisha kutoka kwa rais wa nchi...
We subiri tu.. mi yangu macho,, lakini nasikia fununu wamarekani wataweka no fly zone,, ngoja tuone🤭
 
Mh. Rais usianze kutupoteza hata sisi wapenzi wako ambao bado tunakutetea hata pale unapokosea wazi. Kumbuka umeanza vema kwa kuliunganisha taifa, sasa umesifiwa mgema tembo anaanza kulitia maji.

Kumbuka hata Hayati Magufuli alianza hivi hivi kidogo kidogo na mwisho wake wote tunaujua. Mama hii nchi ni yetu sote, hii nchi ni ya Watanzania wote.

Kwa leo naishia hapa mama, usiku mwema na Mungu akubariki.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake..
Mwanasheria yeyote ambaye ameiva katika Sheria,Huwa na allergy na tawala sizizotenda haki.Katika awamu iliyopita,haki za kibinadamu zilivunjwa zikiwemo kutekwa na kupotea watu na kuwafukuza kazi wenye vyeti feki pasipo malipo ya kazi aliyofanya Ndo kipindi hicho baadhi ya wanasheria walionekana kama wanaharakati
Bahati .nzuri mambo hayo yamepungua utawala wa mama.Kwa hiyo utawala ukiwa wa haki,uanaharakati pia unapungua
 
We subiri tu.. mi yangu macho,, lakini nasikia fununu wamarekani wataweka no fly zone,, ngoja tuone🤭
"No fly zone" ya nini tena mkuu 'Elungata', tena kwa rais kama huyu? Watakuwa wamekosa jambo mhimu la kufanya.
 
Mh rais usianze kutupoteza hata sisi wapenzi wako ambao bàdo tunakutetea hata pale unapokosea wazi.
Kumbuka umeanza vema kwà kuliunganisha taifa sasa umesifiwa mgema tembo anaanza kukutia maji. Kumbuka hata magufuli alianza hvhv kidogo kidogo na mwisho wake wote tunaujua. Mama hii nchi ni yetu sore hii nchi ni ya watanzania wote kwà leo naishia hapa mama usikuwema na Mungu akubariki.
Urais mtamu sana.
 
Back
Top Bottom