Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Sisi ndio uelewa wetu mdogo Rais anaongelea vyama vya kitaalamu hajaongelea vyama vya siasa kama unataka siasa unaingia katika siasa sio kujificha kwenye vyama vya kitaaluma nakufanya harakati. Adui yangu nimshirikishe kwa lipi? aje aharibu apinge kama mpinzani sio kujifanya chama cha wanasheria kama kina Lissu walivyoingia mle kuleta siasa.
Wataalam ndiyo injini ya kuleta maendeleo katika nchi.
Wataalam hawatakiwi kujipendekeza na kuwalamba nyayo wanasiasa.
Mtaalam anapotoa maoni au kukosoa lazima asikilizwe siyo kumchukia au kumuita adui.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Arusha amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake

Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.

Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.

Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.

Mama anataka wanaomsapoti kwenye Mbio zake za Urais 2025 tu.

Nje ya hapo hakuna.

Ni lini Ccm au viongozi wake walishamshilikirisha mtu mwingine kwenye mambo yake?

Rais Samia awe mwazi asizunguke zunguke mbuyu.

Inaonekana Mbio za Urais zinamtesa sana.
 
Maza endelea kupiga hapo hapo kwenye mshono
 
Mama anataka wanaomsapoti kwenye Mbio zake za Urais 2025 tu.

Nje ya hapo hakuna.

Ni lini Ccm au viongozi wake walishamshilikirisha mtu mwingine kwenye mambo yake?

Rais Samia awe mwazi asizunguke zunguke mbuyu.

Inaonekana Mbio za Urais zinamtesa sana.

Mlaumu Nyerere aliyejenga mfumo mbovu
 
Kasema ukikaa ki uadui..sio kila anaepinga adui...sio kila upinzani ni uadui ....adui ni Yule anaepinga kila kitu...mtu analalamika mgao ...akiambiwa tumenunua mitambo ya gesi kuondoa mgao hataki pia ..anataka tusubiri bwawa la Nyerere...sasa watu Aina hiyo ni wazalendo au wanafiki
Kwani Mama kasema anataka wamsapoti kwenye nini?

Hivi ndio kusema Serikali ya Ccm inadhindwa kufanya mambo mazuri sababu ya TLS na taasisi kama hizo?

Mbona visingizio vimekuwa vingi
 
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Arusha amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake

Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.

Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.

Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.

Duh...!, kwa kauli kama hizi, kiukweli kabisa kuna vitu, ili twende salama, Mama lazima asaidiwe, kwa kuelimishwa kuwa ushirikishwa sio hisani, sio favor, sio option, sio choice, ushirikishwaji ni haki, duty and responsibility, yaani ni wajibu!, kama ulivyo utii kwa mamlaka!. Unaweza kuchagua marafiki lakini huwezi kuchagua majirani, ukiisha jikuta unaishi na jirani fulani, ni lazima ushirikiane nae ndipo muishi vizuri.
Sasa leo ndio nimeanza kuielewa hii TLS ya Hosea!.
Duh....!.
Haya...
P
 
Back
Top Bottom